Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,005
- 9,872
Mwandishi wa Habari wa Marekani anayefanya kazi nchini Ukraine ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Irpin, nje ya Kyiv, polisi wamesema.
Brent Renaud, mwenye umri wa miaka 50, alikuwa mwandishi wa habari na mtengenezaji wa filamu ambaye alikuwa akifanya kazi katika eneo hilo kwa muda sasa.
Mkuu wa Polisi wa Kyiv, Andriy Nebytov amesema kuwa alilengwa na wanajeshi wa Urusi. Waandishi wengine wawili walijeruhiwa na kupelekwa hospitali.
Ni kifo cha kwanza kuripotiwa cha mwandishi wa habari wa kigeni aliyeripoti vita nchini Ukraine.
Mmoja wa waandishi wa habari aliyejeruhiwa, Juan Arredondo, alimwambia mwandishi wa habari wa Italia kwamba alikuwa na Renaud wakati waliposhambuliwa.
"Tulikuwa kwenye moja ya madaraja huko Irpin, tukienda kupiga picha za wakimbizi waliokuwa wanaondoka, na tukaingia kwenye gari," alisema katika video iliyochapishwa kwenye Twitter.
"Kuna mtu alijitolea kutupeleka kwenye daraja lingine na tulivuka kituo cha ukaguzi, kabla ya kuanza kutufyatulia risasi. Kwa hivyo dereva akageuza, waliendelea kupiga risasi; Tulikuwa sisi wawili. Rafiki yangu Brent Renaud, akapigwa risasi ... nilishuhudia akipigwa risasi shingoni", alisema.