Brela ni Kizingiti, hawaendani na Kasi ya sasa

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
1,890
2,000
Siku zote nimekuwa ninasoma habari za Brela, lakini nilikuwa sijui kama wana shida kiasi hiki.

Nimeshuhudia mwenyewe. Kuna mtu anasajili kampuni zake tatu, miezi minne sasa bado anasumbuliwa majina. Kuna majina ali propose yalikataliwa ingawa hayakuwa yamesajiliwa (kupitia search) na sababu ya wao kuyakataa ni madai kuwa yalishasajiliwa na mtu mwingine japo hawakutoa namba ya usajiliwa kampuni husika. Baada ya jamaa kuchezesha jina lililokataliwa ili kutofanana na jina la awali, Brela wakataja jina lililopendekezwa awali kama ni kipingamizi cha usajili wa jina lililochezeshwa, kwamba linafanana na jina lile la mwanzo. Lakini jina hili la mwanzo ambalo lilikataliwa ambalo sasa linatumika kukataa jina jipya lililopendekezwa linaonesha lina usajili mpya.

Yote kwa yote mwisho wa siku niwape ushauri mdogo kwa wale mtaodumu na hizo nafasi zenu, maana kwa mwendo huu kuna siku mtatoka hapo:

1. Msiendekeze rushwa.

2. Msifanye usajili wa kampuni au jina kuwa teso na kizingiti cha kufanya biashara.

3. Kabla mtu hajalipia gharama za usajili, pitieni jina kwanza na kulikubali au kulikataa. Mkishalipitisha jina ndipo mruhusu mtu kutengeneza mhuri na kulipia. Hii tabia ya kutaka mhuri utengenezwe kabla jina halijakubaliwa nanyi unaleta usumbufu na gharama zisizo na lazima za kutengeneza mihuri mipya ambayo nayo mwisho wa siku majina yake yana chances za kukataliwa, pia unasumbua kuandika MEMARTS mpya.

4. Sijui ni kweli kuna majina mnayaficha kwenye public au labda mkipendezewa nayo mnayazuia. Kunakuwa hakuna umuhimu wa kufanya search ya jina kisha likaonekana halipo, halafu baadaye unapoomba usajili unaambiwa hilo jina limesajiliwa na baada ya siku kadhaa unaona usajili mwingine mpya unaonekana umefanyika baada ya wewe kuanza maombi.

Nyie majamaa ni hovyo sana.
 
Ntate Mogolo

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
382
1,000

Hawa watumishi wa Brela wanafanya hivyo, kukujengea mazingira uwape rushwa! Rafiki yangu leo amemaliza mwezi wa pili kila jina analoliweka wanalikata, wakati system yao inabainisha kuwa jina hilo halijatumikana mwingine!
 
kyemo

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
571
1,000
hili limenitokea mm,bahat nzuri nimesajili nimefika kuendelea system ikagoma,baada ya cku kupita ikafuta jina langu nikaanza kusajili upya nakuta jina langu tayari lina watu zaid ya mmoja.
imebidi niwe mpole tu.
Cha ajabu wameweka namba zao zaid ya tatu ambazo hazipatikan milele daima.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom