Brela kuomba maoni ya wadau kuhusu Richmond

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Hii kampuni isifutwe mpaka irudishe pesa ilizolipwa shilingi 152 millioni kwa siku kwa zaidi ya miaka miwili ambazo haikustahili kulipwa

Date::9/15/2008
Brela kuomba maoni ya wadau kuhusu Richmond
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

OFISI ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Majina ya Biashara (Brela), inakusudia kutoa fursa kwa wadau mbalimbali watakaokuwa na pingamizi ya notisi ya kuifuta Kampuni ya Richmond Tanzania Limited.

Hatua hiyo inachukuliwa baada kampuni hiyo kushindwa kujibu notisi ya siku 30 ilyotolewa na Brela kuhusu kusudio lake la kuifuta.

Uamuzi huo ni sehemu ya hatua za serikali kutekeleza azimio namba 17 la Bunge, ambalo lilitaka Richmond Development (LLC) ifutwe na baadaye kubainika kuwa kampuni hiyo ilikuwa Marekani na iliyopo katika orodha ya Brela ni Richmond Tanzania Limited.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Estariano Mahingila, alisema wadau hao wataweza kuweka pingamizi au madai yoyote ya kupinga kufutwa kwa kampuni hiyo mara baada ya kutolewa notisi ya kusudui hilo.

Mahingila kwa ufafanuzi, alisema ni vema kutoa fursa kwa wadau ambao watakuwa na madai dhidi Richmond Tanzania Limited.

"Baada ya kuandika notisi kuiarifu kampuni hiyo ya kupoteza sifa kutokana na kuwa na mwanahisa mmoja, hatujajibiwa, kwa hiyo tunakusudia kutoa notisi ya siku 15 kwa upande mwingine (third part)," alisema na kuongeza:

"Ili kama kuna mtu anapingamizi la kufutwa Richmond Tanzania Limited aseme," alifafanua Mahingila.

Alisema: “ inawezekana kuna watu wakasema sisi tunaidai au vinginevyo hivyo, msiifute, huo ni utaratibu wetu, huwa tunatoa fursa hiyo ya mwisho kwa wadau hao na tunakusudia kufanya hivyo wakati wowote."


Uamuzi huo wa Brela unatokana mwanahisa mwingine wa Kampuni ya Richmond Tanzania LTD, ambayo ni Richmond Development (LLC) kumepoteza sifa baada ya kutokuwepo.

Taratibu za kisheria zinaeleza bayana kwamba, ili kampuni iwe hai au kupata usajili inapaswa kuwa na wanahisa kuanzia wawili.

Kumbukumbu za Brela, zinaonyesha kuwa Kampuni ya Richmond Tanzania LTD, ilisajiliwa Julai 13, 2006 ikiwa ni mwezi zaidi ya mmoja baada ya mkataba kuzalisha umeme wa dharurua na serikali, ikiwa na wanahisa wawili ambao ni LLC na Naeem Gire.

Katika mchanganuo huo wa hisa, Gire ana miliki hisa 250,000 na LLC hisa 750,000 na kuanza na mtaji wa Sh1.260bilion.

Sakata la Richmond lilitikisa nchi hasa wakati wa mkutano wa 10 wa bunge la mwezi Februari, baada ya Kamati Teule ya Bunge kuwasilisha ripoti yake ya uchunguzi na hatimaye kutoa maazimio 23 yaliyotakiwa kutekelezwa na serikali likiwano la kuchunguza usajili wa Brela.
 
Back
Top Bottom