BRELA hutumia mchakato upi kutafutia wateja wao majina ya kampuni?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
ninachojua ni kuwa kama mtu anataka kusajili kampuni au biashara yake ni lazima kwanza afike BRELA ili wamsaidie kusach jina kama tayari lipo au la. Mchakato huu unahusisha kuandika barua ya maombi ya kutafutiwa jina la kampuni kati ya majina uliyopendekeza kwenye barua yako.

Tatizo upande wangu linakuja, ni vigezo vipi hawa jamaa hutumia? Unaweza kusach jina kwenye google ukalikuta. Jina hilohilo brela wakalipendekeza liwe jina la kampuni yako.

Wakati mwingine unakuta jina ulilopendekeza halipo google (google kwa sababu is the largest search engine) bado brela wanalikataa na halina kipingamizi chochote.
 
jukumu la kupata jina la biashara/kampuni ni lammiliki wa biashara/kampuni, brela hawahusiki kukutafutia jina la biashara/kampuni

visit thier website
 
jukumu la kupata jina la biashara/kampuni ni lammiliki wa biashara/kampuni, brela hawahusiki kukutafutia jina la biashara/kampuni

visit thier website

tatizo unaishia kwenye taito tu. Soma uzi mzima
 
amkuu nakunukuu; "maombi ya kutafutiwa jina la biashara" hapa ndipo penye hitilafu

nadhani wanachofanya brela ni kuhakiki uwepo wa jina linalofanana na hilo, ukienda kwenye website yao wameelezea mchakato mzima na vigezo vinavyotumika kukubali au kukataa kupitisha chaguo lako la jina la biashara na mifano ya similarity ya majina wametoa pia

just have an indepth visit at brela website

i hope you will grab something
 
unapopeleka maombi brela kichwa cha habari ni REQUEST FOR NAME SEARCH. Sasa sijui unatafsiri vipi hapo.
 
Search ya Brela haifanyiki Google au kwenye search engine kubwa kubwa. Wao wanafanya search kwenye Database yao (index of registration) kama jina unalotaka limeshatumika au linafanana na jina lililokwishatumika.
 
BRELA hawahusiki na majina yaliyopo DUNIANI, zaidi ni Tanzania. Tusisahahu kwamba Google haina kila kitu, majina yaliyomo kwenye Google ni yale tu ambayo wamililki au watumiaji wameamua kuyaweka kwenye internet. Google is Google, just a website with extensive data (but not everything on this world)
 
Back
Top Bottom