Breivik Siyo Mwendawazimu, Ni Aliyeua Watu 77 Nchini Norway Mwaka Jana.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125







Mahakama ya Norway yameamua kuwa Anders Behring Breivik ana akili zake timamu, na imemhukumu kifungo cha miaka 21 kwa kuuwa watu 77 mwezi wa Julai mwaka jana.
Breivik anatabasamu


Upande wa mashtaka ukitaka kupata uamuzi juu ya akili ya Breivik, na angekutikana punguani angewekwa kwenye jela ya wendawazimu kwa muda usiojulikana.Breivik siku zote amekiri kufanya mashambulio ya mabomu na bunduki, bila ya kuonesha majuto.


Amekuwa akishikilia kuwa ana akili yake, na kwamba aliyofanya ni vitendo vya kisiasa.Alitabasamu hukumu ilipotolewa.Wakili wa Breivik amethibitisha kuwa mteja wake hataomba rufaa.


Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
 
I don't think the trial was fair to the families of the victims ,atatoka jela akiwa na 53 and life goes on kama kawa. Huyu ni wakumweka kwenye kiti cha umeme tu,
 
Miaka 21 michache..hukumu haikai kwenye mizani...77 people for 21 yrs?
 
Miaka 21 michache..hukumu haikai kwenye mizani...77 people for 21 yrs?

Na yule wa issue ya Lockerbie, Scotland; aliyeshiriki kulipua ndege na kuteketeza miili ya binadamu wasio na hatia zaidi ya 300, alipewa adhabu gani?
 
Nilikua nafuatilia kesi ya huyu jamaa sio siri wenzetu wanajali sana,walionesha jela zao dah kibongobo unaweza ukatamani usitoke
 
Nchi nyingine raha sana. Yaani mtu unaua watu 77 halafu unahukumiwa kwenda kuishi kwenye nyumba nzuri yenye kila kitu ndani kwa muda wa miaka 21.
Ulaya ndio kwenye sheria unauwa kisha unapimwa kuangaliwa kuwa una kichaa au huna kichaa? ikithibitishwa kuwa una ugonjwa wa kichaa huna kesi la kama hauna Ugonjwa wa kichaa ndio unakwenda jela. mkuu Radhia Sweety
 
Last edited by a moderator:
Ulaya ndio kwenye sheria unauwa kisha unapimwa kuangaliwa kuwa una kichaa au huna kichaa? ikithibitishwa kuwa una ugonjwa wa kichaa huna kesi la kama hauna Ugonjwa wa kichaa ndio unakwenda jela. mkuu Radhia Sweety

Sheria gani hizo za ulaya, majela yao poa na anaweza akasoma huyo akatoka hapo akawa na PhD. Huyu angepelekwa saudi arabia, akapigwa mapanga mara 77....
 
Back
Top Bottom