Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,157
- 17,968
Baada ya Kibaki na Odinga kukubaliana, Waziri Mkuu wa Uingereza bwana Gordon Brown amegusia leo jioni hii kwamba anakusudia kuandaa hafla kwa wahisani mbalimbali wa Afrika ili wajadili namna ya kuiokoa Kenya kiuchumi.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari hafla hio itafanyika mwanzoni au katikati ya mwezi ujao wa March mjini London katika tarehe itayopangwa.
Uingereza na nchi zingine za wahisani pamoja na Marekani hawakupendezwa na utaratibu wa kuibiana kura huko Kenya na kuamua kumtuma mtu mzito Koffi Annan ambae ni katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa.
Koffi alikwenda Kenya kama mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ambayo inajumuisha nchi zote zilizoendela pamoja na Israel ambazo zimehakikisha zinaratibu makubaliano hayo kwa kutumia mawasiliano ya moja kwa moja ama watu kama Condoleeza Rice na baadae bwana Koffi Annan.
Kenya sasa haijulikani imeathirika vipi kiuchumi kutokana na kukosa fwedha za kigeni na kusimama kwa shughuli nyingi za biashara ambazo zilikuwa zililetwa na watalii, ina hamu kubwa ya kukutana tena na wahisani hao ambao watakuwa tayari kurudisha tena shughuli zao za biashara ambazo zilisimama kwa kiasi fulani na kuleta hali ya wasiwasi kwa nchi hiyo kipenzi cha wazungu.
Lakini kwa kufikiwa makubaliano kati ya viongozi hao wawili kuna dalili kwamba shilingi ya Kenya bado iko imara kwa "standard" yake.
Kenya ilikuwa koloni la Uingereza mpaka mwaka 1963 ilipopewa uhuru wake ambao uligawiwa kwa kabila la Wakikuyu ambao walikuwa ndio kipenzi cha wazungu na wachache kiidadi na ndio ambao wamefaidika kwa kiasi kikubwa kiuchumi kwa kuwa na nafasi katika nyanza mbalimbali za uongozi wa nchi hio.
Sasa ni matumaini kwamba katiba itaangaliwa upya na serikali mpya ya mseto ambayo itaipitisha bungeni na kutoa nafasi kwa kila mkenya nae afaidi ardhi, asione ukabila na apate sehemu ya utajiri wa Kenya.
Source: World Media
NB:
Lakini pia nna swali ni kwanini Raisi wa Uganda Mzee Yoweri Kaguta Museveni hajahudhuria mazungumzo hayo? Si ndio baada ya makubaliano ikafanzwa bonge la party ya EAC katika miji yote ya Dar-es-Salaam/Dodoma/Arusha, Nairobi au Kampala?
Je pia unajua maana ya serikali ya mseto? Fuatilia kwa makini video hii ifuatayo:
http://article.wn.com/view/2008/02/...oalition/?template=africadaily/topstories.txt
Naomba tuchangie mawazo.