Breaking news: Watu 6 wahofiwa kufa mkoani Lindi baada ya kufunikwa na kifusi mgodini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Breaking news: Watu 6 wahofiwa kufa mkoani Lindi baada ya kufunikwa na kifusi mgodini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by cjilo, Sep 6, 2012.

 1. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  PICHA 2.jpg
  watu wapatao sita wahofiwa kufa baada ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa chimbila (mnacho) wilayani ruangwa –mkoani lindi.
  Jitihada za kuwaokoa watu hao zimekuwa zikiendelea japo zinaendelea kufanywa katika hali ya ugumu kutokana na ukosefu wa zana/vifaa vya kuokolea.
  Hadi muda huu kufuatia harakati hizo ni maiti moja tu ndio imeweza kupatikana
  source: Blog ya issa michuzi
  my take: Ajali huwa tunasema inapangwa na mungu, sasa hata vyombo vya uokoaji kwetu bado ni tatizo kila sekta, kuanzia ya uvuvi mpaka ya madini, jamani tutapona kweli?
   
 2. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mwe! Mungu tunusuru weeeeee! Mbona maafa tu kila siku kila siku, au kuna mkono wa mafrimasoni?
   
 3. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Pumzikeni kwa amani ndugu zetu 6 wa Lindi. Hivi hawa viongozi wanafanya kazi gani kuzuia vifo vya kizembe namna hii? Watu wengine bwana.
   
 4. ketwas

  ketwas JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 213
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  waseme chadema nayo imehusika tena huko lindi,waunde tume za ulaji
  MUNGU WAREHEMU WALIOKUFA NA WAFIWA
   
 5. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hivi hakuna sheria inayowabana makampuni kuwa huwezi anzisha shughuli bila ya kuwa na vifaa vya uokoaji pindi ajali inapotokea? Sijasomea sheria lakini hii kitu nafikiri lazima iwepo jamani...Kwa hivyo ndo uone kuwa rushwa ni ufisadi ni adui wa uhai, watu wamepokea mlungura wakaruhusiwa kuanzisha machimbo hayo bila kufuata sheria...
  Mungu tuokoe na haya majanga sie makosa sio yetu bali ni ya mafisadi wa ccm
   
 6. awp

  awp JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huko lindi kuna madini gani jamani? poleni sana wafiwa
   
 7. peri

  peri JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  poleni sana wafiwa,
  Mwenyezi Mumgu atunusuru.
  Inasikitisha hakuna vifaa vya uokoaji, soo sad.
   
 8. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  hizi sheria zipo na nadhani na wewe unazijua. Mfano mzuri ni kuwa kila gari (chombo cha moto) iliyosajiliwa kihalali inabidi iwe na fire extinguisher "faya tingisha" lakini kama unavyojua mfumo wa utawala Tanzania umeshavurugika kutokana na kutokuwa na wasimamizi wa sheria na kanuni. Waliopo ndio wanaongoza na kusaidia uvunjaji!
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Poleni sana wafiwa na Mwenyez Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Poleni wafiwa.
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  so, unauhakika hao ni waajiliwa wa kampuni?, je kama ni wachimbaji binafsi?!
   
Loading...