Breaking News:Tanesco yapigwa chini kesi ya Dowans

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Katika hukumu yake yenye kurasa zaidi ya 100.Jaji Mushi wa Mahakama kuu,ametupilia mbali maombi ya Tanesco katika kuipinga tuzo iliyotolewa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi.Ninatafuta nakala ntaiweka baadae.
 
Katika hukumu yake yenye kurasa zaidi ya 100.Jaji Mushi wa Mahakama kuu,ametupilia mbali maombi ya Tanesco katika kuipinga tuzo iliyotolewa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi.Katika hukumu yake hiyo ameeleza kuwa hakuna sababu hata moja yenye kuonesha kuwa kulikuwa na upotoshwaji wa aina yoyote uliyofanywa na wasuluhishi.Ninatafuta nakala ntaiweka baadae.

Tutashukuru sana kwa nakala ya hukumu
 
DU! inamaana yale mabilioni tutayalipa? Tumekwisha nahisi bei ya umeme inapanda soon.unit moja inakimbilia elfu tano mda si mrefu.
 
Jaji kateuliwa na Rais....Rais 'hawajui' wamiliki wa Dowans....Dowans inashinda kesi
 
Katika hukumu yake yenye kurasa zaidi ya 100.Jaji Mushi wa Mahakama kuu,ametupilia mbali maombi ya Tanesco katika kuipinga tuzo iliyotolewa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi.Ninatafuta nakala ntaiweka baadae.

Ulifikiri Rostam mjinga kukubali kwenda kuipigia kampeni CCM Igunga siku ya uzinduzi jimbo ambalo alikuwa analishikilia mwenyewe? Mwenye akili haambiwi fikiri na mwenye macho haambiwi ona! Siasa za Bongo ni uozo mtupu ila kiama chao kinakuja!
 
Jaji ameamuru hiyo tuzo isajiliwe haraka na Dowans walipwe chao.
 
DU! inamaana yale mabilioni tutayalipa? Tumekwisha nahisi bei ya umeme inapanda soon.unit moja inakimbilia elfu tano mda si mrefu.

Alishasema Pinda kwamba December bei ya umeme juu! Alikuwa anajua alisemalo! Ila kiama chao kinakuja!
 
Jaji ameamuru hiyo tuzo isajiliwe haraka na Dowans walipwe chao.

I stand to be corrected, kesi nyingi ( si zote tafadhali) za High court zikienda Court of appeal huwa zinashindwa. Hivyo hukumu hiyo siyo conclusive.
 
hapana aisee haiwezekani wakina lowasa na wenzie walipwe wakati watanzania 2nakufa njaa, umeme hakuna pesa hakuna hlf wanalipana mabilion aisee. BWANA HAPA PANAHTAJIKA NGUVU YA UMA.
 
TANESCO walishakubaliana na DOWANS kwamba purukushani lolote na kisheria likitokea wataenda kushitakiana kwa arbitrators nje ya nchi, kwa maneno mengine, walishadharau mahakama za kwetu, wameenda huko wameshindwa ndio wanarudi kwenye mahakama zetu zitengue hukumu? Jaji amekataa ushenzi na dharau hiyo ya TANESCO, kasema eff that!.

Nina hakika asilimia 99.9 kwamba Jaji lazima ndivyo alivyosema, "mlitaka wenyewe kwenda kushitakiana nje ya nchi, yamewashinda ndio mnaniletea mimi, kwendeni zenu huko." Honorable Judge, great job.
 
'Tanzania ni zaidi ya unavyoijua' ...katika ili suala itabidi nasi tujue ni nini hicho kilicho zaidi ili historia isije kutukumbuka kama Dinosaurs!
 
TANESCO walishakubaliana na DOWANS kwamba purukushani lolote na kisheria likitokea wataenda kushitakiana kwa arbitrators nje ya nchi, kwa maneno mengine, walishadharau mahakama za kwetu, wameenda huko wameshindwa ndio wanarudi kwenye mahakama zetu zitengue hukumu? Jaji amekataa ushenzi na dharau hiyo ya TANESCO, kasema eff that!.

Nina hakika asilimia 99.9 kwamba Jaji lazima ndivyo alivyosema, "mlitaka wenyewe kwenda kushitakiana nje ya nchi, yamewashinda ndio mnaniletea mimi, kwendeni zenu huko." Honorable Judge, great job.

Sasa wewe unachofurahia ni nini?au unafikiria wewe hauhusiki na ulipaji wa hilo deni?endelea kufurahia wakati upande wa pili unaumia.
 
TANESCO walishakubaliana na DOWANS kwamba purukushani lolote na kisheria likitokea wataenda kushitakiana kwa arbitrators nje ya nchi, kwa maneno mengine, walishadharau mahakama za kwetu, wameenda huko wameshindwa ndio wanarudi kwenye mahakama zetu zitengue hukumu? Jaji amekataa ushenzi na dharau hiyo ya TANESCO, kasema eff that!. Nina hakika asilimia 99.9 kwamba Jaji lazima ndivyo alivyosema, "mlitaka wenyewe kwenda kushitakiana nje ya nchi, yamewashinda ndio mnaniletea mimi, kwendeni zenu huko." Honorable Judge, great job.
yani wewe ni kiazi
 
Watu wanagawana tu.....na huyu atakuwa kashikishwa hela 'ndefu' tu!
 
Wakuu...Mtu wa kwanza kutamka kwamba lazima tullipe hili deni alikuwa mwanasheria mkuu wa sirikali, akafuatiwa na bwana mdogo Ngereja..anzia hapo utapata picha......wa TZ tunauliwa tena kwa mkusudi ..let us think together.....lets talk ...speak out what we have...nasubiri mkuu atuwekee tuweze kudadavua jaji kasemaje
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom