Breaking news: Rais Uhuru Kenyattta Atangazwa Rasmi Kuwa Mshindi Katika Marudio Ya Uchaguzi Kenya

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,082
2,000
image.png
Tume ya uchaguzi Kenya kupitia Mwenyekiti wake Ndugu Chebukati wametangaza rasmi Rais Uhuru Kenyatta mgombea wa chama cha Jubilee kuwa ni mshindi wa uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini Kenya tarehe 26th October 2017 kwa kupata kura milioni 7400000. Chama cha upinzani cha NASA kiligoma kushiriki uchaguzi huo. Mabalozi wa Jumuia ya Ulaya, Balozi wa Marekani na waangalizi wa kimataifa wakiwemo na Rais wastaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na Paul Banda wa Zambia wamehudhuria tangazo la tume ya uchaguzi katika makao makuu yao yaliyopo Bomas of Kenya. Tume hiyo imeendelea kutangaza ushindi wa Rais Uhuru Kenyattta licha la kutofanyika kwa uchaguzi kwenye majimbo manne yaliyopo jimbo la Nyanza.
Uchaguzi wa kwanza ulifanyika tarehe 8th August 2017 na Mahakama kuu ya nchi hiyo ilitengua matokeo ya uchaguzi huo uliokuwa umempa Rais Uhuru Kenyattta ushindi baada ya kugundulika taratibu zilikiukwa kwenye uchaguzi huo.
Rais Uhuru Kenyattta anategemewa kuapishwa na Jaji yeyote kwa mujibu wa mabadiliko ya katiba yaliyofanywa hivi karibuni na bunge la nchi hiyo.
 

mlimilwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,370
2,000
Wamenifurahisha Hapo kwenye 43000 keshi.
Hesabu kama hizo zinakuaga na shaka.
Haiwezrkani isiwe na mamia wala mamoja.
 

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
909
1,000
Wamenifurahisha Hapo kwenye 43000 keshi.
Hesabu kama hizo zinakuaga na shaka.
Haiwezrkani isiwe na mamia wala mamoja.

Africans sijui kwanini hatujui kupika data!! Hakuna data kama hii 43,000 katika uchaguzi!!! Haiwezekani!!!!
Huu nao ni Wizi mwingine wa kura na demokrasia kwa wananchi wa Kenya.!!
Period!!
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,247
2,000
Hongera sana Mh. Uhuru Kenyatta. Tangu jamaa alipochagua upande waziwazi nilimdharau jumla. Alitaka kuintroduce dictatorship in Kenya; ashindwe. And luckily, nyakati zake ni kama zimekwisha hatoinuka tena.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,247
2,000
Africans sijui kwanini hatujui kupika data!! Hakuna data kama hii 43,000 katika uchaguzi!!! Haiwezekani!!!!
Huu nao ni Wizi mwingine wa kura na demokrasia kwa wananchi wa Kenya.!!
Period!!
Tatizo nini? Hiyo sio numba? Isn't it in the valid range? Sijaelewa mantiki yako nini hasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom