Breaking News: Polisi wakataza mkutano wa Chadema Arusha leo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Breaking News: Polisi wakataza mkutano wa Chadema Arusha leo.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mu-sir, Dec 22, 2010.

 1. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Kamanda wa polisi ametoa tangazo la kukataza mkutano wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kwa sababu zifuatazo. 1. Taarifa ya chama hicho kwa polisi imetolewa chini ya masaa 48 kwa mujibu wa sheria. 2. Barua ya chama hicho kwa polisi haikuonesha madhumuni ya mkutano huo. 3. Kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia zinaonesha kuwa hali ya usalama ni tete kwa kuwepo kwa mipango ya baadhi ya vijana kuvunja maduka na kuiba mali. OVER Source. Live interview with clouds fm.
   
 2. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuwa upinzani aimaanishi wewe ndo kila kitu,naomba wafuate sheria
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wakifanya mkutano CCM nao huwa wanafuata sheria kweli?
   
 4. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  polisi wanakuza mambo bila sababu , madhumuni ya mkutano wa hadhara wa kisiasa ni obvious kuongea na wananchi , hao wanaotaka kuiba hawatakuwa walengwa wa mkutano au walikuwa wafanye maandamano na mkutano unaisha saa kumi na mbili maduka yamefungwa intelligence ya tz bana .
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  source????
   
 6. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  mfumo wetu bado ni wa chama kimoja, na ndiyo maana huwezi kusikia mbunge au diwani wa CCM kapigwa virungu na police - kukuhakikishia hilo yule mgombea ubunge aliyemlamba makofi OCD uliona hatua gani alichukuliwa? angekuwa wa chama cha upinzani nafikiri wangemvunja mbavu.

  Tatizo si mapolice tatizo ni mfumo.
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Eti taarifa za kiintelijensia, intelijensia my ass hakuna lolote badala ya kufanya uintelijensia kwa manufaa ya nchi kazi yao ni kuhujumu tu vyama pinzani too cheap
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Uwe unasoma kwa umakini thread before haujauliza source
   
 9. semango

  semango JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  maadili ya polisi mkoa wa arusha hayapo tena kwa sababu hakuna uongozi mzuri.kuna ma-mbumbumbu tu wanaongoja kupewa amri ili watekeleze.
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwenu wanajamvi.

  Ikiwa sheria inaelekeza chama kutoa taarifa masaa 48 sioni kosa la polisi CHADEMA wanatakiwa kutoa notice nyingine itakayokidhi matakwa ya sheria na kanuni hakuna haja ya kuendeleza malumbano wakati ipo fursa ya kurekebesha kasoro.Hoja ya pili kidogo inanitatiza kidogo sioni umuhimu wa kueleza maudhui ya mkuto polisi.Polisi kazi yao kubwa ni kulinda usalama wa mali na watu na inapaswa wajue CHADEMA ni chama halali cha siasa kina wajibu wa kuwaambia chochote wanachama na wapenzi wake.Hoja kwamba wanazo taarifa za kiiteligensia zinazo onyesha kutakuwa na hali tete ya kiusalama.Hii hoja inaweza kutumiwa vibaya na jeshi la polisi wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanawakamata watu wote waliopanga kujiushisha na vitedo vya uvunjifu wa amani.
   
 11. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Polisi kutokuelewa wajibu wao ni matokeo ya Katiba mbovu kwani bado tupo katika Katiba mbovu.
   
 12. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu sidhani hata kama wanaomba kibali, unakumbuka kwenye kampeni JK alikuwa anazidisha mda hadi saa moja usiku, Jemadali wetu Dr. Slaa kalalamika hadi akachoka akaamua na yeye kuzidisha mda, Tendwa akalikoroga ili kumtetea boss wake.

  Hakuna tofauti ya Serikali na CCM. na polisi wanatekeleza matakwa na maagizo ya serikali ambayo ni CCM
   
 13. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tatizo Chadema kuna wahuni wengi. Na hii inasababisha chama hicho kishindwe kuweka mikakati mizuri ili kuweza kufanikiwa. Na hii ndiyo iliyopelekea wakapigwa bao la kiupuuzi kule Arusha. Wakiamua kufuata sheria maamuzi yatatolewa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mwingine.

  Chama kisicho na mwelekeo wala dira kama ilivyo Chadema ni sawa na genge la wababaishaji.
   
 14. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu unajichanganya na pia umenichanganya.
  CCM (SERIKALI) siku zote imekuwa inawaita wahuni wate wote wanaojitokeza kudai haki zao, na kwa Kutumia Kikosi cha Kupambana na Mawazo Mbdala (KIKUWAMBA) wao wanawaita FFU wamekuwa wakiwapiga, kuwadhalilisha wananchi na raia halali wa taifa hili. Iwe ni wanafunzi, watanyimwa mikopo miezi nenda rudi wakilalamika, utasikia hilo ni genge la wahuni wachache wanaotumiwa na vyama vya upinzani.
   
 15. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  ...kanyafu nkanwa,kwa CCM yeyote anayedai haki yake inayodhulumiwa na CCM ni 'mhuni'. hata wewe it is matter of time,kwa sasa kula makombo ya hao mafisadi ila siku ukifunguka macho ukaona unavyoibiwa na kudai haki yako utaunganishwa kundi la wahuni nasi 'wahuni' wa kudai haki tutakukaribisha. by the way, jina lako kwa lugha yetu ni tusi kubwa saaaaaaaaaaaaana! je linachangia kuwa na akili hiyo?
   
 16. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Polisi ni idara,inayofanya kazi zake kiusanii kuliko idara zote za serikari, siasa na longolongo tupu zimewajaa makamanda wake, ukitaka ufanikiwe jipendekeze' uhalifu unatokea utasikia upelelezi wa kiitelenjesia unaendelea. Watuhumiwa wengi wanabambikiwa kesi huku wahusika wanapeta uraiani. Laana za mwenyezi mungu zinawasumbua viongozi wengi wa polisi pale wanapostaafu wanakufa mapema. Hata wafanye jambo gani katika maisha hawafanikiwi .
   
Loading...