Breaking News: Muda wowote kuanzia sasa Mtangazaji Machachari na mwenye Maneno ya Shombo Antony Nugaz wa CMG atatangazwa kuwa Msemaji wa Yanga SC

Ndugu yangu Haji Manara ( Msemaji wangu wa Simba SC ) nadhani sasa kwa huyu Msemaji mpya wa Yanga SC Mtangazaji Antony Nugaz wa Clouds Media Group ambaye muda wowote kuanzia sasa atatangazwa na Uongozi wa Yanga itabidi ujipange kwani kama ni maneno ya Shombo, ya Karaha, Kuudhi na Utoto wa Mjini huyu nae anao tena sana tu hivyo niseme tu mapema Kwako kuwa sasa umempata Mbabe wako.

Sitegemei sasa kuwaona mkicharurana kwa ' Madhaifu ' yenu Binafsi kwani najua mtaharibiana bure na kuharibu hata Taswira ya Vilabu vyenu hivi viwili vyenye nguvu na ushawishi mkubwa hapa nchini. Hakuna Mtoto wa Mjini ambaye halijua tatizo binafsi na Antony Nugaz na pia hakuna Mtoto wa Mjini asiyejua tatizo binafsi la Haji Manara hivyo nawaombeni mkiwa mnacharurana yawe tu ni Matani ya Kunogesha Upinzani wetu wa Jadi na siyo Kuchafuana japo nikiri wazi kabisa kuwa ukiweka katika Mizania tatizo binafsi alilonalo Antony Nugaz ni baya zaidi kuliko lile la Haji Manara.

Nikiwa kama mwana Simba SC na Mwanamichezo nimependa huu Ujio wa Msemaji mpya wa Yanga SC Antony Nugaz kwani utamfanya sasa Msemaji wa Simba SC asibweteke na asijione kuwa Yeye pekee ndiyo Mbabe wa Mdomo ( Maneno ) badala yake anatakiwa sasa ajipange vyema vinginevyo asije Kushangaa anazidiwa na Nugaz kwa mbali mno.

Kitu pekee ambacho nina uhakika nacho kuwa Klabu ya Yanga SC ( Watani zangu ) watafaidika na Msemaji wao huyu mpya Antony Nugaz ni kwamba Jamaa ukiachia mbali kuwa nae ana maneno mengi tena yale ya Shombo, Karaha na Kuudhi pia ni Mbunifu mzuri wa Kampeni za Maendeleo hivyo huenda uwepo wake hapo Yanga SC ukawa na Faida Kubwa na Kuitangaza Yanga SC vyema na pia kuisababishia Kuizidishia Mapato vile vile.

Pole sana kwa akina Hemed Kivuyo wa ITV na Radio One kwa Kuikosa hii nafasi japo natambua uliitaka sana tu ila Kutojiamini Kwako na Kusitasita ndiyo Kumekuangusha kwani nakumbuka hata Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC Fredrick Lugano Mwakalebela kwa Kukuheshimu alishakufuata hadi hapo Ofisini Kwako na kukuita ndani ya Gari lake na mkaongea kisha akakupa Mkataba wako Uusome na kama ukishindwa basi umuhusishe Mwanasheria wako na Wewe ukampa Mwanasheria wa hapo Ofisini Kwenu akusaidie Kuutafsiri lakini cha Kushangaza huku ukidhani kuwa Yanga SC inakuhitaji mno ukawa unawaringia na hata kuna muda ukawa hupokei Simu zao hatimaye sasa wamekutosa rasmi na utaendelea Kusota hapo ITV na Radio One ambapo Mishahara yenu huwa mnapewa kila baada ya Miezi Minne Minne au hata Mitano Mitano wakati ungekuwa Yanga SC Umasikini ndiyo ungekuwa bye bye Kwako.

Karibu sana Antony Nugaz ndani ya Yanga SC kama Msemaji ( Afisa Habari ) wao mpya.
Kwa hiyo kupata Msemaji huyo tutarajie mini Makombe au maneno na matusi?
 
Back
Top Bottom