Breaking news: Mechi ya Simba na Yanga kutochezwa leo?

Status
Not open for further replies.

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
125
Taarifa zinazojiri hivi sasa ni kuwa ule mpambano wa Simba na Yanga leo upo hatarini kuakhirishwa baada ya kutokea utata kwenye tiketi za mchezo huo. Utata huo umesababishwa na viongozi wa Yanga kwa kuweka muhuri wenye aya za Quran na kupelekea wanaharakati na viongozi wa Kiislam kutaka ziondolewa mara moja kwani tiketi hizo hizo upande wa pili zinatangaza pombe.

Shirikisho la soka Tanzania ( TFF ) kwa kushirikiana na vilabu hivi viwili walikubaliana kila timu iweke alama katika tiketi ili kuepusha uwezakano wa kughushi tiketi. Simba wakaweka alama yao lakini viongozi wa Yanga wakaamua kuweka alama ya mojawapo ya sura ktk quran tukufu na kupelekea mtafaruku huo ulioanza jana.

Hadi wakati tukienda mitamboni nusu ya tiketi zilikuwa zimeshauzwa na waislam wametangaza leo kwenda kufanya fujo uwanja wa taifa kama tiketi hizo zitatumika.

Kwa upande wao Bakwata nao wametoa tamko kutaka mechi hiyo iakhirishwe na tiketi zingine zitengenezwe.

Akiongea na mwandishi wetu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Imani Madega amekiri kweli wameweka aya za quran tukufu kwenye tiketi lakini amedai wamefanya hivyo kwa nia njema kabisa kuwafanya wanaofoji tiketi waone vibaya kufoji mpaka quran tukufu.


Wakuu habari ndio hiyo! kandambili washalikoroga....
 
Nimetune Radio Sauti ya Quran 104.1 Fm. Wanawasisitiza waislamu waende mpirani kwa wingi ila wasiingie uwanjani. Pia wanalaani tamko la Baraza la Maaskofu.
 
Mimi nadhani ifikie wakati watanzania tujifunze kuwajibika.kwa mfano kuna ubaya gani mwenyekiti wa yanga na kamati yake wakijiuzulu ili kuonyesha uwajibikaji katika suala hili.hebu fikiria kama tiketi zimeuzwa nusu ina maana watu zaidi ya elfu 30 watapoteza muda na pesa zao.kibaya zaidi kwa ajili ya mchezo huu kuna watu wamesafiri toka mikoani mwanza,moro,mbeya,arusha etc kwa gharama kubwa kuja kuangalia mechi.this is cantankerous!
 
Na ni kwanini wahusishe dini na michezo hali wakijua kuna dini zaidi ya moja! wamelikoroga na walinywe!
 
na kwa taarifa tu mvua imeshaanza kunyesha maeneo ya uwanja wa taifa.
 
Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mh Kandoro mchana huu na kuhudhuriwa na viongozi wa Bakwata. Viongozi wa Yanga wakiongozwa na Madega wamewaomba radhi waislam na Bakwata imekubali tiketi zitumike hivyo mechi ipo.

Hata hivyo wanaharakati wa kiislam wamesema wataenda kufanya fujo tu kwani Bakwata hawaitambui na ni chombo cha serikali.

Lets wait and see
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom