Maandamano makubwa chuo kikuu Mkwawa

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Hivi sasa mji wa Iringa unazizima kwa maandamano ya wanachuo kikuu kishiriki cha Mkwawa kwenda kwa mkuu wa mkoa kisa hawajaingiziwa fedha zao,HII NI HAKI KWELI WAKATI MAMILIONI YA KODI ZETU YANALIWA NA WACHACHE SERIKALINI?
 
Haya yametokea pia duce,hapo wanafunzi wakiandamana kuelekea getini kuzuia magari yanayotoka mbagala-kawe na mwenge kushinikiza ombi lao!
 
Usishangae wakipigwa mabomu hao na WEZI wa hela zetu wakipeta kama Mawaziri
 
Attachments

  • Duce-001.jpg
    Duce-001.jpg
    79.3 KB · Views: 92
hii serikali ya ajabu sana huku UDOM inabidi hela tuingiziwe alhamisi ijayo tarehe3/5,lakini hadi leo kwa utaratibu wa siku hizi hadi tusaini fomu,na ipite hata wiki mbili baada ya kusaini,mpaka leo hakuna hata dalili za kusaini
 
Hivi sasa mji wa Iringa unazizima
kwa maandamano ya wanachuo
kikuu kishiriki cha Mkwawa
kwenda kwa mkuu wa mkoa kisa
hawajaingiziwa fedha zao,HII NI
HAKI KWELI WAKATI MAMILIONI YA
KODI ZETU YANALIWA NA
WACHACHE SERIKALINI?

Haya mambo yanasikitisha,kuna dr. moja wa mkwawa ni rafiki yangu, juzi aliniambia kuwa wanafunzi wa mkwawa wana hali mbaya ya kiuchumi kiasi kwamba wana shindia mapera. aliniambia kua alikutana na wanafunzi wake wakiwa chini ya mti wa mapera akawapongeza kwa utulivu na ku discus,wakamwambia "ticha yani hapa sio kwamba tuna discus ila hu mti wa mpera unatusaidia sana maana hatuna hata hela ya chakula muda wa week sasa hivyo tuna kula mapera kama lunch"huyo dr.aliniambia kuwa kwa hali hii lazima wanafunzi watagoma. Na kweli wamegoma. Ama kweli serikali sikivu.
 
hii serikali ya ajabu sana huku UDOM inabidi hela tuingiziwe alhamisi ijayo tarehe3/5,lakini hadi leo kwa utaratibu wa siku hizi hadi tusaini fomu,na ipite hata wiki mbili baada ya kusaini,mpaka leo hakuna hata dalili za kusaini

Msijali vumilieni kidogo, mwezi wa sita si bunge linaanza wafadhili watakuwepo. Acha wacheleweshe kidogo, heshima irudi maana 'totoz' za vyuo vikuu vilitukacha kwa muda sababu ya waheshimiwa!
 
Haya mambo yanasikitisha,kuna dr. moja wa mkwawa ni rafiki yangu, juzi aliniambia kuwa wanafunzi wa mkwawa wana hali mbaya ya kiuchumi kiasi kwamba wana shindia mapera. aliniambia kua alikutana na wanafunzi wake wakiwa chini ya mti wa mapera akawapongeza kwa utulivu na ku discus,wakamwambia "ticha yani hapa sio kwamba tuna discus ila hu mti wa mpera unatusaidia sana maana hatuna hata hela ya chakula muda wa week sasa hivyo tuna kula mapera kama lunch"huyo dr.aliniambia kuwa kwa hali hii lazima wanafunzi watagoma. Na kweli wamegoma. Ama kweli serikali sikivu.

Ni kweli hili ulisemalo la mapera au ni changamsha genge tu mkuu!
 
Hawa wasomi wetu bana?? sawa kudai allowance zao pia lakini tunatarajia pia kuona wakiandamana kupinga mambo ya kipuuzi kama ubadhirifu ulioonyeshwa na mawaziri kwenye report ya cag na kiwango duni cha ufaulu wa shule za msingi na sekondari! kwamba wao wanawaza allowances tu hawafikirii matatizo yanasababisha kukosekana allowances hizo kama ufisadi na poor management ya resources zetu??
 
Ningefurahi kusikia kama kuna wana CCM katika hayo maandamano..hapo ndio mahali muafaka kuelewa nguvu ya maandamano!
Hayo ndiyo maswala ambayo yalipaswa kuwaumiza wale 'wasomi' walioenda Ofisi za CCM kuunga mkono hatua ya CC ya CCM jana.
Mkuu wa chuo Mkwawa ametajwa katika ripoti ya CAG kama chanzo cha ubadhirifu chuoni hapo...halafu vijana wanataabika.
Poleni kwa tabu mnayoipitia..bila shaka mmeshamjua adui yenu.
 
Hopeful Shukuru Kawambwa ni mmoja wa watu wanaotarajiwa kulamba chaki wakati JK atakapowawajibisha wezi wakubwa wa hela zetu!!!!!
 
Back
Top Bottom