Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,392
- 39,495
Habari zinazoingia taratibu zinasema kuwa yule mpiga debe maarufu wa CCM Kapt. John Komba anatafutwa na Polisi kutokana na kufanya vurugu kwenye mkutano wa Upinzani. Kesi ya jinai imefunguliwa mjini Kibaya huko Kiteto na baadhi ya viongozi wa upinzani. Kapt. Komba alivamia mkutano wa Chadema ambapo alilazimishwa kushushwa jukwaani na FFU. Kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi ya 1985 (as ammended) ni marufuku kwa mtu kuingilia kampeni za uchaguzi wa chama kingine.