Breaking news:hali ya majeruhi wa maandamano ya chadema arusha

Wikiliki

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
528
139
Ndugu wana jf nipo katika hospitali ya mkoa wa Arusha Mt. Meru ambapo wamelazwa majeruhi wa maandamano ya jana. Nimelazimika kufika hapa hospitali baada ya kusikia malalamiko mtaani kuwa majeruhi hao wananyanyaswa na hawapati huduma. Baada yakufika hapa nimejionea mwenyewe hali ni mbaya majeruhi wamejilalia bila huduma na ndugu zao wasema wanapodai huduma wanaambiwa kwa dharau ni nani aliwaambia waende kwenye maandamano. Kwa taarifa za hapa hospitali waliokufa ni watu watatu ila bado kuna majeruhi wenye hali mbaya sana.
 
Inasikitisha, Tuwaombee daima ili Manani awape ahueni. Ni update nzuri na inatufaa humu.
 
Ipo siku kilio cha watanzania kitasikika, na wakati huo Serikali ya Jk haitasikilizwa tena hata na hao mbwa anaowatuma wakaue au kujeruhi watu!
 
Eheeee Mungu ibariki Tanzania,wabariki majeruhi wote wa huko arusha wapate kupona,mbariki Dr.slaa(Phd) na viongozi wengine wa chadema,mungu ibariki CHADEMA.
 
Hta McCain alipotunguliwa na ndege na kuruka na mwavuli na kutua katikati ya jiji Huko Vietnam wavietnam walitibu majeraha yake.

Wavietnam waliweza kumtibu mtu aliyekuwa akiwamwagia mabomu bila huruma.

Iweje Maadakatari na Manesi wetu walio kula kiapo kutumia ujuzi wao kunusuru maisha ya Watanzania wanaingiza siasa kwenye matibabu?
majeruhi wa maandamano nilazima watibiwe mara moja, wakumbuke kuna kesho KANU iko wapi???

Kwanza kuandamana si kosa, polisi hawatoi kibali cha kuandamana kazi yao ni kulinda usalama.

Hata Madaktari wa Makaburu wa Afrika kusini walikuwa na afadhari wengi walijitolea kutimu waliojeruhiwa bila kuingiza rangi wala itikadi.

Hii ni Aibu yetu wote.
 
Hta McCain alipotunguliwa na ndege na kuruka na mwavuli na kutua katikati ya jiji Huko Vietnam wavietnam walitibu majeraha yake.

Wavietnam waliweza kumtibu mtu aliyekuwa akiwamwagia mabomu bila huruma.

Iweje Maadakatari na Manesi wetu walio kula kiapo kutumia ujuzi wao kunusuru maisha ya Watanzania wanaingiza siasa kwenye matibabu?

Hata Madaktari wa Makaburu wa Afrika kusini walikuwa na afadhari wengi walijitolea kutimu waliojeruhiwa bila kuingiza rangi wala itikadi.

Hii ni Aibu yetu wote.

tucomfirm kwanza.naamini hata manes na madakta ni chadema.inawezekana kazi zimewazidia.msongamano unaweza kupungua iwapo majeruhi wengine watapelekwa hospitali za pembezoni mf tengeru,seliani,kaloleni na levolosi.
Nguvu ya umma iendelee!!
 
Ndugu wana jf nipo katika hospitali ya mkoa wa Arusha Mt. Meru ambapo wamelazwa majeruhi wa maandamano ya jana. Nimelazimika kufika hapa hospitali baada ya kusikia malalamiko mtaani kuwa majeruhi hao wananyanyaswa na hawapati huduma. Baada yakufika hapa nimejionea mwenyewe hali ni mbaya majeruhi wamejilalia bila huduma na ndugu zao wasema wanapodai huduma wanaambiwa kwa dharau ni nani aliwaambia waende kwenye maandamano. Kwa taarifa za hapa hospitali waliokufa ni watu watatu ila bado kuna majeruhi wenye hali mbaya sana.

Kama ni kweli huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu...... huwezimnyima mgonjwa huduma ya afya kwa kuwa amejitakia, mbona majambazi wakiwa na majeraha huhudumiwa na pingu zao kitandani?? Hili limekaa kisiasa zaidi ....... nina uhakika hao manesi/wauguzi wanaotoa maneno hayo ya kashfa kuna sehemu wanapopatia jeuri hiyo.
 
Nice updates, wadau wa JF tuzidi kuwapa moyo mshujaa wetu wa demokrasia ya kweli, siku zote utawala ulioshindwa kwa hoja hutumia nguvu kuzima vuguvugu, CHADEMA KITAENDELEA KUTUMIA NGUVU YA UMMA KUDAI HAKI, USAWA NA UTAWALA WA SHERIA, ndugu zetu ANC walipambana kwa miaka mingi hatimaye waliondoa dhuluma, pia Msumbiji, Angola, sasa zamu yetu Tanzania!!
 
you can stop demonstrations but you can not stop changes in the minds of the people.
 
kazi yao si bure wanaweza wasivune wao matunda yakazi waloifanya ipo cku tanganyika itakuwa huru uwezi kudanganya watu ckuzote ipo cku watagundua ukweli na cku hyo tayari ole wao mapolic wanaojerui na kuua watanganyika wenzao mana mbaya wetu ni huyo huyo anayekuamuru kutudhuru
 
Ndugu wana jf nipo katika hospitali ya mkoa wa Arusha Mt. Meru ambapo wamelazwa majeruhi wa maandamano ya jana. Nimelazimika kufika hapa hospitali baada ya kusikia malalamiko mtaani kuwa majeruhi hao wananyanyaswa na hawapati huduma. Baada yakufika hapa nimejionea mwenyewe hali ni mbaya majeruhi wamejilalia bila huduma na ndugu zao wasema wanapodai huduma wanaambiwa kwa dharau ni nani aliwaambia waende kwenye maandamano. Kwa taarifa za hapa hospitali waliokufa ni watu watatu ila bado kuna majeruhi wenye hali mbaya sana.

POLENI WAPIGANIA UHURU WETU SISI WENZENU TUPO NYUMA YENU NA IKIWEZEKANA TUANZISHE MFUKO WA SAIDIA MAJERUHI ILI WATIBIWE HATA PRIVATE HOSPITALS
 
Iko siku Demokrasia ya kweli itachukua mkondo wake. Tunawaombea majeruhi Mungu awaponye haraka. Wanadai haki za hao wanaoleta kiburi huko hospitali hivi wataelewa lini, watu wanajitolea kwa ajili ya wao kupata unafuu wa maisha kweli hawaoni its very bad.
 
Kama ni kweli..hiyo ni habari yakusikitisha sana!Kama mpaka huduma muhimu hivyo mtu ananyimwa tunapoelekea hakufai!!Kwaza polisi sasa maDr.!Kweli kazi tunayo...sijui siku mafisadi waking'olewa madarakani hawao vibaraka wao watahama nchi au nao watachekelea uhuru tutakaoupata!
 
Kwakweli hali ni mbaya. Serikali ya Kiwete ni serikali ya kimabavu , Kigaidi, na Ukandamizaji. Hivi kuna tofauti gani kati ya magaidi wa Al qaeda wanaolipua mabomu kwenye mikusanyiko ya watu wasio na hatia na hawa Polisi Pumbaf wa Kiwete?

Hivi huyu Kiwete kweli atasimamia mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya? Huwezi kuwa na dhamira ya kweli ya jambo kubwa kama la katiba, lakini ukashindwa kwenye jambo dogo kama hili la maandamano ya amani.

Damu ya watu wasio na hatia, haimwagiki hivi hivi. Lazima itajibu tu!!
 
Poleni saaana wa AR. Tupo pamoja. Bila kusahau haki huwa haipatikani bila damu kumwagika. Pia mmenikumbusha kipindi kile huku kwetu ZNZ. Tulifanya maandamano makubwa ya amani ila watu waliuliwa kama kuku. Angalau kidogo tuna mabadiliko kwa sasa ktk uendeshaji serikali.
 
Hao madaktari wanaokataa kuwatibu walaaniwe tena wafe kiajabu hata maiti zao zisionekane,Mungu nakuomba uwalaani na uzao wao,Mungu nakuomba pia uwaponyeshe wote walioumia,
 
Naona mambo ni magumu. Kwenye picha nimeona Dr Silaa ana POP (mhogo) kwenye mkono wake wa kushoto, ameanguka lini au ni ile ya wakati wa kampeni haijapona?
 
Mbona manesi hawana tofauti na polisi kimaisha sidhani kama wanaweza watelekeza majerui
 
Back
Top Bottom