Breaking News: Bondia Dulla Mbabe amuomba Waziri Mwakyembe amuite ili amlipulie bomu kubwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Akizungumza kwa masikitiko makubwa kabisa katika ' Segment ' ya Michezo Clouds tv Kipindi cha 360 Bondia anayekuja kwa Kasi kwa sasa nchini Tanzania Dulla Mbabe ametema ' cheche ' na kumtaka Waziri husika mwenye dhamana ya Michezo nchini Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe awaite haraka sana ' Mabondia ' wote ili wampe taarifa za ' Kashfa ' kubwa zinazoendelea katika Tasnia ya Ndondi / Ubondia nchini Tanzania.

Katika kuonyesha kwamba Dulla Mbabe kweli anajiamini na wala haogopi kitu wala mtu ameenda mbele na kusema kwamba ' Maadui ' wakubwa wa kuendelea kwa mchezo wa Ndondi nchini Tanzania ni Watu watatu tu ambao ni ' Mapromota ' pia:

  1. Yassin Abdallah
  2. Emanuel Mlundwa
  3. Chaurembo Palasa
Aidha ' Bondia ' huyo amedai kwamba kuna mambo mengi sana ya ' Hatari ' yanafanyika kwa ushirikiano wa hao watajwa hapo juu, Watendaji wa juu kabisa wa Baraza la Michezo nchini Tanzania pamoja na Wafanyakazi wasio waaminifu wa Uwanja wa Ndege wa Tanzania JNIA.

Baadhi ya ' Kashfa ' ambazo Bondia huyu ' machachari ' kabisa Dulla Mbabe amezitaja ni ile ya hao ' Mapromota ' Watatu tajwa hapo juu kuwasafirisha ' Mabondia ' wenye umri mdogo, wasiopimwa afya na wala hawana vibali vya kucheza mapambano. Pia akasema kuna ' Mabondia ' ambao wanatumika kama ' Mabegi ' ya kusafirisha dawa za kulevya.

Naamini humu JF Waziri Dkt. Mwakyembe yupo au Watendaji wake wapo au hata wana Familia wake hivyo naomba tu kama akiuona huu uzi au anaweza kufikishiwa huu uzi basi afanye upesi akutane na hawa Mabondia akina Dulla Mbabe ambao wamesema wana mengi ya ' Siri ' ambayo wanaamini yanaweza kuwa na msaada mkubwa kabisa mchezo wao wa Ngumi.

Nawasilisha.
 
Washamdhulumu ameamua kufunguka.

Madai mazito sana nayo, hasa issue ya madawa naamini Dulla anajua na ana uhakika wa anachosema.
 
Siasa za michezo zinavuruga wachezaji maana nao wanakuwa wasemaji badala ya kujikita kwenye michezo.
 
Huyo yassin abdalah a.k.a ustadh ndo adui wa kwanza kwenye mchezo huu anajifanya don king yeye, Tyson yeye, tpbc yeye. Tpbo yeye!
 
Back
Top Bottom