Brazil yashuhudia idadi kubwa zaidi ya vifo vya corona kwa siku ya pili mfululizo

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
96
150
Brazil imeendelea kuweka rekodi ya vifo vingi kwa siku ya pili mfululizo baada ya kurekodi vifo 1,910 siku ya Jumatano pekee, huku watu 71,704 wakipata maambukizi mapya.

Hii ni baada ya vifo vya watu 1,641 siku ya Jumanne pekee, kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ya taifa hilo, ikiwa ni rekodi mpya ya idadi kubwa zaidi ya vifo, ikizidi rekodi ya vifo 1,595 ndani ya siku moja iliyoshuhudiwa mwishoni mwa mwezi Julai mwaka jana.

Taifa hilo ni la pili kuathirika zaidi duniani baada ya Marekani, ikishuhudia vifo vya zaidi ya watu 257,000 tangu kuzuka kwa maambukizi ya corona.

Licha ya kushuhudia vifo vingi, Rais wa Brazil ameendelea kupuuzia njia za kisayansi za kupambana na corona ikiwamo uvaaji wa barakoa akisema zinaweza kusababisha kuumwa kichwa na kumuondolea mtu furaha. Ametishia kutotoa fedha kwa miji na majimbo yanayoweka sheria kali za kutokutoka nje na uvaaji wa barakoa.

Gavana wa Jimbo la Sao Paulo, Joao Doria amemlaumu Rais Bolsonaro kuwa kuweka afya ya wananchi wake hatarini akisema hali inayotokea sasa ni kutokana na kukataa ukweli kuhusu corona.

"Zaidi ya watu 1,000 wanakufa kila siku nchini Brazil. Hii ni kama ndege tano zinazoanguka kila siku. Wengi wa wananchi wa Brazil waliozikwa wamekufa kwa sababu haukufanya ulichopaswa kukifanya: kuongoza," alisema Doria.

Brazil imeanza mpango wa kutoa chanjo katikati ya mwezi Januari lakini ni asilimia 3 tu ya watu wote ndio waliopatiwa chanjo, ikipanga kuwapatia chanjo wananchi wote itakapofika mwishoni mwa mwaka.

Chanzo: Al Jazeera
 

longi mapexa

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
2,845
2,000
Atleast wako na mpango wa chanjo.

Liko taifa Moja tu duniani ambako huko hakuna chochote si wagonjwa vifo wala takwimu.

Lakini sasa wako na CHANGAMOTO ya kutisha.
 

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
4,889
2,000
Janga hili kubwa sana sio mchezo bahati mbaya kule Brasil wana Rais anaesema huu ugonjwa haupo ila wao wanaweza kumbana kidogo.
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
2,574
2,000
Hiyo nchi ina zaidi ya watu mil.250 sasa ukichukua ratio ya waliokufa nawaliopo hai ni 0.000 huko something like normal vifo per day
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
58,497
2,000
Dah....
Corona ni ugonjwa mbaya sana, sisi tuliopatwa na haya maswahibu ndio tunaweza kuelezea vyema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom