Brazil vs Tanzania: A tale of two elections


F

Fareed

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2010
Messages
328
Likes
13
Points
0
F

Fareed

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2010
328 13 0
Brazil vs Tanzania: Tofauti kati ya uchaguzi wa Oct. 31

Tafakari,

Tanzania na Brazil zote zilifanya uchaguzi wa Rais siku moja ya Jumapili, October 31, 2010.

Tanzania ina population isiyozidi watu milioni 44 na ina idadi ya wapiga kura kama milioni 20.

Brazil ina population ya watu milioni 200 na watu waliojiandikisha kupiga kura ni 135 milioni.

Brazil turnout ilikuwa 82 percent, Tanzania ilikuwa 43 percent.

Matokeo kamili ya kura za Urais Brazil yenye wapiga kura 135 milioni yalitangazwa siku MOJA tu baada ya uchaguzi (November 1, 2010).

Tanzania, ambayo watu waliopiga kura walikuwa kama milioni 8 tu, ilitangaza matokeo kamili ya kura za Rais Novemba 5, siku TANO baada ya uchaguzi.

Kikwete aliapishwa siku 1 tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi kutokana na hofu ya watu kupinga matokeo ya kura za wizi.

Rais mpya wa Brazil ataapishwa Januari 1, 2011, wakati matokeo yalitolewa Novemba 1, 2010. Hii itakuwa ni miezi MIWILI tangu matokeo yatangazwe. Rais wa Brazil alipata ushindi wa halali wa 55% ya kura. Kikwete alipata ushindi wa wizi wa 61% ya kura.

Tunaelewa sana kuwa Brazil iko dunia nyingine kiuchumi na maendeleo kufananisha na Tanzania and it has strategic importance to the Americans kuliko Tanzania.

Lakini kwa kutambua kuwa uchaguzi wa Brazil ulikuwa huru na haki na hakuna wizi wa kura kama Tanzania, Rais Obama siku hiyo hiyo ambayo matokeo ya kura za Rais yalitangazwa alimpigia simu yeye mwenyewe Rais mteule wa Brazil kumpa hongera.

Kwa upande wa Tanzania, baada ya kuona wizi mkubwa wa kura uliofanywa na mizengwe kwenye matokeo hasa ya kura za Rais, Obama hajampongeza Kikwete kwa ushindi.

Badala yake, amewapongeza Watanzania kwa kukamilisha uchaguzi kwa amani. Lakini amempongeza Shein kwa ushindi kwa kutambua kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa credible kuliko wa Tanzania.

Wadadisi wa duru za kidiplomasia wanasema kitendo cha Obama kuipongeza Tanzania na si Kikwete mwenyewe ni ishara kuwa Marekani hairidhiki na matokeo ya uchaguzi huo.

Obama alituma salamu hizo za kuipongeza Tanzania na siyo Kikwete Novemba 13, 2010, siku 7 baada ya kuapishwa kwake.

Hii ni ishara tosha kuwa viongozi wa dunia wanaamini kuwa ushindi wa Kikwete haukuwa wa haki na ameiba kura.

Kuna tetesi kuwa Rais Obama sasa ameahirisha mpango wake wa kuja Tanzania na badala yake anaweza kwenda Zanzibar peke yake kama akiamua kuja.
 
K

KipimaPembe

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2007
Messages
1,284
Likes
66
Points
145
K

KipimaPembe

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2007
1,284 66 145
Matokeo ya uchaguzi wa Tanzania yalikuwa tayari siku moja baada ya Uchaguzi, ila mahitaji ya kubadilisha matokeo yakafanya uchaguzi huo uchelewe mno.

Visingizio vya miundo mbinu mibovu havina uhusiano na kuchelewa kwa matokeo kwa muda wa siku tano. Inatakiwa sheria ya uchaguzi sasa hivi iseme, matokeo si zaidi ya Masaa 48 baada ya uchaguzi.

Muda mwingi unaotumiwa unawapa nafasi mawakala wa wizi wa kura kujua matokeo haraka kabla ya kutangazwa rasmi. Wakishajua huingilia ili kuhakikisha anashinda yule wanayemtaka.

Wizi wa kura ulikuwa rampant hasa katika kujumlisha matokeo kwa kuingiza figures zisizokuwa halisi.

Sheria ya uchaguzi lazima iweke kikomo cha masaa 48 yakipita hayo, basi uchaguzi utangazwe kutokuwa halali.
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
81,000
Likes
46,697
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
81,000 46,697 280
Miafrika never get anything right....
 
The Dreamer

The Dreamer

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2009
Messages
1,280
Likes
0
Points
0
The Dreamer

The Dreamer

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2009
1,280 0 0
Ahsante. Uchambuzi wako mzuri na glass yangu ya maziwa ladha imedouble. Ubarikiwe
 

Forum statistics

Threads 1,239,129
Members 476,369
Posts 29,343,548