Brazil: Rais Luiz Lula da Silva aliye gerezani kwa makosa ya rushwa huenda akaachiwa huru

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
636
1,842
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, ambaye anazuiliwa jela kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa makosa ya rushwa, hivi karibuni anaweza kuachiliwa huru baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu Alhamisi usiku.

Silva.jpg

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amekuwepo gerezani kwa zaidi ya siku 500 sasa
Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Brazil wamepiga kura ya kubadilisha kanuni ambayo imekuwa ikitaka wafungwa ambao hupoteza rufaa ya kwanza, kufungwa jela.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa, hatua hii huenda ikasababisha rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva kuwa huru.

Aidha, uamuuzi huu unamaanisha kuwa, maelfu ya wafungwa wakaachiliwa huru.

Uamuzi wa majaji 11 wa Mahakama Kuu ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na hamu na tayari umetolewa, baada ya mjadala mrefu, kwa kura 6 dhidi ya 5, na unaweza kuwaachilia huru wafungwa wengine 5,000.

Lula, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 8 na na miezi 10 jela kwa makosa ya ufisadi, alifungwa jela mwezi Aprili 2018, muda mfupi baada ya hukumu dhidi yake kuthibitishwa na Mahakama ya Rufaa, ingawa bado anaendelea kukataa rufaa katika mahakama za juu.

Mara tu baada ya uamuzi huo kutolewa, mawakili wa kiongozi huyo wa kihistoriakutoka mrengo wa kushoto nchini Brazil wametangaza kwamba wanataka kuomba mteja wao aweze kuachiliwa huru.

Lula anazuliwa jela kwa siku 579.

Waendesha mashtaka wanaohusika na uchunguzi huo wamesema kwa taarifa kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu unaenda kinyume na "hisia za kutokujali kuadhibu" na umuhimu "wa mapambano dhidi ya ufisadi, ambavyo ni vipaumbele kwa nchi yetu "Chanzo: RFI Kiswahili
 
Safi,Huyu mzee kafanya makubwa sana kwa wabrazili wengi hasa kuwainua kiuchumi,Kumfunga kwa visa vya kisiasa ni kumdhalilisha
 
Lula está livre washamwachia na punde tu alikuwa akiwashukuru wote walioshiriki kwa namna moja ama nyengine ili kufanikisha kutoka kwake jela huko Curitiba.
Nami naungana na watu wote waliokuwa wakiimba Lula eu te amo
Nalog off
 
Back
Top Bottom