BRAZIL inaenda kuwa bingwa wa Kombe la Dunia 2022

Yohana469

JF-Expert Member
Feb 16, 2021
302
448
WAZEE WA SAMBA BALL, ni miaka 20 iliyopita tokea Brazil itwae Kombe la Dunia kwenye ardhi ya Japan na Korea ikiwa na nyota pendwa Ronaldo de Lima, Rivaldo, Cafu, Zee la mashuti Roberto Carlos, Dida, Gilbeto Silva bila kumsahau Ronaldinho Gaucho hakika Brazil ni taifa lililojaliwa vipaji lukuki vya soka toka soka linaanzishwa.

Kwa miaka za hivi karibuni Brazil imekuwa ikifanya uzembe kwa kutotwaa makombe pendwa na hii imewafanya mashabiki wailaumu sana, ukiangalia Brazil ni taifa ambalo % kubwa wachezaji wengi wanacheza Ulaya tena klabu vikubwa vinavyocheza ligi kubwa EPL, Laliga, Seria A nk.

Tokea Brazil ifahamike inajua soka na vipaji vya hali ya juu wachezaji wamekuwa wakilewa sifa kwa kiasi kikubwa na hii ikipelekea kupoteza mechi mfano ukiangalia nyota wa sasa Neymar ni mchezaji mzuri na kipaji kikubwa kinachomuharibu ni utoto wake.

Sasa kuelekea World Cup 2022 safari hii Brazil imepania hawatafanya uzembe na kulewa sifa kama miaka iliyopita, ukiangali takwimu Brazil toka mechi za kufuzu zianze kule America Kusini, Brazil kashinda mechi 24 kati ya 27 na sare 3 na ameongoza kundi. Hivyo, safari hii inashauku na nia ya kufanya vizuri na kutwaa taji.

Ngoja tusubiri!
 
Kule Tuna Fundi Bishoo , mtaalamu wa Mpira kipenzi cha watoto wa Kike Neymar Jr huyu hana mfanowe

Kule kuna Fundi mwingine mtaalamu wa kuweka mpira mguuni ., akikupa pasi kam hujui mpira basi hutulizi Ufundi mwingi sana yeye mwenyewe anaitwa Paqueta.

Mabawa ya wings za hatari nikieleza hapa ntaonekana Mtunga Riwaya ..Vini Jr moto wake mnaujua pale madrid, Richarlison, Antony mchawi wa mpira kutoka Ajax

Hapo sijaja huku nyuma , kocha hajui ampange nani???

#Brazil bingwa asee
 
Njia pekee ya Brasil kuchukua ni kuliiba tuu
Hawana timu yenye muunganiko wanategemea individual brilliance yao
Hili ni tatizo kubwa
Wakifanikiwa ni robo final
 
Germany are favourites to be a champions in Qatar after disappointing 2018 world cup let's wait and see.
 
Kama tutaacha makosa yakiafrika kwenye kandanda uwanjani Afrika mwaka wetu Senegal lazima ichukue
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom