Kitendo cha Mheshimiwa RAIS kumlipia faini Mchungaji Msigwa ili atoke gerezani, kimedhihirisha Uhuru wa mahakama nchini Tanzania.
Mheshimiwa Rais ambaye ndiye humteua mwendesha Mashtaka(DPP), Majaji na kuwaapisha mawakili angeweza tu kuagiza Mchungaji Msigwa
a) Afutiwe mashtaka au
b) Aachiwe huru bila faini
c) Aachiwe Huru kwa dhamana n.k
Mheshimiwa Rais, hakuingilia Uhuru wa mahakama kwa kuruhusu mwenendo wa kesi ufikie Mwisho.
Katika nchi zisizoruhusu Uhuru wa mahakama. Mheshimiwa Rais hawezi kulipa faini ili kumnusuru ndugu yake na kifungo wala ndugu wa Rais hawezi kushtakiwa wala kutuhumiwa.
Hata kwa Dokta Mashinji aliyehamia CCM kutoka Chadema, katika nchi majirani zetu, kamwe asingeweza kuhukumiwa, kulala gerezani wala kudaiwa faini.
Mheshimiwa Rais, umetudhihirishia watanzania na Dunia kwa ujumla kwamba, Mahakama za Tanzania zipo huru, nawe unaunga mkono Uhuru wa Mahakama.
Mara zote unapoapisha mawakili na kuteua majaji, umekuwa ukihimiza haki, uwajibikaji na uzalendo kwa mhimili wa Mahakama. Ndio maana nasema.
Bravo Mheshimiwa Rais, kudhihirisha Uhuru wa Mahakama nchini, Watanzania tumuunge mkono