Bravo polisi, hebu tuboreshe na angle hii pia....

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,071
Jeshi letu la polisi limekuwa kinara sana katika kudhibiti uhalifu na vurugu hasa hizi za kisiasa na matumizi mabaya ya mitandao.

Hadi sasa wamefanya mengi ktk kipindi hiki kifupi cha mwaka wa awamu hii ya tano. pamoja na yote, tumefail bado kudeal na uhalifu hasa ujambazi na ukatili mwingine katika jamii.

Nadhani wote tunalihitaji jeshi la polisi na wao pia wanatuhitaji.
Sehemu nyingi duniani ushirikiano wa askari na raia hauanzii ktk sungusungu bali mawasiliano ambayo ni bilateral baina ya askari na raia.
sehemu kubwa ya kuunda hilo ni kwa kuwa na open communication kati ya polisi na wananchi. kwa sasa wananchi wengi hawajui namba za simu za vituo vya usalama vilivyo karibu nao, sehemu kubwa ya namba zinazotolewa ni za makamanda wa juu ambao hata wananchi hawawezi kuwahitaji ktk maisha yale ya kawaida ya siku hadi siku.

Wengi huwa wanaona uharifu mdogo, wakati na mkubwa lakini inakuwa ngumu kusafirisha ujumbe. mfano wapo watu wanafanya vitendo vya ukatili kwa watoto au wanawake ila hakuna sehemu ya haraka ya kureport.

Mwigulu na team yako hebu wekeni sheria za kila kituo cha polisi kuweka namba za simu za dharura kwa ajili ya wananchi kuwasiliana nao panapotokea tatizo. lakini pia tuwe na namba za kituo cha juu ya hapo kururhusu watu kurefer their cases once alarm imekuwa ignored na madhara kutokea.

Kwa kasi ya kudhibiti matusi ya mitandaoni nadhani hata uhalifu tunaweza kuumaliza tukitumia hizi approaches.
 
Back
Top Bottom