Brasil yamtimua kocha Mano Menezes

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Mano Menezes ametimuliwa kazi mapema Ijumaa hii kufuatia kile kilichodaiwa kuwa ni muendelezo wa matokeo duni ya timu hiyo.
Andres Sanchez, mkurugenzi wa timu ya taifa alithibitisha hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari na akasema kuwa kocha mpya atatangazwa ifikapo Januari mwaka 2013.
Kocha huyo ambaye alirithi kibarua hicho kutoka kwa nahodha wa zamani wa Selecao, Dunga mwaka 2010 ameiongoza Brazil kushinda michezo 20, kutoka sare michezo mitano na kupoteza mechi sita.
Brazil ilishindwa kutamba kwenye kombe la mataifa ya Amerika Kusini na kutolewa na Paraguay katika hatua ya robo fainali mwaka 2011 na kikosi chake cha Olimpiki kikashindwa kutwaa medali ya dhahabu huko Wembley mwaka huu.
Duru zinasema kuwa huenda kocha wa zamani wa timu hiyo, Luiz Felipe Scolari akarudia kazi yake ya zamani.
Menezes alikuwa kocha wa klabu ya Brazil, Gremio tangu mwaka 2005 mpaka 2007 ambapo aliiongoza kufika fainali ya Copa Libertadores na kufungwa na CA Boca Juniors.
Toka hapo akafundisha Corinthians ambayo aliiongoza kubeba kombe la ligi la nchini humo.
 
Back
Top Bottom