Branch manager wa nbc mlimani city afukuzwe kazi

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Huwezi kuamini NBC mlimani city Dar hua inatakiwa iwe imefunguliwa kuanzia saa 4 asubui,ila mpaka sasa hawajafungua.Wateja wamejaa hata ATM hazifanyi kazi.NBC imekua inafanya vibaya sana kwa wayeja wake.Hapa pembeni yake kuna CRDB inafanya vizuri sana,wamewawekea wateja hadi viti vya kukaa.NBC wao wanavuna tu hela ila kumjali mteja ni zero kabisa.Ni upuuzi sana.Kuna mteja anataka hela na anasafiri,amelalamika sana
 
mjifunze kuwa na account sehemu zingine....hao NBC upuuzi wao haukuanza leo
 
Hivi huwa zinafunguliwa hata j2 eeh? Na suluhisho pekee ni kumfukuza kazi?
 
Juzi NBC CORPORATE ya kule Posta Mpya ambayo ndio kama Head Office wateja waliwatukana wafanyakazi kwa kuwaweka almost an hour kwenye mstari bila kupewa huduma yoyote kila mtu akija anawaangalia wateja halafu anaondoka, wanakuja wamevaa suti zao na vimini vyao wanawaangalia tu bila kuwapa huduma yoyote ilibidi wateja waanze kuporomosha matusi benki nzima ili wapate hizo huduma ndipo walipokuja na kuanza kuomba msamaha.
 
Kwani Tanzania katika kutoa huduma za bank ipo? Kazi ya meneja sio kukaa ofisini na kuchart kwenye facebook ni kusimamia huduma za kibenki hata kama kuna foleni kubwa ya wateja anatakiwa kuhakikisha kuwa wateja wanahudumiwa haraka ili kuokoa mida yao (Time is money) sio kuja kukaa banki 1-5hrs ku-deposit au ku-draw pesa. Wajifunze kupitia nchi nyingine. Mameneja na wafanyakazi wa Bank za kitanzania ni wajeuri utafikri hiyo huduma inatolewa bure kumbe unalipia na mishahara yao inatokana na pesa ya wateja.
 
Kwa ufupi, banking sector Tanzania nzima ni ovyo na inakera kupindukia! Huduma ni mbovu sana na kauli mbovu za wafanyakazi ni mbaya kupindukia. Unaweza kuwa hata na akaunti benki tatu tofauti tofauti, na una shida ya pesa (eg weekend) hapo ndio utajua ubovu wa huduma za benki za bongo. Binafsi natumia tu mara chache sana na inapobidi sana, otherwise najitahidi sana kuziepuka benki za bongo.
 
yamenikuta jana crdb kijitonyama,atm hazfany kazi,ukipiga cal center inaita hawapokei,ni ujingaujinga 2,hela zako then unazsoteeeea
 
Mimi sikuhizi siweki hela zangu kwenye hizi benk kubwa ni upuuzi mtupu....hela zangu zipo kwenye hizi benk zenye umoja switch....ukitaka hela nyingi hukai sana, just few seconds unaenda benk unatoka na mkwanja wako, hawa nbc chai sana....unakuta unataka milion kadhaa wanakuweka kwenye kibulk room hakina hewa watu kibao humo ndani basi balaa tupu....mimi sitaki kuwasikia kabisa toka hii benk iende kwa wasauz imekua ya kipuuzi kupindukia, customer service hovyo yani mteja ni **** wakati kwingine mteja ni mfalme.
 
Wewe hukujua km NBC ni benki ya Ki*******g:A S 13:
Mbona kuna benki poa tu km EXIm, FBME hazina hata foleni sasa unakaa kusubiri hao makaburu. Achana nao tena ifunge fasta akaunti yako hamia benki za maana.
 
mjifunze kuwa na account sehemu zingine....hao NBC upuuzi wao haukuanza leo
Kufungua account sehem nyingine pia na kuwa na account nyingi ni kuongeza cost unnecessarily. Kama walivyosema wengine, benki zetu zina matatizo makubwa saana kuanzia na transaction costs zao na takataka nyingine. Hazina tofauti na makampuni ya simu. Tatizo wengi wetu huamini huduma zile tunazopewa ni hisani yaani si stahili yetu. Mteja anafanyiwa vile na bado anang'ang'ania benki ile. Dawa ni kuondoka kutafuta nafuu ya huduma. Hivi wateja wengi wakiwa na hulka ya kurejea kule walipohudumiwa vibaya unadhani hizi huduma mbovu hazitakoma?
Pia kuna haja ya kuharmonise transaction costs na kufanya hizi withdrwaring costs ziwe uniform throughout hata kama mtu akidraw pesa kwenye benki nyingine. Mbona nchi nyingine haya yanafanyika? Sie tunangoja nyinyi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom