Boyfriend anatapika kwenye party baada ya kupombeka

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,270
Mmeanza kudate na mwenyewe umeridhika kuwa nae, mmekutama chuo na jamaa ni kupanga anakusaidia assignment. Umeona si vibaya kwenda nae nyumbani ukiamini kuwa hii pia security yako kuwa hatatongoza ovyo kwani hata kwenu anajulikana.

Mkoa huu ndiyo ulikozaliwa ingawa jamaa amekuja kwa mara ya kwanza kwasababu ya chuo. Weekend iliyopita wazee wako walifanya Sherehe kubwa ya ufunguzi nyumba.

Padri aliitwa asubuhi na misa ya shukrani kwa Mungu ilisomwa. Mbuzi kadhaa walipoteza uhai na baada ya chakula sherehe iliendelea mpaka kesho yake asubuhi kwa waliyoyaweza.

Binamu zako navwadogo zako wamekuita ukatoe msaada wa huduma ya kwanza kwani yule mgeni wako alizima ghafla kwenye kiti na sasa shati lake limejaa matapishi.

Hii hali utakabiliana nayo vipi?
 
unapomkubali mtu lazima ukubaliane na chochote kitakachotokea, haikwepeki iwe kwa mwanaume au kwa mwanamke, ila yapo yanayotokea ambayo unakuwa huyajui na hakuwai kuyasikia au kuyaona kutoka kwa mhusika, swala la kuzimia ghafla inaweza kuwa la kawaida au ana kifafa au magonjwa mengine ambayo labda akifanya kitu flani lazima tatizo hilo limtokee sasa tunao pendana lazima tufahamiane vizuri na kwa undani zaidi kuanzia ki afya, kiuchumi na tabia ni muhimu sana maana hutusaidia huko mbeleni. utawaona marafiki wengi huwa wanawakataza wenzi kutofanya kitu flani kutokana na hali yake kimaisha au ki afya ni kwa sababu hiyo. tatizo tajwa hapo juu kwenye thread likitokea lazima ukabiliane nalo kwa msaada wa wengine wenye uwezo wa kukusaidia endapo hutaweza mwenyewe maana huyo ndiye si mwingine. ukimkataa au kumkimbia kwakuwa limetokea basi ww ni mbaya sana hufai.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom