Boti za askari wa AU zaelekea Anjouan

Mbogela

JF-Expert Member
Jan 28, 2008
1,384
257
Boti za askari wa AU zaelekea Anjouan

2008-03-25 09:08:36
Na MORONI, Comoro

Boti tano zikiwa zimebeba wapiganaji wa vikosi vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyoongozwea na Tanzania jana zimeondoka kisiwa cha Moheli kwa ajili ya kuanza kufanya mashambulizi ya kumuondoa kiongozi anayekikalia kisiwa cha Anjouan visivyo halali, Kanali Mohamed Bakar, limendika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana.

Taarifa za BBC jana zimesema kwamba kisiwani Anjouan hali iliendelea kuwa shwari pamoja na kuwepo uwezekano wa kushambuliwa na vikosi vya AU ambavyo vimekuwa vikijichimbia Moheli, umbali wa kilomita 50 kutoka Anjouan tangu kuwasili Comoro.

Vikosi hivyo vya AU vyenye askari wengine kutoka Sudan na Senegal pamoja na wenyeji, kwa pamoja wanaunda kikosi chenye askari 1,800.

BBC imesema kwamba Kanali Bakari ameendelea na msimamo wake kwamba atakitetea kisiwa cha Anjouan hadi mwisho akidai kwamba lengo lake ni kulinda maslahi na utamaduni uliopo.

Habari zaidi kutoka Comoro zimesema kwamba askari wa vikosi vya AU jana walikuwa wakifanya mazoezi ya kijeshi ya namna ya kutua kutoka kwenye ndege kwenye fukwe za Moheli.

Comoro ambayo inaundwa na visiwa vya Moheli, Ngazija na Anjouan ina marais watatu kila kisiwa na Rais mmoja wa Shirikisho la visiwa hivyo vyote.

Kuna habari pia kwamba makundi ya raia wamekuwa wakikikimbia kisiwa cha Anjouan kelekea Moheli na Ngazija. Aidha wengine wakiwa na mizigo pamoja na familiwa zao wamekuwa wakiingia kwa makundi katika kisiwa cha Mayotte ambacho bado kinatawaliwa na Ufaransa.

``Nimedhamiria kuilinda Anjouan kwa gharama yoyote, achilia mbali ukweli kwamba kuna majeshi ambayo yatakuja na kuwapiga risasi wananchi wa Anjouan,`` Kanali Bakar aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) katika mahojiano maalum Alhamisi iliyopita.

Kanali Bakar anakadiriwa kuwa na askari wapatao 300 huku nchi hiyo ikiwa imeshakabiliwa na majiribio ya mapinzdizi 19 na machafuko kadhaa tangu visiwa hivyo vitatu vipate uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1975.

SOURCE: Nipashe
 
Mbogela, umespecialize kupost tu mada bila kusoma za wenzio? Ungesoma mada nyingine ungegundua kuwa kuna watu wamesharipoti major developments za Comoro kuliko hii ya kwako. Bila shaka hata kama uko Comoro hujui hali ikoje kwa sasa! Plz soma kwanza kabla hujapost topical issue kama hii.
 
Back
Top Bottom