Boti yazimika baharini leo mchana

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,369
14,065
Boti ya Sea Express inayofanya safari zake kati ya Zanzibar-Dar, Dar-Zanzibar.
Imezimika ghafla ikiwa inaelekea jijini Dar,
kwa mujibu wa rafiki yangu ambaye alikuwa ndani ya boti hiyo amesema; boti ilipofika karibu na kisiwa cha Chumbe, injini zote zilizima, umbali kutoka Bandari ya Zanzibar mpaka kisiwa cha chumbe ni kama KM 10. Lakini baada ya muda injini za boti ziliwaka na boti ikageuza kurudi bandari ya Zanzibar.
Taarifa zisizo rasmi zinasema Meli ya MV Serengeti nayo imeungua moto. Nitawajuza zaidi.
 
More update plz....hiyo serengeti ndo ikiyoopoa maiti toka mv spice?
 
Kwa mwendo huu itabidi usafiri wa asili uruhusiwe ili kupunguza haya majanga...
 
baa zinachomwa, meli zinazama,boti zinazima, watu wanakufa vyote tumsingizie Mungu mbona ulaya haya hayapo
 
Hapo kuna watu/mtu hajatimiza wajibu wake. Hivi SUMATRA hapa wanasemaje?
 
More update plz....hiyo serengeti ndo ikiyoopoa maiti toka mv spice?
<br />
<br />

MV Serengeti, ni moja ya meli zinazoenda huko Pemba na lenyewe limechoka, ilikuwa ya Bakheresa akaiuza kwa 400 millions tu,
inasemekana kwamba siku ambayo MV Spice Islander inazama hii MV Serengeti iliiona na zilipishana lakini ilishindwa kusaidia lolote maana ilikuwa imejaza kuliko ile iliyozama.
Yaani hata kama ingeongeza mtu mmoja tu na yenyewe ingezama.
 
Boti ya Sea Express inayofanya safari zake kati ya Zanzibar-Dar, Dar-Zanzibar.
Imezimika ghafla ikiwa inaelekea jijini Dar,
kwa mujibu wa rafiki yangu ambaye alikuwa ndani ya boti hiyo amesema; boti ilipofika karibu na kisiwa cha Chumbe, injini zote zilizima, umbali kutoka Bandari ya Zanzibar mpaka kisiwa cha chumbe ni kama KM 10. Lakini baada ya muda injini za boti ziliwaka na boti ikageuza kurudi bandari ya Zanzibar.
Taarifa zisizo rasmi zinasema Meli ya MV Serengeti nayo imeungua moto. Nitawajuza zaidi.
haya tuna subiri tamko la serikali na tume iundwe mara moja.....maana ndiyo zao
 
More news jamani kuhusu Mv. Serengeti kama kuna mwenye data kamili tujue imeungua ama lah!
 
mmmmmh sasa hii presha nyingine mbona makubwa haya duh ????????????????????
 
si sahihi kwa baadhi yetu kuhusisha kuchomwa kwa baa na ajali zinazotokea znz tukumbuke hata wabara wapo znz tena wengi tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom