Boti yazama Pangani, Tanga, sita wafa maji

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Boti, yazama, Tanzania, Pangani, Tanga,sita, wafa, maji, visiwani ,Zanzibar
Pangani. Watu sita waliokuwa wakitokea Bandari ya Kipumwi wilayani Pangani kuelekea Kikokotoni visiwani Zanzibar wamekufa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika bahari ya Hindi.

13 waliokuwepo katika boti hiyo wamenusurika, ikielezwa kuwa chanzo cha kuzama ni mawimbi makali.

Akizungumza leo Jumatano Mei 15, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema boti hiyo iiitwayo Mv Njemba ilizama usiku wa kuamkia juzi.

Amesema waliokufa katika ajali hiyo majina yao hayajajulikana, akibainisha kuwa wanawake ni wanne, mwanaume mmoja na mtoto na kwamba hadi jana 13 walikuwa wameokolewa.

Ofisa mdhibiti usalama na usafiri wa shirika la uwakala wa meli Tanzania (Tasac), Christopher Mlelwa amesema boti hiyo ilisajiliwa kwa ajili kuendesha uvuvi na na si kupakia abiria.

"Nilishapeleka taarifa kwa Serikali za vijiji vyote kikiwamo Kipumbwi ya kuzuia vyombo vyote kuingia baharini kutokana na hali ya hewa kuchafuka hasa baharini na wamiliki wengi wa vyombo walitii amri hiyo lakini MV Njemba iliamua kuiba safari,” amesema Mlelwa.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kipumbwi, Sabiri Abdi amesema baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Tasac alitoa tangazo la kuamuru vyombo vyote vya uvuvi kutoingia baharini.
 
Back
Top Bottom