NGOGO CHINAVACH
JF-Expert Member
- Apr 8, 2011
- 943
- 368
- Thread starter
- #21
Ukerewe ipo MV clariasUkerewe haiendi
Ukerewe ipo MV clariasUkerewe haiendi
Upungufu wa wateja.Kama ni masaa manne kwa nini isondoke asubuhi ikarudi jioni ?
Hiv ishu kama hizo huwa zinasimamia bei gani?Nitasifu sana na kufurahi iwapo hiyo boat imeundwa na Songora Marine transport ya Mwanza.Mleta mada hebu nijuze mtengenezaji wa hiyo boat. Kama imeagizwa toka nje wooooi! nalaani.
Ni nzuri sema nafikiri watakuwa wanastudy route yao ili waone wanatekebisha/kuboresha wapi. Uzuri naona wako positive katika maoni ya wateja wao ...kwa kuanzia siyo mbaya hata kidogoSasa kama ni Masaa 4, Si wapige ruti mbili Go & Return kwa siku
Unataka kumaanisha nini, ama hutaki wengine nao wafanye? hizi ni hira tayariAzam atatesa milele
Bikiko ndo wapiUkerewe Iendelee Hadi Bukiko Huko
Ukerewe Yaani Nansio Nako Kuna Visiwa VidogoBikiko ndo wapi
Ndio vizuri. Lakini vipi utulivu wake, inaonekana ni ndogo imetulia kwenye maji au ndio mwendo wa kutapikiana hasa ukiwa na watoto.Changamoto iliyopo ni kwamba watu wanakuja muda umeisha hivyo wanaachwa, jamani hii boti wenyewe hawazidishi muda muda ukifika hata kama wana abiria mmoja wanaondoka.
Huko hakuna abiria, hawa ndugu zangu wamezoea kupanda malori ya ndizi ama ng'ombe katika safari zao ukizingatia hawaendagi kwao mpaka lifti za misiba.Kampuni ya Earthwise Ferries (T) LTD ambayo imeleta boti ya kisasa MV Bluebird kwa ajili ya safari za Bukoba na Mwanza imepunguza nauli kutoka Tshs 50,000 hadi Tshs 30,000 kuanzia tarehe 11/01/2018.
Boti hiyo ambayo inatumia masaa manne kutoka mwanza kwenda Bukoba, na Bukoba kwenda mwanza, inauwezo wa kubeba watu 100.
Ratiba ya boti hiyo kwa wiki (11/01/2018 hadi 17/01/2018) hii ni;
N.B
- Itaondoka Mwanza kwenda Bukoba saa nne asubuhi (10:00AM) siku ya Alhamisi (11/01/2018), Jumamosi (13/01/2018), Jumatatu (15/01/2018) na Jumatano (17/01/2018)
- Itaondoka Bukoba kwenda mwanza saa saba mchana (13:00) siku ya Ijumaa (12/01/2018), Jumapili (14/01/2018), Jumanne ( 16/01/2018)
Kwa kifupi safari zao zinapishana kwamba akiingia leo Bukoba basi kesho yake anaenda Mwanza.
Kwa mawasiliano unaweza kufika katika ofisi zao zilizopo bandari ya Bukoba au bandari ya Mwanza kaskazini (Mwanza North Port) au mawasiliano +255 764 954 687 au +255 782 660 297
NAULI ni Tshs 30,000
Picha na video zipo hapo chini