Boti ya kisasa (speed boat) inayofanya safari zake Mwanza-Bukoba imepunguza nauli kutoka 50,000 hadi 30,000

NGOGO CHINAVACH

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
943
368
Kampuni ya Earthwise Ferries (T) LTD ambayo imeleta boti ya kisasa MV Bluebird kwa ajili ya safari za Bukoba na Mwanza imepunguza nauli kutoka Tshs 50,000 hadi Tshs 30,000 kuanzia tarehe 11/01/2018.

Boti hiyo ambayo inatumia masaa manne kutoka mwanza kwenda Bukoba, na Bukoba kwenda mwanza, inauwezo wa kubeba watu 100.

Ratiba ya boti hiyo kwa wiki (11/01/2018 hadi 17/01/2018) hii ni;

  1. Itaondoka Mwanza kwenda Bukoba saa nne asubuhi (10:00AM) siku ya Alhamisi (11/01/2018), Jumamosi (13/01/2018), Jumatatu (15/01/2018) na Jumatano (17/01/2018)
  2. Itaondoka Bukoba kwenda mwanza saa saba mchana (13:00) siku ya Ijumaa (12/01/2018), Jumapili (14/01/2018), Jumanne ( 16/01/2018)
N.B
Kwa kifupi safari zao zinapishana kwamba akiingia leo Bukoba basi kesho yake anaenda Mwanza.

Kwa mawasiliano unaweza kufika katika ofisi zao zilizopo bandari ya Bukoba au bandari ya Mwanza kaskazini (Mwanza North Port) au mawasiliano +255 764 954 687 au +255 782 660 297

NAULI ni Tshs 30,000

Picha na video zipo hapo chini

 

Attachments

  • IMG_20180105_151158.jpg
    IMG_20180105_151158.jpg
    32.6 KB · Views: 116
  • IMG_30112016_103932.jpg
    IMG_30112016_103932.jpg
    82.9 KB · Views: 122
  • IMG_30112016_105022.jpg
    IMG_30112016_105022.jpg
    49.1 KB · Views: 157
Nitasifu sana na kufurahi iwapo hiyo boat imeundwa na Songora Marine transport ya Mwanza.Mleta mada hebu nijuze mtengenezaji wa hiyo boat. Kama imeagizwa toka nje wooooi! nalaani.
 
Back
Top Bottom