BoT yazuia wabunge kuwemo bodi za mabenki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BoT yazuia wabunge kuwemo bodi za mabenki

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BAK, May 27, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,781
  Likes Received: 83,138
  Trophy Points: 280
  Date::5/26/2009

  Benki Kuu Tanzania yazuia wabunge kuwemo bodi za mabenki

  Na Ramadhan Semtawa

  Mwananchi

  KATIKA hatua moja kubwa ya kuondoa mgongano wa kimaslahi, Benki Kuu Tanzania (BoT), imetoa mwongozo mzito kwa mabenki nchini ukitaka wabunge wasiwe wajumbe wa bodi za taasisi hizo za kifedha ambazo serikali ina hisa.

  Serikali ina hisa katika benki ambazo ni Rasilimali (TIB) ambayo mbunge Kondoa Kaskazini, Zabein Mhita ni mjumbe wa bodi, NBC 1997 Limited, ambayo mbunge wa Nkasi, Ponsian Nyami ni mjumbe, NMB na Benki ya Posta.

  Kwa agizo hilo la BoT, wajumbe wote wa bodi ambao ni wabunge katika taasisi za fedha zenye mkono wa umma, watapoteza nafasi hizo hivyo kuondoa mgongano wa utendaji na usimamizi kama ambavyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amekuwa akisisitiza katika ripoti zake.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe alitangaza hatua hiyo jijini Dar es Salaam jana ndani ya wakati wa kikao cha kamati yake wakati na watendaji kutoka makao makuu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina.

  Kabwe, ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alisema uamuzi huo ni sehemu ya kuimarisha utawala bora na kuondoa mgangano wa kimaslahi.

  "Nafikiri itakumbukwa, CAG amekuwa akisisitiza kwamba hali ya wabunge kuwa wajumbe wa bodi, husababisha mgongano wa kimaslahi. Amelalamika hili katika ripoti mbili, sote ni mashahidi," alisema Kabwe.

  "Sasa, tayari Benki Kuu imetoa maelekezo kwa taasisi zote za fedha ikiwemo mabenki, kwamba wabunge wasiwe wajumbe wa bodi," alisema Kabwe akimaanisha taasisi hizo za fedha za umma.

  Kabwe alikuwa akijibu hoja ya mgongano wa kimaslahi iliyotolewa na msajili msaidizi wa Hazina, Geoffrey Msella ambaye alilalamikia mgongano huo akidai kuwa wakati mwingine huathiri utendaji wa ofisi yake.

  Awali, Msella alikuwa akifafanua swali aliloulizwa na mbunge wa Igalula, Tatu Ntimizi ambaye alitaka kujua matatizo hasa yanayokwamisha usimamizi wa mashirika unaopaswa kufanywa na Msajili wa Hazina.

  Msella alisema bodi za mashirika huteuliwa na mamlaka nyingine na akahoji: "Sasa, sisi tutawezaje kuwajibisha bodi ambayo wajumbe wake huteuliwa na mamlaka nyingine."

  Alifafanua kwamba, tatizo hilo pia lipo kisheria kwa kuwa Msajili wa Hazina anapaswa kuwa na mamlaka na mashrika ya umma, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa bodi.

  Kuhusu hatua hiyo ya BoT, Msella alisema itaondoa mgongano wa kimaslahia kwa sababu itaondoa hali ya mtu mmoja kuwa msimamizi na wakati huohuo mtendaji.

  "Uamuzi wa Benki Kuu kutaka wabunge wasiwe wajumbe wa bodi ni sahihi. Kusema wametumia vigezo gani, kwa undani sitaweza kueleza, lakini kigezo kikubwa ni kuondoa conflict of interest," alisema.

  Alipoulizwa baadaye na gazeti hili kwamba hadi sasa kuna wajumbe wabunge wangapi katika taasisi za fedha zenye mkono wa serikali, alisema zipo sita, lakini akasisitiza si vema kuwataja majina.

  "Takwimu nilizonazo hadi sasa ni kwamba, kuna wabunge sita ambao ni wajumbe wa bodi katika mabenki yetu, "alifafanua Msella na kuongeza:

  "Lakini si vema kuwataja majina kila mmoja, nafikiri ifahamike idadi tu kwamba ndiyo hiyo tusitaje majina."

  Suala la wabunge kuwa wajumbe wa bodi wa taasisi mbalimbali limekuwa gumzo katika miezi ya karibuni kutokana na baadhi ya wadau kutaka watungaji hao wa sheria wasiruhusiwe kuwa wajumbe wa bodi za mashirika ili waweze kushughulikia masuala hayo vizuri kwa nafasi zao kwenye kamati za bunge.

  Suala hilo liliwahi kuibuka bungeni mwaka jana lakini baadhi ya wabunge wakapinga, huku CAG akisisitiza kuwepo na kutenganisha majukumu kati ya mamlaka hizo mbili.

  Gavana wa BoT Profesa Benno Ndulu, ni mmoja wa watendaji wa taasisi za umma ambaye tayari ametangaza mwenyewe kujitoa ujumbe wa bodi ya benki hiyo ili kuepuka mgongano wa kimaslahi.
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Prof. Ndulu alikuwa mjumbe wa bodi wa benki ipi aliyojitoa? As governor of the centrl bank ,he is the chairman of the BOT board and hence a member of the board. He cannot be a board member of any other bank because BOT regulates all other banks!!
   
 3. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ni hatua nzuriii ila naomba iende mbali zaidi kwa waheshimiwa wabunge kutokuwa kwenye bodi zozote za taasisi au mashirika ya umma ili kuwapa nafasi nzuri ya kuyasimamiaa...

  Good governance inaanziaa hapoooo.....

  BOT wameanzaa vema na wengine wafuatee..
   
Loading...