BOT yamwaga mikopo ya mamilioni kwa wafanyakazi wake-Ndio bailout ya serikali hiyo!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BOT yamwaga mikopo ya mamilioni kwa wafanyakazi wake-Ndio bailout ya serikali hiyo!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Dec 14, 2009.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  MILANGO ya neema imefunguka kwa wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Kila mfanyakazi ataweza kukopa kati ya Sh 100milioni na Sh 30milioni kulingana na wadhifa wake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

  Habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema kwamba mikopo hiyo itatolewa katika madaraja manane. Viwango hivyo vya mikopo ni vipya ambavyo vimetokana na maombi ya wafanyakazi hao ya kuongezewa kiasi cha mikopo hiyo kutoka katika kiwango cha awali walichokuwa wakipewa.

  Wafanyakazi wa daraja la chini kabisa, watakuwa wanakopeshwa Sh30milioni, wakati wafanyakazi wa ngazi ya juu kabisa watapata mkopo wa Sh100milioni.

  Wafanyakazi wa daraja la kwanza ambalo ni la juu kabisa na ambao watakuwa wanapata mkopo huo wa Sh100milioni ni pamoja na wakurugenzi, wakurugenzi washiriki na wataalamu washauri waandamizi.

  Daraja la pili ni la wafanyakazi wenye vyeo vya mameneja na wataalamu washauri ambao watapata mkopo wa Sh90milioni, wakati daraja la tatu linawahusisha mameneja wasaidizi na maafisa wakuu waandamizi (professional I) ambao wao watapata mkopo wa Sh70milioni.

  Daraja la nne linawahusisha wafanyakazi wenye vyeo vya maafisa wakuu (professional I) na maafisa wakuu waandamizi (professional II), ambao wao watajipatia mkopo wa Sh 60milioni, huku wafanyakazi katika daraja la tano ni wale wenye vyeo vya maafisa waandamizi (professional I) na maafisa wakuu (professional II) ambao watajipatia mkopo wa Sh 55milioni.

  Katika daraja la sita kuna wafanyakazi wenye vyeo vya maafisa ngazi ya III-I (professional I), maafisa waandamizi (professinal II) na maafisa- makarani wakuu (cleric officers) ambao watajipatia mkopo wa Sh45milioni.

  Daraja la saba ni la wafanyakazi wenye vyeo vya maafisa-makarani kuanzia ngazi ya III hadi ngazi ya maafisa-makarani waandamizi (cleric officers), makarani waandamizi na makarani wakuu (clerks) ambao wao watajipatia mkopo wa Sh40milioni.

  Daraja la nane ambalo ni la chini kabisa linawahusisha wafanyakazi wa taasisi hiyo ambao ni walinzi, wapishi, madereva, wahudumu wa ofisi na wa zahanati na makarani ngazi ya daraja la III-I ambao watapata mkopo wa Sh30milioni.

  Habari hizo zinasema kwamba viwango vya awali kwa wafanyakazi wa daraja la kwanza na la pili kama ilivyoainishwa hapo juu vilikuwa ni Sh50milioni, daraja la tatu vilikuwa Sh35milioni, daraja la nne na la tano Sh30milioni.

  Katika daraja la sita viwango vya awali vilikuwa ni Sh25milioni, daraja la saba walikuwa wakipata mkopo wa Sh20milioni wakati daraja la nane ambalo ni la chini walikuwa wakipata mkopo wa Sh15milioni.

  Kwa mujibu wa waraka uliosainiwa na Naibu Mwenyekiti wa Mfuko wa Mikopo ya Nyumba, Len Kisarika kwenda kwa wafanyakazi wote wa makao makuu na katika matawi ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Zanzibar na Chuo cha Benki Mwanza kuwafahamisha kuridhia nyongeza hiyo, menejimenti hiyo imeridhia nyongeza hiyo ya mikopo ili kukidhi ongezeko la gharama za ujenzi.

  Katika waraka huo wa Desemba 2, mwaka huu ambao nakala yake imepelekwa kwa Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndullu na kwa Manaibu Gavana, menejimenti hiyo pia imeidhinisha ongezeko la kiwango cha mkopo kwa ajili ya matengenezo ya nyumba kutoka asilimia 15 hadi 20 ya mkopo uliotolewa.

  Waraka huo pia unabainisha kuwa kufuatana na hali ya Mfuko wa Mikopo ya Nyumba na ili kuhakikisha kuwa mikopo inayotolewa inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa, utoaji wake umefanyiwa marekebisho kutegemea vipaumbele na masharti mbalimbali.

  Kwa mujibu wa waraka huo, kipaumbele cha kwanza ni kwa waombaji wapya, cha pili ni maombi ya nyongeza ya mikopo kwa ajili ya nyumba ambazo bado hazijakamilika na kipaumbele cha tatu ni maombi ya nyongeza ya mikopo kwa ajili ya uboreshaji wa nyumba.

  Masharti yaliyotajwa katika waraka huo kwa kipaumbele cha kwanza ni pamoja na salio la theluthi moja ya mshahara wa mwombaji baada ya makato, kama ilivyoainishwa kwenye Sheria ndogo za utumishi za (BoT Staff By Laws, 2008), uwezo wa mkopaji kurejesha mkopo na kuwasilisha hati ya kiwanja ambayo haijatolewa kama dhamana na isiyo na kikwazo chochote.

  Katika kipaumbele cha pili na cha tatu, mbali na masharti yanayotajwa katika waraka huo pamoja na masharti ya kwenye kipaumbele cha kwanza, kuna nyongeza ambayo ni pamoja na ukaguzi wa nyumba husika itakayofanyiwa uboreshaji kwa kipaumbele cha tatu.

  Masharti mengine ya kipaumbele cha pili ni ukaguzi wa nyumba husika ili kuthibitisha hatua iliyofikia katika ujenzi, tathmini ya thamani ya nyumba husika kutoka kwa mthamini wa majengo aliyesajiliwa, tathmini ya kamati ya kuthibitisha kama kiasi cha mkopo kinachoombwa kama kinatosheleza kukamilisha ujenzi wa nyumba husika.

  Wakati nchi ina njaa!!! maskini wanaongezeka watu wananeemeka wasikimbie tu tutakapowakomalia kutwambia wanachaji interest kiasi gani hao wanaokopa??? Waliolipa wangapi??? na vigezo vinavyotumika kufatilia mikopo ikishindikana!!!! Hawa jamaa baada ya kupata pesa ya World Bank kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama ya bei nafuu kwa wananchi wameenza kuzitafuna haya baba!!! tutabanana tu Tanzania Hivi nyie subirini maskini akizidi kuwa maskini hubadilika na kuwa mnyama (Martin Luther King and Malcom X)!!!
   
 2. Jobjob2

  Jobjob2 Member

  #2
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 8, 2006
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  EPA nyingine nini manake uchaguuzi unakaribia
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Yap ndio hiyo hiyo kwasababu pesa walizopewa na World Bank wanazitafutia sababu ya kuzitumia na kwakuwa objective ilikuwa ni kuwapatia wananchi nyumba za kukaa waishi vizuri hesabu itachukuliwa na wafanyakazi wa benki kuu pia.


  Tutafika kweli Tanzania!!!!
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,493
  Likes Received: 2,738
  Trophy Points: 280
  Tatizo la BOT wanasahau kuwa hizo pesa ni za wananchi. Nafikiri ni Bongo tu ndiyo utakuta Central Bank kuna ulaji wa nguvu kushinda mashrika binafsi. Hawa jamaa wanagawana pesa kama hawana akili nzuri vile. Hivi kweli mlinzi ama dereva kama anchukuwa mkopo wa 30 million ina maana mshahara wake ni kiasi gani? na atalipa kwa muda gani?? Je kuna intrest inachargewa kwenye huo mkopo. Nafikiri hawa jamaa wameamua kula pesa za EPA wenyewe this time!!!
   
 5. e

  echonza Senior Member

  #5
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naomba nitofautiane kidogo na wachangiaji waliotangulia. Kwanza kabisa, suala la kujenga nyumba kwa kutegemea mishahara ya utumishi wa umma bila kuiba au kufuja pesa za walipa kodi haliwezekani kabisa mpaka hapo mtu anapopata kuwezeshwa (incentives) kwa kupata mkopo wenye masharti nafuu kama mpango huo uliotajwa hapo juu. Tatizo ni kwamba, Tanzania tayari umaskini wa watu unazidi kuongezeka na pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho pia linaongezeka vile vile. Sababu kubwa inayosababisha hayo ni kuwa na sera mbovu (zisizotatua matatizo halishi) au utekelezaji wa sera mbovu unaotokana na ufujwaji wa fedha zilizopangwa kutumika kwenye miradi mbalimbali (mfano, ujenzi wa majengo pacha ya Benki kuu).

  Hivyo, mradi huu wa mikopo Benki Kuu ni moja ya miradi ninayoweza kuisema kwamba inaongoza pengo kati ya wenye nacho na wasionacho. Inakuwaje watumishi hao hao kwa jina la watumishi wa umma wapate kuwezeshwa kuwa na nyumba za kisasa wakati watumishi wa umma kutoka sekta zingine waachwe nyuma? Haya ni maswali ya kujiuliza siyo kwetu tu wananchi tunaochangia na kuyaona madudu yanayofanya, bali pia hata watumishi wa ngazi za juu serikalini wanatakiwa wajiulize na majibu yake ni kutatua matatizo ya watanzania wote siyo kundi la watu wachache tu eti kwa jina la wanafanya kazi Benki Kuu!

  Hivi Benki Kuu ingekuwepo kama sekta zingine zisingekuwepo au zisingezalisha? Angalia, kupanga nyumba Dar es Salaam kwa mfano, ni gharama kubwa mno ukilinganisha na vipato vya watumishi wa umma. Serikali haijawahi kuliona hilo hata siku moja. Inasahau kwama inapotokea mazingira kama hayo hata uwezo wa kununua (purchasing power) wa mwananchi unakuwa duni maana pato lake linaishia kwenye mahitaji muhimu kama malazi na chakula tu. Inabidi kuwe na sera katika uchumi wa jumla (macroeconomic policies) na sera za uchumi wa mdogo (microeconomic policies) tukizingatia kitu kikubwa kupunguza pengo kati ya wenye nacho wa wasionacho kwa mtazamo wa (equity). Kugawa kwa usawa rasilimali na fursa za mwananchi kuwezesha kufanya mambo yake ili kuwa na maisha bora (decent life).

  Hivyo, mawazo yangu ni kwamba Serikali itafute pesa (naamini zipo kama ufisadi hautakuwepo) za kuwawezesha watumishi wote wa umma. Maana najua leo wao (Benki Kuu) wanawezeshwa na hao hao watawapangishia watumishi wenzao wa umma ambao hawako BOT kwa bei aghali kuliko kipato na inavyotakiwa iwe.
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Infact kinachotakiwa ni kuanzisha iwe Bank ya Nyumba au hizo hizo bank zetu ziwe na kitengo cha mikopo ya nyumba, ndio maana namuona Serikali ya Tz pamoja na Govenor wote wababaishaji maana suala la kokasa nyumba/mikopo ya nyumba lina kuwa kichocheo cha wizi
  pili ujenzi holela, watu kushindwa kufikiria kuboresha utendaji maana anawaza Baba/mama mwenye nyumba nitamlipaje au nitajengaje nyumba, watoto wanakulia kwenye chumba kimoja na wazazi wao, maana bei ndio hiyo haiwezekani, mazingira ya kusomea kuwa mabaya kwa watoto na wazazi nk nk.
  Na ndipo hapo hapo Mkapa alipokosea kwa kufikiria kuuza nyumba za serikali ni kutatua tatizo, badala ya kuanzisha mikopo ambayo ita wasaidia watanzania wote.
   
 7. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nchi hii kuna makundi mengi sana ndugu. Wakati wengine wakikopeshwa 100M zisizo na riba, na masufuru kibao, huku wakiwa wanaishi kwenye nyumba zinazogharimiwa na waajiri wao, watumishi wengine wanaishi kwenye "madebe" mfano polisi, sijui wakati wa joto kali kama Dar na Tanga hali inakuwa vipi. Waalimu huko vijijini ndio usiseme.

  Swala la afya ndio usiseme, wakati wengine wanalipiwa harama za matibabu wengine wanakatwa karibia 15% ya mishahara yao ya kila mwezi kwa huduma za afya wasizozipata.

  Kuna haja ya kuwa na sheria moja kwa wote:

  Kama ni mikopo ya nyumba, itolewe na chombo kimoja kwa wafanyakazi wote wa serikali, kama ni huduma za afya basi kama ni bima na iwe moja n.k

  Vinginevyo, ni kuzidi kumyonya mnyonge hadi tone la mwisho wakati waheshimiwa hawana wafanyalo na mshahara wo, kwani nyumba imelipiwa, usafiri, maji hadi watumishi wa ndani!

  Kweli haya yanawezekana tu afrika!

  Tulitak
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tuko pamoja kamanda ndio maana kichwa cha habari kinasema ndio government bailout hiyo!!! BOT inatoa mkopo kwa wafanyakazi wao ambao hupangisha nyumba hizo kwa maxepart kule msasani na mikocheni wao bado wanaendelea kukaa katika nyumba za shirika eti walikojenga mbali.

  Tuje katika mikopo yenyewe mchangiaji mmoja alisema hapa kuwa dereva milioni 30 atailipa kwa kiwango gani??? Kimshahara dereva wa Tanzania anapokea 400,000 tuseme laki mbili zimetumika maisha yake ya kila siku Payback period ni miaka 12 je unadhani huu ni mkopo wa busara???? unampa mkopo mtu for 12 years!!!!!! Hapo tumeignore interest charges, tumeignore grace period tumechukua facts and figures.

  Matokeo yake wanakopesha hivi ili kutajirishana maana wanajua wasipowawezesha wanaweza kuvujisha siri zao
   
 9. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huyo mfanyakazi wa hali ya chinni atalipia mkopo huo mpaka anapostaafu!
  Mbona wizara ya Afya hawatuletei mikopo kama hii jamani? au tubadilishe taalumma?
   
 10. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Ninadhani mikopo kama hii ni muhimu kwani inapunguza umaskini. Kwa mfano, wafanyakazi wa BoT watakapokuwa wanajenga majumba kwa kutumia pesa waliyokopeshwa, ni dhahiri kuwa ndugu zetu mafundi uashi n.k. watanufaika kwa kupata kazi. Additionally, wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi watapata biashara na kulipa kodi. At the end of the day, huo mkopo unakuwa na impact kuliko kulalia hizo hela hapo BoT. This is why nchi kama Marekani wanahaha kuhakikisha walaji wana pesa ya kutumia. Obama anahangaika kushawishi mabenki yakopeshe for the same reasons. So, sioni ubaya wa utaratibu kama huu wa kukopesha watumishi. Cha msingi ni kuweka utaratibu wa watu wengi zaidi kuweza kukopa. After all wasipokopeshwa watumishi, wajanja watakuja na maarifa tofauti (e.g. EPA) na pesa zitaishia kwenye mabenki ya Jersey, Uswisi e.t.c.
   
 11. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  We chapa kazi usiangalie jikoni watu wanapika nini maana unaweza ukaacha kufanya kazi yako ya kuwasaidi watanzania masikini kwasababu ya wezi wachache.
   
 12. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  sawa, but is your assumption correct? hii ni mara yao ya ngapi kupata mkopo huo? mapato ya mwezi (mshahara) wa hao mabossi ni kiasi gani? Mbona ni wafanyakazi wa BOT tu ndo wanaopata huo mkopo?

  Je hakukuwa ni nyia nyingine ya BOT kujenga nyumba za wafanyakazi? Je, ni kweli hao wafanyakazi hawana nyumba?

  Hapa tunatakiwakucheza na vipaumbele siyo mahitaji.
   
 13. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii mikopo ni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba! Nafikiri ni sahihi na inamsaidia mfanyakazi! Mashirika mengine na ya watu binafsi wanatakiwa kuiga jambo hili ! Safi sana BOT mmeona mbali
   
 14. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Cjui hii wizara yetu ya mifugo na uvuvi inasubiri nini na sisi kutuka kamkopo... kila kukicha story za mikopo ni huko huko tu mjini huku Tazara hamna??
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  What about us who don't work for BOT? Where shall we go to get those house loans? Infact those are soft loans because even if somebody leaves the bank or dies, the house would never be taken back to BOT, isn't?
   
 16. n

  nyakyegi Member

  #16
  Dec 15, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hapa nimejaribu kuangalia ni jinsi gani baadhi ya watu humu wana upeo mdogo kifikra.
  hivi ni makampuni mangapi yanakopesha wafanyakazi wake?
  na huwakopesha kiasi gani?
  hurudisha mkopo kwa muda gani?
  je tumelinganisha na nani?, CRDB, NBC, NSSF, PPF, STANBIC, BARCLAYS, STANCHART, AKIBA ZAIN, VODACOM, TIGO LAPF. je haya hayawakopeshi wafanyakazi wake??
  hawa wafanyakazi wa BOT hawana right ya kukopeshwa na mwajili wao?
  KAMA SEKULA YAO ILIVYOONYESHA KUWA HII NI NYONGEZA AMBAYO WAFANYAKAZI WAMEIOMBA KWA MUDA MREFU. JAMANI MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI.
  HIVI WHAT IS 30M KWA UJENZI WA NYUMBA??
  AMA HAWA WACHANGIAJI HAWAJAWAHI KUJENGA NA KUONA GHARAMA ZA UJENZI??
  HEBU TUUULIZIEN MAKAMPUNI MENGINE HUKOPESHA WAKURUGENZI WAKE KIASI GANI?? HAPO WE CAN ARGUE WITH EVIDENCE.
  SIO KWA KUWA KULIKUWA NA SCANDAL YA EPA NA TWIN TOWERS BASI MAANA YAKE WAFANYAKAZI WALIO WENGI WASIPEWE HATA HAKI ZAO ZA MSINGI.
   
 17. A

  August JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Dogo/Kubwa hapa watu wanazungumzia in general , je watu wa wizara zingine kama kilimo inakuwaje, wa afya nk nk, na ni % ngapi ya Watanzania wapo kwenye hizo institution ulizo zitaja hapo juu.
  Kinachogombaniwa ni kwanini serikali isiwe na sera ambayo inamlenga kila mtanzania?
  Hata world health organisation wakisema dawa ya kitu fulani imepatikana , wanaangalia uwezekano wa watu wengi kuweza kuipata hiyo dawa, ikiwa ni aghali watasema dawa haijapatikana. sasa kama unavyo fuata hiyo slogan yako, kwamba utajitahidi kuelewa kabla ya wengine kukuelewa nafikiri sasa utaifuata inavyotakikana/ kuitekeleza.
  na kama unajua Biashara Zain au Vodacom, sio institution za kutoa mikopo hivyo ziada yao wanatakiwa wawekeze kwenye reaseach and development, kuboresha mitambo etc, na ndio maana mashirika yetu yana feli kwa sababu ya kushindwa kuelewa majukumu yao ni nini, na ku-specialise huko. Hichi unacho ki-preach ndio kina sababisha mashirika kama bandari badala ya kununua winch, waende kutoa mikopo nk nk.
  Na hata kama makampuni mengi hukopesha wakurugenzi, haku halalishi hiyo sera. na hiyo pia inatakiwa kuzungumziwa au kupigiwa kelele.
  Na kuongezea ni kwamba Zain, au Voda nk kwa kuwa hiyo sio biashara yao watakuwa na limited resource za kuweza kutoa mikopo, matokeo yake hiyo sera iaonekana ni ya kibaguzi, kwamba wengine wamepata wengine hawakupata.
  kama hiyo unayosema kwamba kuna wakurugenzi kwenye mashirika/kampuni/serikali wanapata wengine hawapati.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio watu wa BOT kupewa mikopo. BOT ni institution ya selikali inayoendeshwa kwa kodi za wanachi, kudadisi mambo yanavyokwenda sio kosa. Kama kuna fairness basi hata wale walioko kwenye mawizara na idara nyingine za serikali nao wapewe mikopo. Kwa mfano, hivi TCRA au EWURA nazo si idara za serikali tena zinakusanya kiasi kikubwa tu cha pesa kama agency fee. Kwanini na wao wasipeane hizo soft loan?
   
 19. bona

  bona JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  wafanyakazi wa benki kuu wanadhani wanastahili kulipwa zaidi ya watumishi wote wa umma eti tu kwa sababu wanafanyakazi benki kuu,hii si sahihi hata kidogo ni suala tu la division of labour ndio maana wao wakawa hapo sio kwamba wao ni bora kuliko wengine au wanazalisha zaidi ya wengine, binafsi si mwajirirwa wa serikali lakini kwa wafanyakazi wa serikali kulipwa tofauti wenye qualification zinazofana haiingiii akilini eti tu kwa sababu wwako bot na mwingine yuko halmahsauri ya kiteto(mfano) na si ajabu dereva benki kuu akawa analipwa zaidi ya afisa kilimo uko nzega.
  kama ni nyumba iwe ni universal police kuwe na benki ya nyumba kila mfanyakazi wa serikali akope ili kuleta usawa!
   
 20. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Really interesting and tempting..,
  inabidi kwa udi na uvumba nipate kanafasi BOT hata u-mesenja...
  Kumbe waTz wanafanyaga kazi pande hizo,sisi wengine tutafute nchi yetu...
   
Loading...