BOT washusha statutory Minimum reserve toka 10%-8% hii inaashiria nini kwa uchumi na kuadimika pesa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,884
IMG-20170322-WA0063.jpg
 
Wanaongeza ulojolojo wa kifedha mtaani jambo ambalo si baya. Kwa hiyo kama benki ilikuwa inabana mikopo sasa itaiachia.
 
Huu huongeza mzunguko wa pesa maana sasa kiwango ambacho kingekaa bot sasa kinarudishwa uraiani
 
wachumi waje watufafanulie kwa kina, hii ni akiba ya mabank katika Bank kuu, au, ni Akiba ya Fedha za Taifa au serikali ndani ya Bank kuu.

Hii ina maana gani kwa Mtanzania wa kawaida?
 
Ni hatua nzuri,Sasa wakopaji wataweza kukopa kwa akili ya biashara na Ujenzi wa Tanzania ya viwanda,na ukizingatia mabank nayo pia Kwa sasa yamepunguziwa riba ya kutoka asilimia 16 hadi 12 ya kukopa Bot
 
Moja ya njia ya kuongeza money supply in economy, wanaiongeza mzunguko Wa pesa katika uchumi kwa kulegeza kiwango cha akiba(minimum reserve requirement) ya mabenki katika benki kuu.
 
Wameshusha kiwango cha hela za wateja (dhamana) kinacholazimika kubaki kwenye benki. Zamani benki iliruhusiwa kutumia hadi asilimia 90 ya dhamana za wateja kufanya biashara za ukopeshaji, unuzi wa tb etc. Sasa hivi wanarusiwa kutumia mpaka asilimi 92.
 
Back
Top Bottom