Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
BoT katika taarifa yake imeeleza kuwa inatambua juu ya uwepo wa watu wanaofanya malipo kwa kutumia sarafu hizo na yapo matukio ya uhamasishaji wa sarafu hizo
Wapo wanaodai kuwa wamewasiliana na Benki Kuu kuhusu uhalali wa matumizi ya sarafu kauli ambazo ni potofu
Taarifa ya BoT imewaonya wote kuwa biashara na uhamasishaji wa sarafu hizo ni kinyume na kanuni za udhibiti wa fedha za kigeni
====
TAARIFA KWA UMMAKUHUSU FEDHAZA KIMTANDAO
Benki Kuu ya Tanzania imeshuhudia kuwepo kwa wananchi wanaotumia fedha za kimtandao (cryptocurrencies) katika kufanya malipo hapa nchini. Aidha, Benki Kuu inatambua kwamba kuna matukio ya kuhamasisha biasharaya fedhahizi za kimtandao hapa nchini ili zionekane kamani fedha halali kwa ajili ya kufanya malipo. Vitendo hivyo ni pamoja na baadhi ya watu kudai kwamba wamewasiliana na Benki Kuu kuhusu matumizi ya fedha hizo za kimtandao.
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutahadharisha umma kwamba uuzaji, uhamasishaji wa biashara hiyo na matumizi ya fedha za kimtandao ni kinyume chakanuni za udhibiti wa fedha za kigeni.
Benki Kuuya Tanzania, kama taasisi pekee hapa nchini yenye mamlaka ya kuchapisha noti na kutengeneza sarafu na kuamua fedha halali kwa ajili ya matumizi hapa nchini,kama ilivyoainishwa kwenye Vifungu vya 26 na 27 vya Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006, inautarifu umma kwamba Shilingi ya Tanzania ndiyo fedha halali kwa ajili ya kufanya malipo hapa Tanzania. Fedha zingine za kigeni zinauzwa na taasisi zilizosajiliwa hapa nchini kwa mujibu wa taratibu zilizopo za kubadilisha fedha za kigeni. Fedha hizo zinazonunuliwa zinarudishwa kwenye nchi husika kwa mujibu taratibu zilizopo.
Hivyo, kwa taarifa hii, umma unatahadharishwa kutojihusisha na fedha za kimtandaona kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha kanuni zilizopo za fedha za kigenina kunaweza kusababisha hasara kwa anayehusika.