BoT Saga Unfolding: Meghji says I was duped by governor Ballali

Hapo wote ni WAOVU. Kwa upende mmoja kuna WEZI/MAFISADI na upande mwingine kuna WAZEMBE. Huyu mama yupo kwenye kundi la WAZEMBE

ok nimekuelewa..... tupambane kwa nguvu zote na "Wazembe" kama vile kuhakikisha polisi wazembe wote wanafungwa na kuchapwa viboko na ndio baadaye sasa tuangalie idadi ya polisi wetu watakaokwenda kukamata majambazi. Wote ni wakosaji cha muhimu ni nani wa kuanza kushughulikiwa, majambazi ama polisi? Kazi kwelikweli!!! Kama mtu ana lake kichwani haelewi kitu
 
Kwenye dili kama hii utakuta figure ya muombaji(RA) inakuwa ni ndogo tu,lakini katika kila mkono inapopita inaongezeka kutokana na hao watakayoipitisha kuweka cha juu chao.
Kutokea mwanzo ilijulikana ni wizi tu,sidhani kama Balali anaweza kumficha Waziri wake,wakati akijua iko siku hili litabumbulika.
Hivyo kwa mtazamo wangu,nadhani Rostam aliomba 'kupiga' labda $10m,Balali labda akaongeza $4m,Mgonja nae akaweka cha juu hivyohivyo,then mwishowe huyu mama nae 'analazimishwa' kwa kuwa kila mtu kaweka cha juu,huku wakikubaliana kuwa hili ni national security issue!
Sasa leo anamruka Balali,kwa kumuwahi tu kabla Balali hajasema yale anayojua.Maana ikumbukwe,sisi huku tutajua robo tu ya ukweli kamili.Na hii inaelekea ni mchezo wa Mawaziri wote wa fedha,hivyo huyu mama alijua hii dili ni clean.Kama sio hivyo,she shud have taken a leaf from Mbilinyi's book,maana nae alilengeshwa na mkwe wake hivyo hivyo na mwishowe akaishiwa ku resign.
Here she is trying to be aggresively defensive,lakini its too late.Yeye kama waziri ilikuwa ni lazima aipitie kwa umakini sana na kujua hizo National Security issues ni zipi.Kama ni usalama wa taifa,then obviously angecheki nao,kama ni jeshi vilevile pia>Lakini yeye kaamua kutulia na gavana ili walaji wawe wachache,maana figure ingeongezeka zaidi ya pale,labda kwa wao wanaona inge raise eye brows!
 
Wakati Dr Slaa alipotaka kuwekwa ndani eti kwa sababu alighushi nyaraka za serikali, wapenda haki na wapambanaji walisema huo ni ubinyaji mkubwa wa haki na kutetea mafisadi... Sasa sisi wenyewe tunajisahau, eti kwa sababu tu ni Waziri. Tujiulize makampuni 22 ni ya nani? Chanyikeni ni ya nani? HAMJUI MNAKALIA SIASA TUUUUUUUUUU, KUJIUZULU KUJIUZULU!!!! Naya kazi kwenu
 
Kwenye dili kama hii utakuta figure ya muombaji(RA) inakuwa ni ndogo tu,lakini katika kila mkono inapopita inaongezeka kutokana na hao watakayoipitisha kuweka cha juu chao.
Kutokea mwanzo ilijulikana ni wizi tu,sidhani kama Balali anaweza kumficha Waziri wake,wakati akijua iko siku hili litabumbulika.
Hivyo kwa mtazamo wangu,nadhani Rostam aliomba 'kupiga' labda $10m,Balali labda akaongeza $4m,Mgonja nae akaweka cha juu hivyohivyo,then mwishowe huyu mama nae 'analazimishwa' kwa kuwa kila mtu kaweka cha juu,huku wakikubaliana kuwa hili ni national security issue!
Sasa leo anamruka Balali,kwa kumuwahi tu kabla Balali hajasema yale anayojua.Maana ikumbukwe,sisi huku tutajua robo tu ya ukweli kamili.
Na hii inaelekea ni mchezo wa Mawaziri wote wa fedha,hivyo huyu mama alijua hii dili ni clean.Kama sio hivyo,she shud have taken a leaf from Mbilinyi's book,maana nae alilengeshwa na mkwe wake hivyo hivyo na mwishowe akaishiwa ku resign.
Here she is trying to be aggresively defensive,lakini its too late.Yeye kama waziri ilikuwa ni lazima aipitie kwa umakini sana na kujua hizo National Security issues ni zipi.Kama ni usalama wa taifa,then obviously angecheki nao,kama ni jeshi vilevile pia>Lakini yeye kaamua kutulia na gavana ili walaji wawe wachache,maana figure ingeongezeka zaidi ya pale,labda kwa wao wanaona inge raise eye brows!

Kazi kweli kweli, soma juu, fedha zilitoka 2005, Mramba akiwa Waziri mbona munakwepa? TUKISEMA UFISADI UMEINGIA HUMU MUTAKATAAA? Mramba anaogopwa wakati anahusika mwanzo mpaka mwisho
 
Wakati Dr Slaa alipotaka kuwekwa ndani eti kwa sababu alighushi nyaraka za serikali, wapenda haki na wapambanaji walisema huo ni ubinyaji mkubwa wa haki na kutetea mafisadi... Sasa sisi wenyewe tunajisahau, eti kwa sababu tu ni Waziri. Tujiulize makampuni 22 ni ya nani? Chanyikeni ni ya nani? HAMJUI MNAKALIA SIASA TUUUUUUUUUU, KUJIUZULU KUJIUZULU!!!! Naya kazi kwenu

Mkuu Halisi,

Kweli nashindwa kukuelewa unaongea nini juu ya hili. Yaani kama kweli mnataka kukomesha huu ufisadi na uzembe wote basi huyu mama ni mhusika mkubwa mno kwenye hii saga.

Labda sielwi unaongea nini lakini kwa kweli sioni siasa hapa kuhusu Meghji, alikuwa anajua, amelidanganya bunge, katudanganya sisi wananchi kwa kauri zake.

Hata hao wakaguzi kulikuwa na sababu gani wakati yeye kila kitu alikuwa anajua? Ballali kaenda hata bungeni kudanganya, yeye alikuwepo alisema nini?

Huyu mama wala hahitaji kujiuzulu, inatakiwa awe sacked. Tutakuwa wajinga mpaka lini?

Waafrika tunatukanwa sana nje huku shauri ya ujinga na uroho wa kakundi kadogo ka viongozi wetu. Tena viongozi wenyewe wanalipwa vizuru mno kuliko hata wanasiasa wa Europe, lakini ni tamaa tupu kila siku.
 
Halisi mi nakupata. ZM ni mzembe na ametuangusha lakini tukiangalia bigger picture mwenye uamuzi wa kumfuta kazi ni mkuu wa kaya na kwa Tanzania ule utamaduni wa kujiuzuru hatuna. Mi nadhani tuwachambue hawa wezi na mafisadi wenzao hata kama hatuwezi kuwalazimisha kuachia ngazi tutawapa dataz akina Slaa na wengineo wazianike! Taratibu tutafika.

Ila kwa kweli media ya Tanzania (save thisday), kwa kweli inatuabisha kama taifa! Sijui wanafanya kazi gani. Ni yale yale tulisema...elimu yetu inatutayarisha kuwa watu wa kukariri! Hatuna critical journalists.

Harafu kesho JK anaenda kupitisha bakuri la kuomba top up ya budget? where are we going as a nation??

Harafu watu wanataka kuandamana kumpongeza raisi? You know what? ngoja watanzania kwanza tupigike kwa ujinga wetu, itafika kipindi tutajua kudai haki yetu bila kusukumwa!
 
Duped or not she demonstrated a high degree of incompetency.If indeed she was duped, then she does not understand or neglected the overseeing nature of her job. You cant just let somebody throw the national security clause and sign millions of dollars
 
Mtanzania afukuzwe kwa sababu watu walikula wakati yeye hajaingia ofisini? well kama ni kulinda mafisadi at least alikugundua kosa lake na kulisahihisha, suala la kudanganya wananchi, as long as kulikuwa na uchunguzi/ukaguzi unaendelea asingeweza ku pre-empty matokeo yake na kuanza kutoa ripoti in piece-meal.

Haya utayajua iwapo tu utakuwa umefanyakazi serikalini.....
 
Masanja afadhali unanielewa. Tuweke mizani mzembe vs jambazi najua wote ni mafisadi kwa namna moja ama nyingine, lakini anayepambana na mafisadi ukimpiga vita na wewe unakua FISADI ZAIDI. Hamjui ama hamtaki kujua. Nimetoa mfano wa Dk Slaa kwa kuwa yeye alikua na mahali pa kuishambulia serikali, walio ndani ya serikali ambao wanatuunga mkono ni wengi na Zakia ni mmoja wapo na ameonyesha kwa vitendo, sasa tunasema TUMPIGE MAWE... Haya TUENDELEE, na tutasikia kwa mara ya kwanza CCM wanaandamana na wanabeba mabango, "MEGHJI AONDOLEWE" bila kutaja Jitu Patel and coligues
 
Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote..!
Nchi yangu Tanzania fedha zako ni tamu sana,
Walalapo nazichota wewe, waamkapo nawadanganya!
Tanzania TAnzania, Benki yako ni tamu sana!
 
Kazi kweli kweli, soma juu, fedha zilitoka 2005, Mramba akiwa Waziri mbona munakwepa? TUKISEMA UFISADI UMEINGIA HUMU MUTAKATAAA? Mramba anaogopwa wakati anahusika mwanzo mpaka mwisho

Halisi, sisi pia hatukatai kwamba akina Mramba na wenzake ndio engine ya huu ufisadi. Tunachosema sasa ni kuwa kwa vigezo alivyotoa Dk Slaa vya mtu fisadi, dada Zakia naye anaingia humo moja kwa moja. Kumbuka vigezo vya Dk Slaa vya ufisadi ni pamoja na: kufumbia macho au kutochukua hatua... nami naongeza kingine kuwa ni pamoja na kutetea ufisadi ama kwa kujua au bila kujua kama alivyofanya dada Zakia. Lakini nakubaliana na wewe kuwa huyu mama asitutoe kwenye focus; yeye kajiingiza vizuri, kwa hiyo tuendelee kuwabana akina Mramba, mosi, watoke serikali na, pili, wafikishwe mbele ya haki na tatu, wafilisiwe. Sasa vijana wetu wa CKD tunatarajia wafanye maandamano mengine along this line.

Nauliza tena wana CCM mtaendelea kutetea haya?
 
Duped or not she demonstrated a high degree of incompetency.If indeed she was duped, then she does not understand or neglected the overseeing nature of her job. You cant just let somebody throw the national security clause and sign millions of dollars

Again misleading tena makusudi kabisa. Nani kasaini millions of dollars?
 
Nauliza tena wana CCM mtaendelea kutetea haya?

Kitila sisi CCM tutadumu milele, maana tunaweza kuwatoa watu katika mstari kiulaini! Wakizinduka hawajui nani ni nani na wapi pa kushika. Wengi ni wajanja na wajuaji. Sisi CCM hakuna msomi ni sisi kina Khadija Kopa, Tambalizeni tunapeta na kule Zenji tunasema, "Tunachukua tunaweka waaa!!!" "Mapinduzi Daima... na hayapatikani katika sanduku la kura"

Hao ndio SISI "EMU" sisi kina "M", Mahalu, Malegesi, Meghji, Mkapa etc
 
Taarifa muhimu ni kwamba yule jamaa anayegawa magari mekundu kwa dada zetu ameanza kula kibano na vijana wa kazi, na huenda akafikishwa mahakamani soon. Waziri mmoja naye amebanwa mpaka akasema wanampotezea muda atafutiwe ofisi katika majengo alikokua amewekwa..... Kazi kweli kweli
 
Mtanzania afukuzwe kwa sababu watu walikula wakati yeye hajaingia ofisini? well kama ni kulinda mafisadi at least alikugundua kosa lake na kulisahihisha, suala la kudanganya wananchi, as long as kulikuwa na uchunguzi/ukaguzi unaendelea asingeweza ku pre-empty matokeo yake na kuanza kutoa ripoti in piece-meal.

Haya utayajua iwapo tu utakuwa umefanyakazi serikalini.....

Mkuu Masatu,

Meghji alitakiwa wakati ule ule alipojua angetoka clean. Lakini yeye alikaa kimya, badala yake akawakashifu waliokuwa wanatoa hizo habari. Ballali kaenda mpaka bungeni kwenda kulidanganya bunge, yeye yuko pale anaangalia tu.

matokeo yake nchi imetumia si ajabu bilioni nyingine kufanya uchunguzi ambao yeye alikuwa anaujua. Hivi huko ni kuwajibika gani? labda Tanzania mnatumia vipimo vyenu ambavyo viko chini mno.

Yeye na Ballali ni mwanzo tu, kuna akina Mramba na Mkapa ambao ndio hizo pesa zilitolewa wakiwa madarakani. Lakini Meghji pia yumo kwenye kundi hilo hilo.

Yaani maishani mwangu sikuwahi kuamini kwamba pesa zetu zinaibiwa kirahisi hivyo tena na watu wale wale ambao kila siku wako kwenye vikao na wazungu kama omba omba.

Lazima ifike mahali tuseme NO, kwenye huu ujinga. Waafrika tutaendelea kunyanyasika mpaka lini duniani shauri ya watu ambao hata hawana huruma ya watoto na akina mama wanaokufa hospitalini kwa kukosa dawa?

INASIKITISHA SANA! Wewe imagine mtu kama Ballali kweli anahitaji kuiba? Amefanya kazi miaka zaidi ya 20 WB, huko BOT kwenyewe ana mshahara wa maana
kuliko hata mawaziri, kweli kuna haja ya kuanza kushirikiana na mafisadi ili kuiba? Tumezidi sana uroho!
 
OK,mie naomba waendelee kujitetea tu kabla mwenyewe hajarudi,lakini akirudi ataumbuka mtu hapa. Huyu ma mkubwa naye anatuchanganya inatakiwa tumpake sana kwa unafiki, nakubaliana sasa kabisa na wana jf kwamba "eeh mola umlinde balali huko aliko, asife arudi salama ili tujue yaliyomo kifuani kwake" naam tunahitaji upande mwingine wa shilingi
 
Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote..!
Nchi yangu Tanzania fedha zako ni tamu sana,
Walalapo nazichota wewe, waamkapo nawadanganya!
Tanzania TAnzania, Benki yako ni tamu sana!

Nitakuomba kibali tukatengeneze CD nimeimba hapa watu wameshangilia kishenzi, hadi watoto wa vigogo wamekasirika, maana siku zao zinahesabika
 
Halisi unatuchanganya....mara unamtetea Meghji mara CCM mara watoto wa mafisadi...exactly unachosema nini hapa ? Kwamba tunamsingizia ZM au?
 
Taarifa muhimu ni kwamba yule jamaa anayegawa magari mekundu kwa dada zetu ameanza kula kibano na vijana wa kazi, na huenda akafikishwa mahakamani soon. Waziri mmoja naye amebanwa mpaka akasema wanampotezea muda atafutiwe ofisi katika majengo alikokua amewekwa..... Kazi kweli kweli

Du hiyo kali, kama na waziri naye ameshikwa shati basi hata heshima ya hiyo Cabinet yenyewe sana imeporomoka. Kuhisiwa kwanza ni tosha, na kushikiliwa hiyo nayo ni nzuri kweli, kweli mwaka 2007 imeibua mengi, tusubiri mengine zaidi!
 
What a ridiculous admission! Zakia should stop insulting our intelligence and RESIGN! At least she will show the way forward, for being accountable! Duped? Indeed!

Way back in 2000, during the General Elections campaign, I wrote somewhere that, Tanzania is akin to a dramatic play that has no script, the lead players can change at any given time, and there is no director!

I am being proven right!

Nuff said!
 
Back
Top Bottom