BoT Saga Unfolding: Meghji says I was duped by governor Ballali

Mimi nadhani hizi ni stories za kawaida ambazo wadanganyika tunapewa kila kukicha kunapotokea fraud kama hizi. Jamani si watuonee hata huruma wanatukamua sana.
 
Prelude to cabinet reshuffle or disollution! Kwanza twasikia RA kakimbia, kisha RA anakanusha kuchomeka vidole kwenye thupu la BOT kwa kutumia mkate wa Caspiani, then JK asitisha maandamano ya kutukuza Chama, kisha huyu Mama anakuja angua kilio kama Hilari wa Klintoni " Bilalli alinidanganya"

Mbona alimtolea nje Msabaha kuidhinisha mkopo kwa Richimonduli, ndipo Msabaha akakimbilia Ikulu na kuumnbuliwa kuwa atajinyonga?

Hivi wanachama wa CCM ni wapumbavu kiasi hichi waandamane kushangilia kuanza kuangamia kwa Chama chao?
 
Mama jifanye unaenda kwenye horney moon na Rostam then ujiuzulu juu kwa juu maana ukiondoka kwa staili ya kwenda kupata matibabu watu watakustukia.
 
Ili kazi ifanyike ni lazima kuwe na mgawanyo wa kazi n.k, kwa maana kuwa kila mtu pale alipo anafanya kazi kulingana na dira/mwelekeo wa idara au kampuni husika.
Si mlaumu huyu mama kusign barua ya governor etc, ila ninachoshangaa ni kwa nini alikaa kimya? baada ya kujua kwa nini hakuchukua tahadhari na hatua dhidi ya gavana na hiyo Kigoda? inawezekana mwenye kigoda ana mjua ndio maana akawa kimya! na yeye lazima achukuliwe hatua!
 
moderator please unganisha thread ya kuhusika kwa waziri meghji kwenye hili sakata iwe moja ....iliyotangulia...tuwe na flow of information..

members please ukiona thread ipo....usianzishe nyingine ..changia humohumo....kwa hili maoni yangu tubakie na thread mbili za bot...ile ya balali atolewa kafara iendelee ...na moja kati ya hizi za meghji..mnaonaje??
 
moderator please tubakie na thread mbili...moja ya balali atolewa kafara..na moja kati ya hizi za kuhusika waziri meghji...

members naomba mkiona thread ipo msianzishe nyingine...mnaonaje!!?
 
Punguza hasira mzee, kwenye nchi kama hizi utakufa kwa hasira. Maana kuna mambo yanashangaza kweli,ina maana bila hawa jamaa wa nje kuja kutu audit huyu mama angekaa kimya na kutetea kuwa kihenge chetu ni safi kabisa na hakina panya. kumbe panya yupo katikati ya mahindi yetu anayapekechua tu. oooh my God Wadanganyika hali hii mpaka lini. Unajua mtu akikudanganya tayari ameshakuona wewe ni zezeta utakubaliana na uongo wake tu kwa kuwa wewe ni mjinga. Mmh hapo mimi naona bora niitwe mpumbavu, nawakumbusha wenye meno kuwa si kila mfupa utavunjika kwani mifupa mingine ni ngangari bwana.
 
usishangae sana ..ukweli unajulikana kuwa balali alikuwa ana act on his superiors....nyingi zilitumika wakati wa uchaguzi..ndio maana wizi umetokea 2005 ..mtu yoyote mwenye busara anatakiwa awe makini sana kushangilia kufukuzwa balali.....kama angekuwa kajichukulia angekuwa detention na hata njia ya kwenda airport asingeiona.....

muungwana kwa kujua hayo tayari amechukua hatua kuzima maandamano ya wana ccm nchi nzima KUPONGEZA UAMUZI WAKE WA KUMTIMUA BALALI..jk yuko makini sana kwenye hili..na kama mwanasiasa aliyeiva anajua ..muda wowote habari inaweza kuwageukia...ndio maana amemwagiza mkuu wa itikadi na uenezi asimamishe maandamano kwa sasa kwa kuwa sio political timely....

kama huu ni uzinduzi wa santuri ..huu ndio wimbo wa kwanza uliobeba album...bado kabisa album haijachezwa yote tulieni watatajana tu.....wimbo wa mwisho ataimba balali mwenyewe feuturing mwanasheria wake ..huu utakuwa funga kazi!!!!!

Kuna aina fulani ya unafiki imo ndani ya CCM kuna watu wana-act kwa kutaka kuonekana. Thisi is a National Issue nashangaa sana wakati Dr Slaa analipigia kelele hao hao wanaotaka kuandamana walikuwa wamefumba midomo na masikio kujifanya wanaosemwa wanaonewa, Mh Rais alivofanya wanaibuka juu juu kutaka kuandamana, napendekeza polisi wazuie maandamano yao. Lakini bora mwenyewe kawazuia. Hakuna mwenye furaha huko juu wote roho juu.
 
.. Zomba, nimepita "kule", mkuu watu wako wanakulilia, wanasema umewatupa siku hizi. Nikataka niwaambie kuwa siku hizi muda mwingi uko huku nikamezea... (Joke meant for Zomba)
 
Huyu mama sasa yuko kwenye shopping spree ya nyumba hapa mjini. Isije ikawa ni hizo hela za Kagoda na magogo.
Si hiyo tuu, wakati yupo mali asili, mwanawe (kama ni huyo huyo alyenunuwa mikocheni au mwengine sina uhakika) alinunuwa (nunuliwa) nyumba ya serikali au shirika la umma, pale Upanga, nyumba yenyewe ipo exactly opposite na msikiti wa Tambaza. Baada y kununuwa/nunuliwa ile nyumba ikala renovation sio ya kawaida. Sijui mshahara wake ni kiasi gani, lakini kwa bei za nyumba kwa sasa, hasa prime area kama upanga, mikocheni na kadhalika, ujuwe jimama lina mihela mingi tuu, kaipata wapi mihela yote hiyo? kama si ufisadi na dhulma ni nini? Jee hujuwi system ni nini?
 
usishangae sana ..ukweli unajulikana kuwa balali alikuwa ana act on his superiors....nyingi zilitumika wakati wa uchaguzi..ndio maana wizi umetokea 2005 ..mtu yoyote mwenye busara anatakiwa awe makini sana kushangilia kufukuzwa balali.....kama angekuwa kajichukulia angekuwa detention na hata njia ya kwenda airport asingeiona.....

muungwana kwa kujua hayo tayari amechukua hatua kuzima maandamano ya wana ccm nchi nzima KUPONGEZA UAMUZI WAKE WA KUMTIMUA BALALI..jk yuko makini sana kwenye hili..na kama mwanasiasa aliyeiva anajua ..muda wowote habari inaweza kuwageukia...ndio maana amemwagiza mkuu wa itikadi na uenezi asimamishe maandamano kwa sasa kwa kuwa sio political timely....

kama huu ni uzinduzi wa santuri ..huu ndio wimbo wa kwanza uliobeba album...bado kabisa album haijachezwa yote tulieni watatajana tu.....wimbo wa mwisho ataimba balali mwenyewe feuturing mwanasheria wake ..huu utakuwa funga kazi!!!!!

Kuna aina fulani ya unafiki imo ndani ya CCM kuna watu wana-act kwa kutaka kuonekana. Thisi is a National Issue nashangaa sana wakati Dr Slaa analipigia kelele hao hao wanaotaka kuandamana walikuwa wamefumba midomo na masikio kujifanya wanaosemwa wanaonewa, Mh Rais alivofanya wanaibuka juu juu kutaka kuandamana, napendekeza polisi wazuie maandamano yao. Lakini bora mwenyewe kawazuia. Hakuna mwenye furaha huko juu wote roho juu.
 
usishangae sana ..ukweli unajulikana kuwa balali alikuwa ana act on his superiors....nyingi zilitumika wakati wa uchaguzi..ndio maana wizi umetokea 2005 ..mtu yoyote mwenye busara anatakiwa awe makini sana kushangilia kufukuzwa balali.....kama angekuwa kajichukulia angekuwa detention na hata njia ya kwenda airport asingeiona.....

muungwana kwa kujua hayo tayari amechukua hatua kuzima maandamano ya wana ccm nchi nzima KUPONGEZA UAMUZI WAKE WA KUMTIMUA BALALI..jk yuko makini sana kwenye hili..na kama mwanasiasa aliyeiva anajua ..muda wowote habari inaweza kuwageukia...ndio maana amemwagiza mkuu wa itikadi na uenezi asimamishe maandamano kwa sasa kwa kuwa sio political timely....

kama huu ni uzinduzi wa santuri ..huu ndio wimbo wa kwanza uliobeba album...bado kabisa album haijachezwa yote tulieni watatajana tu.....wimbo wa mwisho ataimba balali mwenyewe feuturing mwanasheria wake ..huu utakuwa funga kazi!!!!!

Hapo Balali anakuwa Mshindi wa BOT STAR SEARCH
 
Kuna aina fulani ya unafiki imo ndani ya CCM kuna watu wana-act kwa kutaka kuonekana. Thisi is a National Issue nashangaa sana wakati Dr Slaa analipigia kelele hao hao wanaotaka kuandamana walikuwa wamefumba midomo na masikio kujifanya wanaosemwa wanaonewa, Mh Rais alivofanya wanaibuka juu juu kutaka kuandamana, napendekeza polisi wazuie maandamano yao. Lakini bora mwenyewe kawazuia. Hakuna mwenye furaha huko juu wote roho juu.

Huu ni unafiki wa wazi mzee kwani hii ishu ilipo anza si walisema ni uzushi wa wapinzani? Tena akina Kingunge nao wakasema hizi ni siasa chafu za wapinzani hakuna mambo ya ufisadi. Mzee wa double standard Kingunge sijui sasa anasema nini. Jamani waandishi wa habari naombeni mmhoji huyu mzee tuone kama atarudia maneno yale na aseme yeye kama mzee wa chama inakuwa je sasa wanataka kuandamana na wakati walipingana na hoja ya silaa?

Wakuu wale watu wote waliotishia kwenda mahakamani waliishia wapi?
Au nao JK aliwapiga mkwara?


CCM wanachekesha sana kila penye mwanya wa kujipatia umaarufu wanataka kujipenyeza wananikumbusha walivyo msifia Richard kwa kufanya Ngono
 
Tanzania!, Tanzania!

1. Maneno haya ya Balalli kwa Zakhia(kama ni kweli) yameweka wazi kwamba fedha ziliolewa kwa 'matumizi nyeti ya serikali'- na kwa kuwa Balalli aliyesema akiwa kifua mbele- inaashiria kwamba kuna fungu lilikuwa kwa 'matumizi nyeti ya serikali ya wakati huo'(soma: kwa ajili ya Mkapa na wenzake kugharamia uchaguzi uliomwingiza Kikwete madarakani) lakini pia hapo hapo Baadhi ya wale waliomo kwenye "Orodha ya Mafisadi" wakatumia mwanya huo kujichotea fedha kwa ajili ya 'matumbo' yao binafsi. Hivyo, Balalli ataje waliomtuma- na aliowakabidhi! Sijui kwanini waziri wa fedha wa wakati huo na Katibu Mkuu wake wasichukuliwe hatua kabla hata ya Gavana wa Fedha bwana Balalli? Sijui kwa nini katika mazingira haya bado tunaendelea kuambiwa Mzee Mkapa aachwe apumzike!

2. Bi Zakhia Meghji anapaswa kujiuzulu mara moja- mtu akikudanganya, ukiwa na uwezo wa kujua kudanganywa huko, lakini ukakubali kudanganyika- wewe ni sehemu ya uongo huo- ama kwa kuwa mmoja wa waongo hao au kwa ujinga wa kuukubali uongo huo!. Waziri wa Fedha ni cheo kikubwa sana, unapokubali Gavana wa Fedha akwambie matumizi haya ni SIRI ya serikali, wewe kama mtunza siri ukashindwa kuhoji ni siri gani hiyo; wewe hujui kazi yako! Upaswa kujiuzulu mara moja. Kuna uwezekano mkubwa Bi Zakhia Meghji anaendelea kuwadanganya watanzania; inawezekana kabisa Balalli alimwambia wazi ni matumizi gani hayo nyeti yaliyofanywa na awamu iliyopita ndio maana akakubali kuisaini ile barua. Sasa kwa kuwa Balalli anaelekea 'kunyongwa' ni lazima Bi Zakhia na wengine wamkane mara tatu kabla jogoo halijawika.

Wasichojua Bi Zakhia na Wenzake ni kwamba watu wachache wanaweza kudanganyika kwa muda mchache lakini si watu wote wakati wote. Kazi kwako Rais Kikwete, kijua ndio hiki- usipouanika, utautwanga mbichi.

Natoweka

JJ
 
Hivi Meghji kuwa ni mtu wa Mkoa upi na kwa nini hajawahi kuomba kura za wana jimbo ila anapewa kwa kuteuliwa Ubunge wa Bure na kila akipewa Ubunge wa bure bado uwaziri hakosi ? Amekuwa maliasili na Utalii naamini uozo huko utakuwa mkubwa zaidi.She give hazina ili kuficha ukweli wa kujichotea pesa kwa ajili ya Kampeni . Nakubaliana na Phillimon kwa asilimia kubwa .Balali hajaiba .
 
Meghji, Mramba wajiuzulu - Wapinzani

Ushirikiano wa vyama vinne vya upinzani Wilaya ya Tanga, umemtaka Waziri wa Fedha, Bi. Zakia Meghji na yule wa Viwanda na Biashara, Bw. Basil Mramba kujiuzulu kutokana na kashfa ya ubadhirifu wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Wakati wapinzani Tanga wakitoa tamko hilo, jijini Dar es Salaam, Dk. Wilbroad Salaa naye amemtaka Waziri Meghji kujiuzulu.

Katika mkutano wao wa hadhara mkoani Tanga, vyama vya CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na CUF, vilidai kwamba kwa kuwa ubadhirifu huo umetokea chini za wizara zao, wanatakiwa kujiuzulu ili kumrahisishia kazi Rais Kikwete ya kusafisha nchi.

Tamko hilo lilitolewa jana na makamu mwenyekiti pamoja na katibu wa CHADEMA Wilaya ya Tanga, Bw. Mohamed Waziri na Bw. Rashid Khalid katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mabawa jijini hapa.

Walisema, mawaziri hao ni viongozi wa juu wa wizara hizo na kwamba wanao wajibu wa kusimamia Benki Kuu ambayo ni sawa na injini ya serikali, kuhakikisha hakutokei ubadhirifu wowote, lakini walishindwa kufanya hivyo hadi Rais Jakaya Kikwete alipoingilia kati.

Kwa mujibu wa viongozi hao, ubadhirifu uliotokea BoT ni kielelezo tosha kwamba mawaziri hao hawana uwezo wa kukemea vitendo viovu katika wizara zao, hali ambayo kimsingi inawatia wasiwasi wananchi kwamba huenda na wao walihusika kwa namna moja ama nyingine katika kadhia hiyo.

Wamemtaja Mramba kwa maelezo kwamba ndiye aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa miaka 10 kabla ya Meghji.

Walishauri kwamba mawaziri hao wakijiuzulu watajenga heshima kwao binafsi na kwa serikali ya awamu ya nne.

Wiki iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alimfuta kazi aliyekuwa gavana wa BoT, Dk. Daudi Balali na kumteua Profesa Benno Ndulu kuchuku nafasi yake.

Mbali na kumuondoa gavana, Rais Kikwete pia aliiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya BoT kukutana kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zinazopaswa za kinidhamu dhidi ya maofisa waliohusika.

Katika kashfa hiyo, fedha zinazotajwa kupotea ni kiasi cha Sh. bilioni 133 kutoka Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje (EPA) ambazo kati ya hizo Sh. bilioni 90.3 zililipwa kwa kampuni 13 hewa ambazo zilitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizobatili na za kughushi.

Naye Dk. Slaa, alisema hatua iliyofikiwa na Rais Jakaya Kikwete, kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk Daudi Balali, na kuviagiza baadhi ya vyombo vya dola, kuchukua hatua za kisheria, haitoshi kwake kumpongeza (Rais).

Alitoa madai hayo jana, alipohojiwa na Nipashe, kuhusu azma yake ya kuendeleza hoja ya utoaji wa taarifa zaidi za ripoti ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), kuhusu kashfa za BoT.

``Ndio maana hadi leo sijampongeza Rais Kikwete kwa hatua alizofikia kuhusu BoT, kwa sababu hoja iliyojengwa kwa kuangalia fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA), ni kasma ndogo kati ya mabilioni ya fedha zilizohujumiwa,`` alidai.

``Mimi nilitoa tuhuma zilizohusu matrilioni ya fedha, lakini inashangaza kuona wananchi wanaonyesha kuridhishwa na taarifa ya ufisadi wa Sh. bilioni 133 tu, hizo ni fedha nyingi sana, lakini pia ni kiasi kidogo ikilinganishwa na fedha halisi zilizoporwa BoT,`` alizidi kudai.

Kuhusu Bi. Meghji, Dk. Slaa, alitoa mfano kuwa, Waziri huyo, alishiriki kupinga ripoti iliyowahi kutolewa na kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya Delloit and Touche, ikielezea malipo hewa kwa kampuni ya Kagoda.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Bi. Meghji, alitoa tamko lenye kueleza kuwa, malipo yaliyofanyika kwa kampuni ya Kagoda, yalikuwa halali na yaliyotokana na shughuli za serikali.

Alidai kuwa, taarifa ya kampuni hiyo, ilipingwa na hatimaye Bi. Meghji, kuwafukuza wataalamu wa nje waliokuwa wanafanya kazi Delloit and Touche.

``Kwa hiyo utaona hapakuwa na sababu ya kutumia fedha nyingine kwa kampuni ya Ernst and Young, wakati taarifa za awali, ikiwamo ya Delloit and Touche, zilishabaini matumizi mabaya katika BoT,`` alidai.

``Kwa kuwa Meghji alishiriki kutoa taarifa ya kulinda uhalali wa malipo haramu kwa kampuni ya Kagoda, sioni sababu ya Rais Kikwete, kumuacha aendelee kuwapo katika wadhifa huo badala ya kumchukulia hatua kama zilizochukuliwa dhidi ya Balali,`` alisema.

Kuhusu hatua ya Rais Kikwete, kuitaka Bodi ya Wakurugenzi wa BoT kuipitia ripoti ya ukaguzi ya CAG, Dk. Slaa, alieleza wasiwasi kuhusu ufanisi wake.

Alidai kuwa, miongoni mwa mambo yanayosababisha wasiwasi huo, ni kuwapo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, miongoni mwa wajumbe wa Bodi hiyo.

Dk. Slaa, alidai kuwa Bw. Mgonja, alishiriki kusaini ripoti ya mwaka ya BoT ya mwaka 2005/2006, lakini saini yake na nyingine, zilionekana kuwa za mwaka jana.

Alipohojiwa kwa njia ya simu, Bi. Meghji, alikiri kuandika barua iliyopelekwa Delloit and Touche, ikihalalisha matumizi yaliyofanywa na kampuni ya Kagoda.

Alisema alifikia hatua hiyo, baada ya kufuatwa na Dk. Balali, aliyeomba kuandikiwa barua hiyo, kwa madai kuwa fedha zilizolipwa katika kampuni ya Kadoga, zilihusiana na masuala ya usalama wa nchi.

``Balali alinifuata na kuniambia fedha zilizolipwa Kagoda, zilikuwa for national security purposes (usalama wa Taifa), na kwamba Delloit and Touche walitaka barua ya ku-justify hivyo, nilimwambia akaandike na aliniletea, nikaisaini,`` alisema.

Hata hivyo, Bi. Meghji, alisema baada ya kusaini na barua hiyo kupelekwa Delloit and Touche, aliwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Gray Mgonja, aliyepinga hoja ya matumizi ya fedha zilizolipwa Kagoda, kwamba zilihusu usalama wa Taifa.

``Baada ya kupata maelezo hayo na kufanya vikao vya kiserikali, niliandika barua nyingine kwenda Delloit and Touche, kufuta barua yangu ya awali, na hivyo kumwagiza CAG kufanya ukaguzi uliosababisha Rais Jakaya Kikwete, kufikia hatua mnayoiona sasa,`` alisema.

``Kwa hiyo suala hili la ubadhirifu wa fedha za BoT nilianza kulishughulikia hata kabla ya Dk. Slaa, kupata vielelezo kupitia kwenye internet,`` alisema.

Naye Simon Mhina anaripoti kwamba, Naibu Gavana wa zamani wa BoT, Bw. Bob Makani, amesema Bodi ya Benki Kuu (BoT) haitafanikiwa kuwachunguza, kuwabaini na hatimaye kuwachukulia hatua maafisa wote waliohusika na kashfa ya ulipaji wa fedha kwa makampuni hewa kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Akiongea na Nipashe ofisini kwake jana Bw. Makani alisema Bodi hiyo ambayo mwenyekiti wake ni Gavana wa BoT, na wajumbe wengine ambao kimsingi sio watendaji, ndani ya chombo hicho hawataweza kufanya kazi hiyo.

Akifafanua, Bw. Makani ambaye pia ni mwanasheria, alisema ili bodi hiyo, iweze kufanya kazi ya uchunguzi, italazimika kupata taarifa na ushauri kutoka kwa watendaji ambao wanatuhumiwa kuhusika na ufisadi.

Alisema kimsingi Bodi ya BoT inahusika na kusimamia sera za chombo hicho tu.

Alisema kitakachotokea ni kwamba bodi hiyo inaweza \'kufukia\' baadhi ya mambo.

``Wajumbe wa hii bodi hawawezi kufanikisha kazi hii, hawa kazi yao ni kupelekewa taarifa ya utekelezaji wa masuala yahusuyo Benki Kuu na kisha hutafakari kwamba sera za kifedha hazijakiukwa, hawana jipya,``alisema.

Alisema kinachoshangaza zaidi ni kwamba watendaji wa Benki Kuu watakuwa wanajichunguza wenyewe, hasa ikizingatiwa kwamba Gavana ambaye ndiye bosi na mwajiri wao, ndiye mwenyekiti wa Bodi.

``Hapa lazima kutatokea mgongano wa kimaslahi, hapakuwa na sababu ya Bodi kupewa jukumu hilo,`` alisema.

Bw. Makani alisema kimsingi dhamira ya Rais Jakaya Kikwete kutaka uchunguzi ufanyike na watakaobainika kuhusika wachukuliwe hatua, ni njema, lakini angeweza kuteua chombo kingine kufanya kazi hiyo.

Alikumbusha kwamba sakata la wizi na kughushi BoT zilianza zamani mno, hivyo hana imani kwamba kuna wajumbe hawahusiki moja kwa moja au kwa kupitia njia nyingine katika kashfa hiyo.

Alisema kwa uzoefu wake wa miaka mingi ndani ya Banki Kuu, hana imani na Bodi hiyo kufanya kazi iliyoagizwa na Rais.

Bw. Makani alisema kinachomfanya asiwe na imani na bodi ni kwamba miaka ya nyuma ililetwa kampuni moja toka Afrika Kusini kwa ajili ya kukagua vitabu vya BoT, lakini ikawekewa mizengwe na kisha ikatimuliwa.

Alisema anazo taarifa kwamba kampuni hiyo na mwakilishi wake walitimuliwa baada ya kubaini mchezo mchafu katika ulipaji wa makampuni hewa kupitia akaunti ya EPA.

Alisema kampuni iliyotiliwa shaka na wakaguzi hao, imo kwenye orodha ya makampuni hewa yaliyobainika katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni uliofuatiwa na Rais Kikwete kutoa maelekezo kadhaa ikiwemo kumfukuza kazi Gavana wa BoT, Bw. Daudi Balali.

Bw. Makani alisema haamini hata kidogo kwamba wakaguzi hao waliondolewa bila baraka za bodi hiyo.

``Hili ndilo linanifanya nisiwe na imani na Bodi ya BoT kwa sababu imeshindwa kufuatilia mambo mengi sana, na siamini kwamba walishindwa kwa bahati mbaya, bali walifanya hivi kwa makusudi ya kimaslahi,`` alisema.

Alipoulizwa anashauri nini kifanyike, Bw. Makani alisema suala hilo linapaswa kushughulikiwa na vyombo vya dola.

Alisema kama ambavyo Rais alitoa agizo kwa Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Polisi na Mkurugenzi wa TUKUKURU, kuchunguza makampuni hewa yaliyolipwa, pia wangepewa jukumu la kuwasaka maofisa waliohusika.

``Kwa ushauri wangu hawa viongozi wa vyombo hivi vya dola, wangepewa majukumu yote kwa vile haya makosa ya makusudi yanaonekana yanakwenda pamoja,`` alisema.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom