BoT Saga Unfolding: Ballali ni Kafara

Halisi,
Naamini wapo. Data alizotoa Dr. Slaa alipewa na Watanzania waliochoshwa na uovu huu.
 
Sina ushahidi, lakini nasikia tayari kuna account 62, sita za Kagoda zimesimamishwa huko CRDB. Hayo yalifanyika siku sita kabla ya zogo la Balali kutangazwa, na pia yakaendelea hadi mapema juzi. Mwenye chanzo CRDB atafute taarifa zaidi wakuu JF.
 
na sasa Balali....the list is endless.

Wakuu Mwanakijiji, na Jasusi, endeleeni kutupa dataz hatuhitaji Death Certificate ili kuwaamini kuhusu yanayojiri na Gavana Balali,

hawa wakuu kuna wakati walituletea dataz za Mungai kuwa Waziri Mkuu na kwamba ameshapewa watu wa usalama wa kumlinda imebakia kutangazwa tu, sasa hao hao tena wanadai Death Certificate ili wasiamini kwamba Kombe mkuu wa Intelligence ya Jamhuri, kuuwawa kwake kwa kupigwa risasi na local police eti kwa kumfananisha na jambazi aliyekuwa akitafutwa huko kitongojini, ilikuwa ni Kolimbad style!

Hivi mtu mwenye position kama yake si huwa anafuatana na bodyguards, tena wengi sio mmoja na ni lazima afuatane na magari angalau mawili, na hata mahakama yetu bongo sio ya the Haque ilikubali kuwa kulikuwa na faulo na ikaamuru familia yake ilipwe karibu Shillingi Millioni 400, lakini kuna wanaotaka tuwaletee Death Certificate ambayo hata hakimu hakuihitaji katika kuamua kesi hiyo ya Wrongful Death mikononi mwa serikali,

Jasusi na Mwanakijiji tupeni dataz za ex-Gavana, tunazifuatilia kwa makini, na JF idumu maana hapa ndio mwanzo na mwisho wa dataz, hata Mwana-Halisi sasa huja hapa kutafuta dataz, uliza gazeti lao la juzi lilivyojaaa topic moja ya hapa ya "watoto wa Vigogo na BOT", na "NY", yaani wewe viongozi wanagawana nchi na kuchezeana akili, wewe unauliza Death Certificate?

Eti unataka Death Certificate ya RIP Amina Chifupa?

JF yaani idumu tu na kumkoma nyani mbele, huwa hatuangalii usoni!
 
mimi kuhusiana na ukimya wa jk na serikali kuhusiana na aliko balali na hali yake yanitisha...
kinachokera zaidi nafsi yangu ni kuwa wanawait akishakufa...ndio waibuke oooh tulikua tuna plan za kumleta tz aje ajibu tuhuma n doz kind of stuffs alaf azikwe kitaifa if not kishujaaa
 
Wandugu mimi nina wazo. Hivi hatuwezi kufikisha hii issue kwenye media za kimataifa kama BBC, CNN, FOX, SKY ili waweze kufuatilia hiki kilio cha watanzania??? Hawa jamaa wanaweza kumtrace alipo na kufanya mahojiano naye huyu dalali!! Tumechoka sasa, kila siku tunapiga kelele tu hapa, kila mtu na lake. Tunataka tusikie haya majambo kupitia media za kimataifa. Mwenye uwezo wa ku-influence hili atusaidie. Tutaendelea kubaki gizani mpaka lini???

...good idea lakini tutegemee western media kutufanyia kazi mpaka lini? hata wewe unaweza kumtrack down na hata akikataa kuongea na wewe na kusema hataki hiyo tayari ni news na itaongeza interest kwenye issue,anyway huyu nji fisadi tuu either kwa kuiba au kuachia mafisadi wateketeze account yetu(EPA),vipi kina Jeetu patel na Lukaza mbona hatuwapi nafasi humu maana nao ni wahusika wakubwa na inaonekana ndio waliochukua pesa zote,pls media zetu tafuta hao watu ili kucreate drama.
 
Mtaalam,
They know where he is. Hata alipokuwa Marekani rais alimpigia former gavana simu. Lakini wameamua kumfanya "sacrificial lamb." Nasikia kuna ripoti zitatoka kesho kutoka waziri wa fedha zikimshutumu gavana kwa kutomwambia ukweli. I wish I had been there to ask a few questions. Lakini waswahili wana usemi kuwa Mungu si Asumani. Ngoja Balali apate nafuu, aweze kuzungumza vizuri tu na mtasikia mavituz.
 
Mtaalam,
They know where he is. Hata alipokuwa Marekani rais alimpigia former gavana simu. Lakini wameamua kumfanya "sacrificial lamb." Nasikia kuna ripoti zitatoka kesho kutoka waziri wa fedha zikimshutumu gavana kwa kutomwambia ukweli. I wish I had been there to ask a few questions. Lakini waswahili wana usemi kuwa Mungu si Asumani. Ngoja Balali apate nafuu, aweze kuzungumza vizuri tu na mtasikia mavituz.

Ni kweli Jasusi, inaelekea una data, Waziri wa Fedha Zakia Meghji amekiri kuandika barua kuzuia wakguzi wa mwanzo kukagua akaunti ya Kagoda kwa madai kwamba fedha zile zimekwenda maeneo nyeti, lakini eti baada ya siku nne, akagundua amepotoshwa na Gavana Ballali, ambaye ndiye aliandaa hiyo barua kama mtaalamu wake. Baada ya kubaini kuwa kapotoshwa Meghji aliandika barua nyingine kuifuta ile ya awali akisema kwamba alisaini barua hiyo ya kwanza ya Septemba 15, 2006 kwa makosa kwa kumuamini Ballali na akawasilisha barua mpya Septemba 19, 2006 kuifuta ile ya awali. More datas kukicha hapa TZ tayari saa 11 alfajiri bado saa tatu tu mutasoma katika magazeti ya bongo
 
Kesho nitawawekea barua zote mbili hapa, kama magazeti yatakua hayajaweka
 
Halisi thanks for the link picha inaonesha barua vizuri kabisa ni maneno mawili matatu tu ndio hayaonekani! Lakini barua zenyewe zinaonekana zimeandikwa kitoto sana huwezi kuamni kama ni za kiserikali!
 
Ndugu wanabodi,

Ninafurahishwa sana na mchango wenu mzuri kuhusu hali ya siasa ndani ya Tanzania. Tatizo kubwa ni kwamba hakuna jambo ama hatua zinazochukuliwa ili kurekebisha hali. Hili la BOT la wizi wa mapesa ya wananchi na mengineyo hakuna kitu cha maana kitakachofanywa zaidi ya story na danadana nyingi sana kuchezwa.

Katika Nchi yetu hakuna haki itakayofuatwa na hasa uchafu ukifanywa na wana mtandao.

Ditopile alipiga mtu risasi na kuua mbele ya wananchi, leo yuko wapi?. Kama kutoa roho ya mtu CCM wanaona si kitu je kuiba mapesa itakuwa issue kweli kwao?. Kuwa formula ya kuwa tajiri Tanzania ni lazima uwe mwana chama wa chama cha mapinduzi na uwe mwana mtandao. Utafanya lolote utakalo hakuna cha kukufungisha break.
 
Back
Top Bottom