BoT na Ushindi wa kishindo wa JK: Mambo hadharani

kichwamaji

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
233
12
Sijui kama hii ilikuwa imewafikia. Someni wenyewe muone jinsi ushindi wa kishindo ulivyopatikana. Halafu watu hawa hawa watueleze usafi wa JK na kundi lake.

TAARIFA KWA WANANCHI WA TANZANIA

MABILIONI ZAIDI YALIIBIWA BOT WAKATI WA UCHAGUZI MKUU 2005!

Ndugu wananchi,

Tarehe 15 Septemba 2007 tulitoa Orodha ya Mafisadi yenye kuonyesha ufisadi, wizi na/au ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma unaowahusisha viongozi na watendaji wa juu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano na watu wengine walio kwenye uongozi wa umma. Hadi sasa Serikali haijatoa majibu ya kuridhisha kuhusiana na tuhuma hizi nzito licha ya madai ya kufanya hivyo kutoka kwa wananchi, taasisi zisizo za kiserikali, viongozi mbali mbali ndani na nje ya Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) na hata wawakilishi wa nchi wafadhili walioko Tanzania .

Leo tunaomba kuwajulisha wananchi wa Tanzania kupitia Mkutano huu Maalum na Wananchi wa Dar es Salaam juu ya taarifa zinazoonyesha kuwepo kwa ufisadi na/au wizi wa mabilioni mengine ya fedha za umma uliofanyika wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2005. Nyaraka mbali mbali ambazo tumezipata hivi karibuni zinaonyesha kwamba makampuni hewa (shell companies) kadhaa yalianzishwa katika vipindi tofauti kabla ya Uchaguzi Mkuu kwa lengo mahsusi la kupitishia fedha zilizoibiwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Nyaraka hizi vile vile zinaonyesha jinsi ambavyo fedha hizo ziliibiwa na kwa wakati gani kama ifuatavyo:

1. DEEP GREEN FINANCE COMPANY LIMITED

Mnamo tarehe 18 Machi 2004 ilianzishwa kampuni iitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. kwa madhumuni ya, pamoja na mengine, kufanya biashara kama ‘mabepari’ na wakopeshaji fedha! Kufuatana na taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakurugenzi wa Deep Green Finance walikuwa ni mabwana Mark Ross Weston wa New Zealand ; Anton Taljaard wa Afrika Kusini; na Rudolph van Schalkwyk pia wa Afrika Kusini. Wote watatu ni wakazi wa Afrika Kusini na wanaelekea kuwa ni maafisa na/au wafanyakazi wa Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini. Kufuatana na taarifa za BRELA, wanahisa wa awali wa Deep Green Finance walikuwa ni mawakili Protase R.G. Ishengoma na Stella Ndikimi wa kampuni ya mawakili ya IMMMA Advocates; Nedbank Ltd., Nedbank Africa Investments Ltd. na SBM Nedcor Holdings Ltd. Tarehe 15 Aprili 2005 mawakili Ishengoma na Ndikimi walihamisha hisa zao kwa Nedbank Ltd. na Nedbank Africa Investments Ltd. IMMMA Advocates vile vile ni mawakili wa Tangold Ltd. ambayo imehusishwa na ufisadi tuliouelezea katika Orodha ya Mafisadi.

Taarifa za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba tarehe 1 Mei 2004, Deep Green Finance ilifungua Akaunti Na. 011103024840 katika tawi la Corporate la Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Dar es Salaam. Kitu cha kwanza cha kushangaza ni kwamba siku hiyo ilikuwa ni Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) na ilikuwa siku ya mapumziko. Kitu cha pili cha kushangaza ni kwamba kampuni hii iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti hiyo bila ya kuingiza wala kutoa fedha yoyote kwa zaidi ya mwaka mmoja kuanzia tarehe 1 Mei 2004 hadi tarehe 31 Julai 2005. Kitu cha tatu cha kushangaza ni kwamba pamoja jina la Deep Green ‘Finance’ kuashiria kwamba kampuni hii ni taasisi ya kifedha, orodha ya taasisi za kifedha iliyotolewa na BOT tarehe 21 Agosti 2007 haionyeshi kwamba kampuni hii imewahi kusajiliwa na BOT kama taasisi ya kifedha!

Hata hivyo, kwa kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 na Desemba 1, 2005 kampuni hii ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815. 39 kutoka Wizara ya Fedha na/au BOT. Fedha hizo zilitolewa kwa utaratibu ufuatao:

(a) Tarehe 1 Agosti 2005 BOT, kwa kutumia hundi Na. 241740, ilihamisha dola za Marekani 1,354,167.26 au shilingi za Tanzania 1,546,778,770. 92 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku hiyo hiyo fedha hizo zote zilichukuliwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwa utaratibu maalum wa haraka (special clearance) na kupelekwa mahali kusikojulikana na kwa madhumuni yasiyofahamika;

(b) Tarehe 1 Septemba 2005 BOT, kwa kutumia hundi Na. 015558, ilihamisha dola za Marekani 1,827,137.44 au shilingi za Tanzania 2,083,255,881. 60 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku hiyo hiyo jumla ya shilingi 2,083,333,333. 33 zilichukuliwa kwa mara nyingine tena kwa kutumia utaratibu huo huo maalum wa haraka na kupelekwa kusikojulikana;

(c) Tarehe 8 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha dola za Marekani 100,256.62 au shilingi za Tanzania 114,611,746. 80 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Itakumbukwa kwamba Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni iliyoandikishwa nchini Mauritius tarehe 5 Aprili 2005 na kupewa Cheti cha Kutimiza masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006. Hata hivyo, mawaziri kadhaa wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wameendelea kudai kuwa kampuni hiyo inamilikiwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Tanzania . Wakurugenzi wa Tangold Ltd. ni Gavana Daudi Balali, Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge, Katibu Mkuu (Fedha) Gray Mgonja, Katibu Mkuu (Maji) Patrick Rutabanzibwa na Katibu Mkuu (Ofisi ya Waziri Mkuu) Vincent Mrisho. Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa BOT ya tarehe 21 Desemba 2006, Tangold Ltd. ililipwa na BOT dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kupitia akaunti isiyojulikana ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini na kwa madhumuni yasiyojulikana;

(d) Tarehe 16 Septemba 2005 jumla ya shilingi 129,000,000. 00 zilitolewa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance na kuwekwa kwenye akaunti ya muda maalum (FDR);

(e) Tarehe 3 Oktoba 2005 jumla ya shilingi 2,083,333,333. 33 za Wizara ya Fedha zililipwa kwa utaratibu maalum wa haraka kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Inaelekea fedha hizo zililipwa kabla BOT haijaingiza fedha yoyote kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwa vile tarehe 4 Oktoba 2005 BOT ilihamisha dola za Marekani 1,789,075.89 au shilingi 2,083,891,765. 35 kwenda kwenye akaunti hiyo;

(f) Tarehe 8 Oktoba 2005 jumla ya shilingi 39,761,397.98 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda Tangold Ltd.;

(g) Tarehe 31 Oktoba 2005 jumla ya shilingi za Tanzania 2,083,333,333. 33 fedha za Wizara ya Fedha zilihamishiwa kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(h) Tarehe 2 Novemba 2005 dola za Marekani 1,821,095.57 au shilingi za Tanzania 2,083,653,279. 68 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(i) Tarehe 30 Novemba 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 2,083,333,333. 33 zikiwa fedha za Wizara ya Fedha kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku moja baadaye, dola za Marekani 1,817,199.52 au shilingi za Tanzania 2,184,610,383. 04 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(j) Tarehe 10 Desemba 2005 shilingi 100,940,489. 71 zilihamishwa kutoka Tangold Ltd. kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Hii ilikuwa ni siku nne tu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 14, 2005 kufanyika nchini kote;

(k) Tarehe 19 Desemba 2005, siku tano baada ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, dola za Marekani 88,722.17 au shilingi za Tanzania 104,755,554. 09 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(l) Tarehe 9 Februari 2006 shilingi 3,836,800.00 zilihamishwa kwenda akaunti ya mawakili wa Deep Green Finance, IMMMA Advocates, iliyoko benki ya Standard Chartered. Haijulikani kama fedha hizi zilikuwa ni kwa ajili ya malipo ya mawakili hao au la;

(m) Malipo ya mwisho kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance yalifanywa tarehe 22 Novemba 2006 ambapo jumla ya shilingi 14,465,000.00 zilihamishiwa katika akaunti isiyojulikana ya benki ya Standard Chartered na kwa matumizi yasiyojulikana;

Kutokana na rekodi za kibenki zilizoonyeshwa hapo juu, jumla ya shilingi 10,484,005.39 ziliingizwa katika akaunti ya Deep Green Finance katika kipindi cha miezi minne tu kati ya tarehe 1 Agosti na 10 Desemba 2005. Hiki kilikuwa ni kipindi cha mchakato na/au kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 14 Desemba 2005. Aidha, kuanzia tarehe 11 Desemba 2005 hakuna fedha yoyote iliyoingizwa katika akaunti hiyo hadi tarehe 27 Februari 2007 kampuni hiyo ilipovunjwa ‘kwa hiari’ ya wanahisa wake. Ni muhimu kurudia kwamba, kwa ushahidi huu wa nyaraka za kibenki, kampuni ya Deep Green Finance haikuwa na hata senti moja kabla ya tarehe 1 Agosti 2005 na wala haikupokea hata thumni mara baada ya tarehe 10 Desemba 2005 na mara baada ya Uchaguzi Mkuu.

Kwa taarifa za sasa hivi, inafahamika kwamba faili la Deep Green Finance lililotakiwa kuwa BRELA limetoweka. Tuna kila sababu ya kuamini kwamba hii ilikuwa ni kampuni hewa (shell company) iliyoundwa kwa ajili tu ya kupitishia fedha za umma kutoka Benki Kuu kwenda kusikojulikana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2005. Ndio maana kampuni hiyo haikuwa na fedha zozote benki kutokea tarehe 1 Mei 2004 hadi tarehe 1 Agosti 2005, wiki tatu kabla ya kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu. Na ndio maana mabilioni iliyolipwa na Benki Kuu yalilipwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na mara baada ya Uchaguzi Mkuu kupita malipo hayo ya fedha za umma yalikoma.

2. TANGOLD LIMITED

Kama Orodha ya Mafisadi inavyoonyesha, Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni inayomilikiwa na baadhi ya Mafisadi tuliowataja katika Orodha hiyo. Kuna utata mkubwa zaidi ambao umeigubika kampuni ya Tangold Ltd. Kwanza, licha ya nyaraka kuonyesha kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006, nyaraka za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba Tangold Ltd. ilifungua akaunti ya shilingi Na. 011103024852 NBC Corporate Branch tarehe 1 Januari 2003. Kama ilivyokuwa kwa Deep Green Finance, siku ya Tangold Ltd. kufungua akaunti yake NBC ilikuwa ni Siku ya Mwaka Mpya na siku ya mapumziko kote nchini! Aidha taratibu za kibenki za ufunguaji wa akaunti za makampuni zinalazimu kampuni husika kuwasilisha benki nakala ya usajili wa kampuni, Katiba yake, leseni ya biashara na hati ya mlipa kodi ya TRA (TIN Registration Certificate) kabla ya kuruhusiwa kufungua akaunti. Swali la kujibiwa na NBC pamoja na Serikali ni je, ilikuwaje Tangold Ltd. iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti ya benki kabla hata haijaandikishwa nchini Mauritius achilia mbali kupata hati ya kutimiza masharti ya Tanzania ?

Pili, kampuni ya Tangold Ltd. iliendesha akaunti hiyo bila kuweka au kutoa fedha yoyote ile kati ya tarehe 1 Januari 2003 hadi tarehe 1 Agosti 2005 ilipoanza kunyeshewa mvua ya neema ya mabilioni ya fedha za walipa kodi wa Tanzania kutoka BOT! Mvua hiyo ni nje ya mvua ya dola za Marekani 13,340,168.37 zilizohojiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali na iliinyeshea Tangold Ltd. kama ifuatavyo:

(a) Tarehe 1 Agosti 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 4,703,221,229. 08 kwenda kwenye akaunti ya Tangold Ltd. Tarehe hii ni muhimu sana kwani ndiyo siku ambayo BOT ilifanya pia malipo ya kwanza kwa Deep Green Finance kama ilivyoelezewa katika Taarifa hii;

(b) Tarehe 2 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 244,428,386. 15 kutoka akaunti yake hiyo kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Kama tuliyoelezea katika Taarifa hii, tarehe 1 Septemba 2005 Deep Green Finance ililipwa pia shilingi 2,083,255,881. 60 na BOT;
(c) Tarehe 8 Oktoba 2005 shilingi za Tanzania 39,761,397.98 zilihamishiwa kwenye akaunti ya Tangold Ltd. kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(d) Tarehe 12 Oktoba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 1,690,500,000. 00 kwenda Meremeta Limited;

(e) Tarehe 23 Novemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 555,300,048. 00 kwenda Meremeta Ltd.;

(f) Tarehe 10 Desemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 100,940,489. 71 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(g) Tarehe 12 Desemba 2005, siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu, Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 551,060,000. 00 kwenda kwenye akaunti ya Meremeta Ltd.

Baada ya hapo Tangold Ltd. haikupokea wala kuingiza fedha zozote kwenye akaunti yake hadi tarehe 6 Juni 2006 ilipohamisha shilingi za Tanzania 220,980,370. 00 kwenda ‘TISS.’ TISS ni kifupi cha Tanzania Intelligence and Security Service ambalo ni jina la Kiingereza la Idara ya Usalama wa Taifa! Tangu tarehe hiyo hadi leo hii Tangold Ltd. haijaweka wala kutoa fedha nyingine yoyote katika akaunti hiyo. Kwa maana hiyo, katika kipindi cha miezi minne Tangold Ltd. iliingiziwa na BOT jumla ya shilingi za Tanzania 4,742,982,627. 06 na ilifanya malipo kwa Deep Green Finance na Meremeta Ltd. ya jumla ya shilingi za Tanzania 3,363,531,259. 67.

Maswali muhimu ya kujiuliza kuhusiana na Tangold Ltd. ni haya yafuatayo. Kwanza , ilikuwaje kampuni ambayo haikuwa hata imeandikishwa kisheria ikalipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi na/au ya umma na bila maelezo yoyote? Pili, ilikuwaje Serikali, kwa kupitia Waziri Karamagi, itoe taarifa ya uongo Bungeni kwamba Tangold Ltd. ni kampuni mpya na imeanzishwa ili kurithi mali na madeni ya Meremeta Ltd. wakati makampuni yote mawili yalikuwa yakipeana mabilioni ya fedha za umma wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu katika mazingira ya kutatanisha? Tatu, kwa nini malipo ya mabilioni haya yalikoma mara baada ya Uchaguzi Mkuu? Nne, kama Tangold Ltd. ni kampuni inayomilikiwa na Serikali je ofisi zake ziko wapi? Watendaji wake wakuu ni kina nani? Fedha za kigeni dola za Marekani 13,340,168.37 zilizolipwa na BOT tarehe 29 Desemba 2005 zilikuwa ni kwa ajili gani na kwa nini zimeendelea kuwa katika akaunti ya Tangold Ltd. hadi wakati huu?

Hivi karibuni baadhi ya wanachama wa CCM wameanza kuhoji matumizi makubwa ya fedha wakati wa mchakato wa kumpata mgombea Urais wa CCM wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita. Kama mnavyokumbuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku ametoa hadharani barua aliyomwandikia Mwenyekiti wa CCM aliyepita Bwana Benjamin Mkapa akidai kuwepo kwa ushahidi kuwa “fedha nyingi zinatumiwa katika uchaguzi huu.” Na kama alivyohoji Mzee Butiku katika barua yake kwamba “fedha hizo zinatoka wapi na ni za nani”, nasi tunawaomba wananchi wa Tanzania waidai Serikali iwaeleze mabilioni haya ya fedha za umma yalilipwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2005 kwa ajili gani.

Ili kupata majibu sahihi ya maswali yote haya, Serikali haina budi kuridhia kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi wa tuhuma zote hizi na zile zilizotolewa katika Orodha ya Mafisadi. Ni tume huru pekee itakayoweza kuchunguza ufisadi huu bila woga, upendeleo au hila. Na ni ripoti ya tume huru pekee ndiyo itakayotumika kuwawajibisha wale wote watakaobainika kushiriki kulisababishia taifa letu hasara kubwa namna hii.

Tunatambua kwamba Serikali imeteua wakaguzi wa mahesabu kutoka kampuni ya Ernst Young LLP ili kufanya uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma katika akaunti ya malipo ya nje inayoendeshwa na BOT (EPA) kwa niaba ya Serikali. Tunaomba kuweka wazi msimamo wetu kuhusiana na uchunguzi huo kuwa hauhusu ubadhirifu, wizi na/au ufisadi ndani ya BOT tuliouelezea katika Orodha ya Mafisadi na katika Taarifa hii. Vile vile uchunguzi huo hauhusu ufisadi unaohusu kusainiwa kwa mikataba mibovu na ambayo imeliingizia na italiingizia taifa letu hasara ya mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa maana hiyo, tunatoa taarifa mapema kwamba ripoti ya wakaguzi wa Ernst Young LLP haiwezi na isije ikachukuliwa kuwa ndio majibu ya Serikali kwa tuhuma za ufisadi, wizi na/au ubadhirifu wa fedha za umma zilizotolewa katika Orodha ya Mafisadi na katika Taarifa hii. Tunapenda kusisitiza kwamba tuhuma hizi zinaweza kujibiwa tu na tume huru ya uchunguzi.

Kutokana na uzito wa masuala tuliyoyaeleza katika Taarifa hii, tunapenda kuwataarifu wananchi wa Tanzania kwamba iwapo Serikali itashindwa na/au kukataa kuridhia kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi wa tuhuma hizi hadi kufikia 25 Novemba mwaka huu, vyama vyetu vitatoa maelekezo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla juu ya hatua za kuchukuliwa nao ili kuondokana na ufisadi, wizi na/au ubadhirifu wa mali ya wananchi tuliouelezea katika Taarifa hii na katika Orodha ya Mafisadi.

Asanteni sana
------------ --------- --------- --------- --------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI, CHADEMA------------ --------- --------- --------- ------
AUGUSTINO L. MREMA
MWENYEKITI, TLP

------------ --------- --------- --------- -----
PROF. IBRAHIM H. LIPUMBA

MWENYEKITI, CUF


------------ --------- --------- --------- --
JAMES F. MBATIA
MWENYEKITI, NCCR-MAGEUZI
 
good job freeman, good job Lyatonga, good job professor lipumba, good job Mbatia.

I salute you with vigour of love for my people,

Keep on applying pressure on them, your salt of justice to our motherland will always burn the wounds of traitors.

It is a matter of time, not a long time, the whole truth to unfold before our eyes.
Aluta continua.
 
Mimi nadhani mnataka kupandikiza mbegu za maneno ktk hotuba hii kiasi kwamba tayari mmekwisha fahamu motive ya ufisadi ule. Kwa nini watu wameisha rukia kuwa fedha hizo zinahusiana na Uchaguzi wa JK wakati kilichosemwa ni kwamba mambo haya yametendeka kabla ya Uchaguzi.
Yawezekana kabisa kuwa utawala uliokuwepo wakati huo waliyafanya haya ili hata kama watashindwa wawe wamesha toka na kitu...hakuna wakati mbaya wa kuibiwa nchi kama wakati wa uchaguzi na hawa jamaa wamechagua wakati huo makusudi kabla/kutangulia mabadiliko makubwa ya mawaziri, na manaibu wake.
Kifupi fedha hizo zote zilizoibiwa zinatokana na makapmpuni ambayo kuingia kwake nchini kibiashara kumewahusu watu wengine kabisa pamoja na kwamba wote wanatoka CCM.
Nadhani ni bora tufanye subra kidogo kutoa hukumu hii wakati mambo yote haya yametendeka wakati Mkapa akiwa Rais, mwanasiasa hai.
 
Mimi nadhani mnataka kupandikiza mbegu za maneno ktk hotuba hii kiasi kwamba tayari mmekwisha fahamu motive ya ufisadi ule. Kwa nini watu wameisha rukia kuwa fedha hizo zinahusiana na Uchaguzi wa JK wakati kilichosemwa ni kwamba mambo haya yametendeka kabla ya Uchaguzi.
Yawezekana kabisa kuwa utawala uliokuwepo wakati huo waliyafanya haya ili hata kama watashindwa wawe wamesha toka na kitu...hakuna wakati mbaya wa kuibiwa nchi kama wakati wa uchaguzi na hawa jamaa wamechagua wakati huo makusudi kabla/kutangulia mabadiliko makubwa ya mawaziri, na manaibu wake.
Kifupi fedha hizo zote zilizoibiwa zinatokana na makapmpuni ambayo kuingia kwake nchini kibiashara kumewahusu watu wengine kabisa pamoja na kwamba wote wanatoka CCM.
Nadhani ni bora tufanye subra kidogo kutoa hukumu hii wakati mambo yote haya yametendeka wakati Mkapa akiwa Rais, mwanasiasa hai.

Miongoni mwa waliosaidia kuvujisha hii info ni wanaccm ambao wamechukizwa na connection ya wanamtandao na hii skendo. Wao wanaamini kuwa hizi pesa zilitumika pia kwenye kampeni ya kumweka kikwete ikulu (pesa nyingi sana zilitumika) so wakati ni vyema kuvuta subira kusubiri matokeo ya uchunguzi ambao unaweza usifanyike maishani mwetu) ni vyema pia kukumbuka kuwa wanassm wenyewe waliosaidia kuvujisha haya wanaamini kuwa pesa zilitumika katika uchaguzi!

Asante kichwamaji kwa heading nzuri ya hii thread!
 
Mimi nadhani mnataka kupandikiza mbegu za maneno ktk hotuba hii kiasi kwamba tayari mmekwisha fahamu motive ya ufisadi ule. Kwa nini watu wameisha rukia kuwa fedha hizo zinahusiana na Uchaguzi wa JK wakati kilichosemwa ni kwamba mambo haya yametendeka kabla ya Uchaguzi.
Yawezekana kabisa kuwa utawala uliokuwepo wakati huo waliyafanya haya ili hata kama watashindwa wawe wamesha toka na kitu...hakuna wakati mbaya wa kuibiwa nchi kama wakati wa uchaguzi na hawa jamaa wamechagua wakati huo makusudi kabla/kutangulia mabadiliko makubwa ya mawaziri, na manaibu wake.
Kifupi fedha hizo zote zilizoibiwa zinatokana na makapmpuni ambayo kuingia kwake nchini kibiashara kumewahusu watu wengine kabisa pamoja na kwamba wote wanatoka CCM.
Nadhani ni bora tufanye subra kidogo kutoa hukumu hii wakati mambo yote haya yametendeka wakati Mkapa akiwa Rais, mwanasiasa hai.

Mukandara,
Hivi unaweza kuwazuia watu kufikiri na kuyapa mambo tafsiri wanayoiona karibu yao? Katika hili hapa, mbona mambo haya yalishajulikana? Vilivyohitajika na vielelezo na dondoo chache kama hizi. Siyo kwamba watyu wanahukumu, bali wanasea kila ambacho ni dhahiri. Unataka wamsubiri nani? Ili iweje?
 
Kichwamaji,
Sijakuzuia kabisa kutoa mawazo yako lakini ni kosa kubwa kuweka kichwa cha habari ambazo hazina media back up bali ni mtazamo wako. Ungeweza kabisa kutoa hoja yako ktk mada ile ile ya kwanza bila kupotosha maana kwetu sisi wasomaji.
Nilipoingia hapa nilidhani kuna habari mpya inayothibitisha maneno hayo lakini unapoanzisha motive basi inaweza kutafrisika kuwa ndiyo sababu kubwa iliyowasukuma viongozi hawa wa Upinzani kuiweka report hiyo Mpya.
hapa utakuwa umewapa silaha viongozi ama washabiki kuachana na hoja husika na kujenga hoja mpya kuuliza ushahidi wa aina yeyote ile kama kweli fedha hizo zimetumika ktk Uchaguzi wa JK. Kwa hiyo hapa tunaondokana na kupotea kwa fedha hizo pamoja na kampuni husika ambazo ndio hasa makusudio ya Ufisadi huu mpya.
Pili, ningekuomba wewe na mwafrika wa Kike mfahamu kwamba kiasi cha fedha zilizoibiwa ni nyingi sana kiasi kwamba huu ni uhujumu UCHUMI wa nchi yetu sio kabisa fedha zinazoweza kuchukuliwa/kuibwa kwa sababu ya Uchaguzi mkuu tu. CCM wanaweza chukua fedha wakati wowote bila kuzunguka na hakuna wa kuwauliza hata kama receipt sio za kweli.. hawana haja ya kuhusisha kampuni za nje.
Kumbukeni kwamba wengi wa wahusika ktk zengwe hili walikuwa sii wana mtandao kwani Bi. Meghji baada tu ya kuingia madarakani aligundua hitlafu hizi. Bibie (Mwafrika wa kike) sisi vijana wa mjini tulisha yasikia haya siku nyingi na ndio maana unaona watu kama kina Yona wanacheka pembeni kwani aliyejamba hamtaki kumwonyesha kidole!...
Sintapenda kabisa kujihusisha na ushabiki wa CCM - Mtandao ama Asilia kutafuta ukweli wa uhujumu huu kwani kati yao hakuna aliyekuwa na huruma na maslahi ya nchi yetu. Waliozitoa habari hizi ni watu wenye uchungu na yote yaliyokwisha tendeka toka Utawala wa Mkapa hadi huu wa JK kwani Simba wala nyama ni wale wale pamoja na kuwepo tofauti za kizazi chao...
Kinachotusumbua wengi ni kwa nini utawala huu unawakumbatia wahalifu wote ikiwa ni pamoja na Mkapa ktk zengwe la Ikulu, Meghji na Balali ktk BoT...
 
Admin, kwanini mada hii isiwekwe katika ile ya Urafiki Social Hall iliyotangulia? Maana hii doc ndiko ilikotokea. Hivi tunavurugana
 
Admin,
Kama kutakuwa na repition ya threads kutakuwa na hatari ya kuharibu attention ya threads nyingine zinazokuja, will be much better kama mtu hakusoma thread na akaweka sawa na iliyowekwa, ikaunganishwa na zilizopo
 
ubadhilifu huo wahusiana vipi na ushindi wa kishindo wa JK?? ni kweli kuna hujuma nyingi dhidi ya uchumi wa Inji hii umefanyika kipindi cha awamu iliyopita. ni vizuri tukazungumzia kwa uyakinifu kuliko kupeleka pasipohusika "misplacing attention of the matter".

Hivi huyo JK ni kipi cha ajabu sana alichofanya????? kwamba Balali kaiba BOT mlitaka keshoye akamatwe aswekwe ndani??
Bulyamhulu wanaiba dhahabu, usiku uleule afunge mgodi???
RA mwizi, palepale avunje urafiki, amfukuze ccm,wanainji igunga wamnyang'anye ubunge. Kaiba wapi,lini! hamna jibu, ooh tajiri, muirani, kanunua flana na kofia ccm! achaa! acheni utoto!!

Hivi tukiwa na rais kama huyo, akaamka asubuhi akasema funga JF tutampongeza??? mbona ndio staili ya rais tumtakaye???

Rais si kila kitu ktk innji, kuna taasisi na mifumo ya utendaji kiutawala.

ooh! samahani nimetoka nje ya mada, KWELI WATU WAMEIBA ILA NI KUJIDANGANYA KUSEMA ETI ZIMECHANGIA USHINDI WA KISHINDO WA JK, mnyonge mnyongeni hakiye mpeni!! JK alipendwa na wapiga kura wengi, kama atavurunda, ni swala jingine,

WAKATABAHU
 
Kwasababu wewe ni mkombozi wa mafisadi (joke):)

mie ndie nimekuja kukomboa watanzania waliochoshwa na ufisadi..miezi mitatu Balali anatibiwa huku marekani?ugonjwa gani usiotibika kwa miezi mitatu..nani ana details zake kwa siku analipa sh. ngapi
kw aghrama za hospitali za kitanzania ambazo balali anweza kulazwa as VIP
200,000*30*3=18,000,000 sasa kwa nje itakuwaje?weka na gharama za mtu ambaye amekwenda naye huko kama mwangalizi
mie nadhani mpaka sasa atakuwa ameshatumia kama 180 millions
 
Sina uwezo wa ku-hakiki taarifa hiziTAARIFA KWA WANANCHI WA TANZANIA
KUHUSU
JINSI CHAMA CHA MAPINDUZI KILIVYOCHOTA FEDHA
TOKA BENKI KUU YA TANZANIA
KUFADHILI KAMPENI ZAKE ZA UCHAGUZI 2005


Ndugu wananchi,
Tarehe 15 Septemba 2007 tulitoa Orodha ya Mafisadi yenye kuonyesha ufisadi, wizi na/au ubadhirifu
wa mabilioni ya fedha za umma unaowahusisha viongozi na watendaji wa juu katika Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na watu wengine walio kwenye uongozi wa umma. Hadi sasa Serikali haijatoa
majibu ya kuridhisha kuhusiana na tuhuma hizi nzito licha ya madai ya kufanya hivyo kutoka kwa
wananchi, taasisi zisizo za kiserikali, viongozi mbali mbali ndani na nje ya Serikali na Chama cha
Mapinduzi (CCM) na hata wawakilishi wa nchi wafadhili walioko Tanzania .
Leo tunaomba kuwajulisha wananchi wa Tanzania kupitia Mkutano huu Maalum na Wananchi wa Dar
es Salaam juu ya taarifa zinazoonyesha kuwepo kwa ufisadi na/au wizi wa mabilioni mengine ya fedha
za umma uliofanyika wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2005. Nyaraka mbali mbali
ambazo tumezipata hivi karibuni zinaonyesha kwamba makampuni hewa (shell companies)
kadhaa yalianzishwa katika vipindi tofauti kabla ya Uchaguzi Mkuu kwa lengo mahsusi la
kupitishia fedha zilizoibiwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Nyaraka hizi vile vile zinaonyesha
jinsi ambavyo fedha hizo ziliibiwa na kwa wakati gani kama ifuatavyo:
1. DEEP GREEN FINANCE COMPANY LIMITED
Mnamo tarehe 18 Machi 2004 ilianzishwa kampuni iitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. kwa
madhumuni ya, pamoja na mengine, kufanya biashara kama ‘mabepari’ na wakopeshaji fedha!
Kufuatana na taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakurugenzi wa Deep
Green Finance walikuwa ni mabwana Mark Ross Weston wa New Zealand ; Anton Taljaard wa Afrika
Kusini; na Rudolph van Schalkwyk pia wa Afrika Kusini. Wote watatu ni wakazi wa Afrika Kusini na
wanaelekea kuwa ni maafisa na/au wafanyakazi wa Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini. Kufuatana na
taarifa za BRELA, wanahisa wa awali wa Deep Green Finance walikuwa ni mawakili Protase R.G.
Ishengoma na Stella Ndikimi wa kampuni ya mawakili ya IMMMA Advocates; Nedbank Ltd.,
Nedbank Africa Investments Ltd. na SBM Nedcor Holdings Ltd. Tarehe 15 Aprili 2005 mawakili
Ishengoma na Ndikimi walihamisha hisa zao kwa Nedbank Ltd. na Nedbank Africa Investments Ltd.
IMMMA Advocates vile vile ni mawakili wa Tangold Ltd. ambayo imehusishwa na ufisadi tuliouelezea
katika Orodha ya Mafisadi.
Taarifa za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba tarehe 1 Mei 2004, Deep Green Finance ilifungua
Akaunti Na. 011103024840 katika tawi la Corporate la Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Dar es
Salaam. Kitu cha kwanza cha kushangaza ni kwamba siku hiyo ilikuwa ni Sikukuu ya Wafanyakazi
(Mei Mosi) na ilikuwa siku ya mapumziko. Kitu cha pili cha kushangaza ni kwamba kampuni hii
iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti hiyo bila ya kuingiza wala kutoa fedha yoyote kwa zaidi ya
mwaka mmoja kuanzia tarehe 1 Mei 2004 hadi tarehe 31 Julai 2005. Kitu cha tatu cha kushangaza ni
kwamba pamoja jina la Deep Green ‘Finance’ kuashiria kwamba kampuni hii ni taasisi ya kifedha,
orodha ya taasisi za kifedha iliyotolewa na BOT tarehe 21 Agosti 2007 haionyeshi kwamba kampuni
hii imewahi kusajiliwa na BOT kama taasisi ya kifedha!
Hata hivyo, kwa kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 na Desemba 1, 2005 kampuni hii
ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815. 39 kutoka Wizara ya Fedha na/au BOT. Fedha hizo
zilitolewa kwa utaratibu ufuatao:
(a) Tarehe 1 Agosti 2005 BOT, kwa kutumia hundi Na. 241740, ilihamisha dola za Marekani
1,354,167.26 au shilingi za Tanzania 1,546,778,770. 92 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green
Finance. Siku hiyo hiyo fedha hizo zote zilichukuliwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance
kwa utaratibu maalum wa haraka (special clearance) na kupelekwa mahali kusikojulikana na kwa
madhumuni yasiyofahamika;
(b) Tarehe 1 Septemba 2005 BOT, kwa kutumia hundi Na. 015558, ilihamisha dola za Marekani
1,827,137.44 au shilingi za Tanzania 2,083,255,881. 60 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green
Finance. Siku hiyo hiyo jumla ya shilingi 2,083,333,333. 33 zilichukuliwa kwa mara nyingine tena kwa
kutumia utaratibu huo huo maalum wa haraka na kupelekwa kusikojulikana;
(c) Tarehe 8 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha dola za Marekani 100,256.62 au shilingi za
Tanzania 114,611,746. 80 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Itakumbukwa kwamba
Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni iliyoandikishwa nchini Mauritius tarehe 5 Aprili 2005 na kupewa
Cheti cha Kutimiza masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006. Hata hivyo, mawaziri kadhaa wa
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wameendelea kudai kuwa kampuni hiyo inamilikiwa kwa asilimia mia
moja na Serikali ya Tanzania . Wakurugenzi wa Tangold Ltd. ni Gavana Daudi Balali, Waziri wa
Miundombinu Andrew Chenge, Katibu Mkuu (Fedha) Gray Mgonja, Katibu Mkuu (Maji) Patrick
Rutabanzibwa na Katibu Mkuu (Ofisi ya Waziri Mkuu) Vincent Mrisho. Kufuatana na barua ya
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa BOT ya tarehe 21 Desemba 2006, Tangold Ltd.
ililipwa na BOT dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kupitia akaunti isiyojulikana ya Nedbank Ltd. ya
Afrika Kusini na kwa madhumuni yasiyojulikana;
(d) Tarehe 16 Septemba 2005 jumla ya shilingi 129,000,000. 00 zilitolewa kutoka kwenye akaunti ya
Deep Green Finance na kuwekwa kwenye akaunti ya muda maalum (FDR);
(e) Tarehe 3 Oktoba 2005 jumla ya shilingi 2,083,333,333. 33 za Wizara ya Fedha zililipwa kwa
utaratibu maalum wa haraka kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Inaelekea fedha hizo
zililipwa kabla BOT haijaingiza fedha yoyote kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwa vile tarehe 4
Oktoba 2005 BOT ilihamisha dola za Marekani 1,789,075.89 au shilingi 2,083,891,765. 35 kwenda
kwenye akaunti hiyo;
(f) Tarehe 8 Oktoba 2005 jumla ya shilingi 39,761,397.98 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya
Deep Green Finance kwenda Tangold Ltd.;
(g) Tarehe 31 Oktoba 2005 jumla ya shilingi za Tanzania 2,083,333,333. 33 fedha za Wizara ya Fedha
zilihamishiwa kwenye akaunti ya Deep Green Finance;
(h) Tarehe 2 Novemba 2005 dola za Marekani 1,821,095.57 au shilingi za Tanzania 2,083,653,279. 68
zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;
(i) Tarehe 30 Novemba 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 2,083,333,333. 33 zikiwa fedha za
Wizara ya Fedha kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku moja baadaye, dola za
Marekani 1,817,199.52 au shilingi za Tanzania 2,184,610,383. 04 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti
ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;
(j) Tarehe 10 Desemba 2005 shilingi 100,940,489. 71 zilihamishwa kutoka Tangold Ltd. kwenda
kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Hii ilikuwa ni siku nne tu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa
Desemba 14, 2005 kufanyika nchini kote;
(k) Tarehe 19 Desemba 2005, siku tano baada ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, dola za Marekani
88,722.17 au shilingi za Tanzania 104,755,554. 09 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green
Finance kwenda kusikojulikana;
(l) Tarehe 9 Februari 2006 shilingi 3,836,800.00 zilihamishwa kwenda akaunti ya mawakili wa Deep
Green Finance, IMMMA Advocates, iliyoko benki ya Standard Chartered. Haijulikani kama fedha hizi
zilikuwa ni kwa ajili ya malipo ya mawakili hao au la;
(m) Malipo ya mwisho kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance yalifanywa tarehe 22 Novemba
2006 ambapo jumla ya shilingi 14,465,000.00 zilihamishiwa katika akaunti isiyojulikana ya benki ya
Standard Chartered na kwa matumizi yasiyojulikana;
Kutokana na rekodi za kibenki zilizoonyeshwa hapo juu, jumla ya shilingi 10,484,005.39 ziliingizwa
katika akaunti ya Deep Green Finance katika kipindi cha miezi minne tu kati ya tarehe 1 Agosti na 10
Desemba 2005. Hiki kilikuwa ni kipindi cha mchakato na/au kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika
tarehe 14 Desemba 2005. Aidha, kuanzia tarehe 11 Desemba 2005 hakuna fedha yoyote iliyoingizwa
katika akaunti hiyo hadi tarehe 27 Februari 2007 kampuni hiyo ilipovunjwa ‘kwa hiari’ ya wanahisa
wake. Ni muhimu kurudia kwamba, kwa ushahidi huu wa nyaraka za kibenki, kampuni ya Deep Green
Finance haikuwa na hata senti moja kabla ya tarehe 1 Agosti 2005 na wala haikupokea hata thumni
mara baada ya tarehe 10 Desemba 2005 na mara baada ya Uchaguzi Mkuu.
Kwa taarifa za sasa hivi, inafahamika kwamba faili la Deep Green Finance lililotakiwa kuwa BRELA
limetoweka. Tuna kila sababu ya kuamini kwamba hii ilikuwa ni kampuni hewa (shell company)
iliyoundwa kwa ajili tu ya kupitishia fedha za umma kutoka Benki Kuu kwenda kusikojulikana wakati
wa Uchaguzi Mkuu wa 2005. Ndio maana kampuni hiyo haikuwa na fedha zozote benki kutokea tarehe
1 Mei 2004 hadi tarehe 1 Agosti 2005, wiki tatu kabla ya kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu. Na
ndio maana mabilioni iliyolipwa na Benki Kuu yalilipwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na
mara baada ya Uchaguzi Mkuu kupita malipo hayo ya fedha za umma yalikoma.
2. TANGOLD LIMITED
Kama Orodha ya Mafisadi inavyoonyesha, Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni inayomilikiwa na baadhi
ya Mafisadi tuliowataja katika Orodha hiyo. Kuna utata mkubwa zaidi ambao umeigubika kampuni ya
Tangold Ltd. Kwanza, licha ya nyaraka kuonyesha kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza
masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006, nyaraka za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba
Tangold Ltd. ilifungua akaunti ya shilingi Na. 011103024852 NBC Corporate Branch tarehe 1 Januari
2003. Kama ilivyokuwa kwa Deep Green Finance, siku ya Tangold Ltd. kufungua akaunti yake NBC
ilikuwa ni Siku ya Mwaka Mpya na siku ya mapumziko kote nchini! Aidha taratibu za kibenki za
ufunguaji wa akaunti za makampuni zinalazimu kampuni husika kuwasilisha benki nakala ya usajili wa
kampuni, Katiba yake, leseni ya biashara na hati ya mlipa kodi ya TRA (TIN Registration Certificate)
kabla ya kuruhusiwa kufungua akaunti. Swali la kujibiwa na NBC pamoja na Serikali ni je, ilikuwaje
Tangold Ltd. iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti ya benki kabla hata haijaandikishwa nchini
Mauritius achilia mbali kupata hati ya kutimiza masharti ya Tanzania ?
Pili, kampuni ya Tangold Ltd. iliendesha akaunti hiyo bila kuweka au kutoa fedha yoyote ile kati ya
tarehe 1 Januari 2003 hadi tarehe 1 Agosti 2005 ilipoanza kunyeshewa mvua ya neema ya mabilioni ya
fedha za walipa kodi wa Tanzania kutoka BOT! Mvua hiyo ni nje ya mvua ya dola za Marekani
13,340,168.37 zilizohojiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali na iliinyeshea
Tangold Ltd. kama ifuatavyo:
(a) Tarehe 1 Agosti 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 4,703,221,229. 08 kwenda kwenye
akaunti ya Tangold Ltd. Tarehe hii ni muhimu sana kwani ndiyo siku ambayo BOT ilifanya pia malipo
ya kwanza kwa Deep Green Finance kama ilivyoelezewa katika Taarifa hii;
(b) Tarehe 2 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 244,428,386. 15 kutoka
akaunti yake hiyo kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Kama tuliyoelezea katika Taarifa
hii, tarehe 1 Septemba 2005 Deep Green Finance ililipwa pia shilingi 2,083,255,881. 60 na BOT;
(c) Tarehe 8 Oktoba 2005 shilingi za Tanzania 39,761,397.98 zilihamishiwa kwenye akaunti ya
Tangold Ltd. kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance;
(d) Tarehe 12 Oktoba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 1,690,500,000. 00 kwenda
Meremeta Limited;
(e) Tarehe 23 Novemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 555,300,048. 00 kwenda
Meremeta Ltd.;
(f) Tarehe 10 Desemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 100,940,489. 71 kwenda
kwenye akaunti ya Deep Green Finance;
(g) Tarehe 12 Desemba 2005, siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu, Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za
Tanzania 551,060,000. 00 kwenda kwenye akaunti ya Meremeta Ltd.
Baada ya hapo Tangold Ltd. haikupokea wala kuingiza fedha zozote kwenye akaunti yake hadi tarehe 6
Juni 2006 ilipohamisha shilingi za Tanzania 220,980,370. 00 kwenda ‘TISS.’ TISS ni kifupi cha
Tanzania Intelligence and Security Service ambalo ni jina la Kiingereza la Idara ya Usalama wa Taifa!
Tangu tarehe hiyo hadi leo hii Tangold Ltd. haijaweka wala kutoa fedha nyingine yoyote katika akaunti
hiyo. Kwa maana hiyo, katika kipindi cha miezi minne Tangold Ltd. iliingiziwa na BOT jumla ya
shilingi za Tanzania 4,742,982,627. 06 na ilifanya malipo kwa Deep Green Finance na Meremeta Ltd.
ya jumla ya shilingi za Tanzania 3,363,531,259. 67.
Maswali muhimu ya kujiuliza kuhusiana na Tangold Ltd. ni haya yafuatayo. Kwanza , ilikuwaje
kampuni ambayo haikuwa hata imeandikishwa kisheria ikalipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi
na/au ya umma na bila maelezo yoyote? Pili, ilikuwaje Serikali, kwa kupitia Waziri Karamagi, itoe
taarifa ya uongo Bungeni kwamba Tangold Ltd. ni kampuni mpya na imeanzishwa ili kurithi mali na
madeni ya Meremeta Ltd. wakati makampuni yote mawili yalikuwa yakipeana mabilioni ya fedha za
umma wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu katika mazingira ya kutatanisha? Tatu, kwa nini malipo
ya mabilioni haya yalikoma mara baada ya Uchaguzi Mkuu? Nne, kama Tangold Ltd. ni kampuni
inayomilikiwa na Serikali je ofisi zake ziko wapi? Watendaji wake wakuu ni kina nani? Fedha za
kigeni dola za Marekani 13,340,168.37 zilizolipwa na BOT tarehe 29 Desemba 2005 zilikuwa ni kwa
ajili gani na kwa nini zimeendelea kuwa katika akaunti ya Tangold Ltd. hadi wakati huu?
Hivi karibuni baadhi ya wanachama wa CCM wameanza kuhoji matumizi makubwa ya fedha wakati
wa mchakato wa kumpata mgombea Urais wa CCM wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita. Kama
mnavyokumbuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku ametoa
hadharani barua aliyomwandikia Mwenyekiti wa CCM aliyepita Bwana Benjamin Mkapa akidai
kuwepo kwa ushahidi kuwa “fedha nyingi zinatumiwa katika uchaguzi huu.” Na kama alivyohoji Mzee
Butiku katika barua yake kwamba “fedha hizo zinatoka wapi na ni za nani”, nasi tunawaomba
wananchi wa Tanzania waidai Serikali iwaeleze mabilioni haya ya fedha za umma yalilipwa wakati wa
Uchaguzi Mkuu wa 2005 kwa ajili gani.
Ili kupata majibu sahihi ya maswali yote haya, Serikali haina budi kuridhia kuundwa kwa tume huru ya
uchunguzi wa tuhuma zote hizi na zile zilizotolewa katika Orodha ya Mafisadi. Ni tume huru pekee
itakayoweza kuchunguza ufisadi huu bila woga, upendeleo au hila. Na ni ripoti ya tume huru pekee
ndiyo itakayotumika kuwawajibisha wale wote watakaobainika kushiriki kulisababishia taifa letu
hasara kubwa namna hii.
Tunatambua kwamba Serikali imeteua wakaguzi wa mahesabu kutoka kampuni ya Ernst Young LLP ili
kufanya uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma katika akaunti ya malipo
ya nje inayoendeshwa na BOT (EPA) kwa niaba ya Serikali. Tunaomba kuweka wazi msimamo wetu
kuhusiana na uchunguzi huo kuwa hauhusu ubadhirifu, wizi na/au ufisadi ndani ya BOT tuliouelezea
katika Orodha ya Mafisadi na katika Taarifa hii. Vile vile uchunguzi huo hauhusu ufisadi unaohusu
kusainiwa kwa mikataba mibovu na ambayo imeliingizia na italiingizia taifa letu hasara ya mabilioni
ya fedha za kigeni. Kwa maana hiyo, tunatoa taarifa mapema kwamba ripoti ya wakaguzi wa Ernst
Young LLP haiwezi na isije ikachukuliwa kuwa ndio majibu ya Serikali kwa tuhuma za ufisadi, wizi
na/au ubadhirifu wa fedha za umma zilizotolewa katika Orodha ya Mafisadi na katika Taarifa hii.
Tunapenda kusisitiza kwamba tuhuma hizi zinaweza kujibiwa tu na tume huru ya uchunguzi.
Kutokana na uzito wa masuala tuliyoyaeleza katika Taarifa hii, tunapenda kuwataarifu wananchi wa
Tanzania kwamba iwapo Serikali itashindwa na/au kukataa kuridhia kuundwa kwa tume huru ya
uchunguzi wa tuhuma hizi hadi kufikia 25 Novemba mwaka huu, vyama vyetu vitatoa maelekezo kwa
wanachama wetu na wananchi kwa ujumla juu ya hatua za kuchukuliwa nao ili kuondokana na ufisadi,
wizi na/au ubadhirifu wa mali ya wananchi tuliouelezea katika Taarifa hii na katika Orodha ya
Mafisadi.
Asanteni sana
(IMETIWA SAHIHI NA)
------------ --------- --------- --------- --------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI, CHADEMA
------------ --------- --------- --------- ------
AUGUSTINO L. MREMA
MWENYEKITI, TLP
------------ --------- --------- --------- -----
PROF. IBRAHIM H. LIPUMBA
MWENYEKITI, CUF
------------ --------- --------- --------- --
JAMES F. MBATIA
MWENYEKITI, NCCR-MAGEUZI
 
ungesoma ambacho wenzako wameshapost inawezekena usingekuwa mtu wa tatu kurudia. TUnashukuru kwa taarifa, ila ilishabandikwa.
 
Please jamani muwe munasoma kwanza mada kama hizo zinazofanana i.e. BOT kuona kwamba je unachotaka kupost kipo au hakipo...........anyway........ni ustaarbu tu............wala hulazimishwi................ndio demokrasia ya JF
 
WaBongo sasa wanaweza kukodiwa kuandika habari feki,zote nimezisoma kuhusu hii mada na zinaonekana ni copy and paste from origino,sasa kule kwenye sahihi ndio kindende maana wameogopa kuziiga ,ikiwa kutazuka patashika watajwa wanaweza kuzikana kwamba hazitokani na ridhaa yao tofauti na ile ya mkataba sahihi zilikuwepo.Kama haya mambo ni kweli basi toeni ronyo za hundi zilizotumika,sio minamba na kuwazuga wananchi ,unajua upinzani utafanya kazi kweli kweli kuwasilimisha watu ili kukiasi chama cha mapinduzi kwani dau hili wanalotaka kuvukia linaonekana hakuna kitakachokuwa zaidi ya proper ganda ,wakati ndizi zimekwisha kuliwa halafu unawakuwa watu wa vijijini huko wao ndio waumini halisi wa CCM ,ibada yao ni ile ile ya CCM ndio baba na CCM ndio Mama huna lugha ya kuwasimulia wakakufuata.
Na huu muungano wa Upinzani ni unafiki mtupu ,unaokwenda na wakati hawa hawa si ndio waliwawekea pingamizi wabunge sijui wawakilishi wa CUF kule Pemba .sasa hapa si kuna uzinguaji tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom