BoT mnisikilize ili kwendana na wakati dunia inataka nini

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,720
Kitu kilichonileta na kushtuka kama mnakumbuka miaka ya nyuma china ilihodhi sana dola ya Kimarekani nchini mwao ambapo malipo mengi walikuwa wanataka dola na kufikia mzunguko wa dola ukawa upo China.

Hapo ndipo Marekani akashtuka kuwa pesa yake yote ipo China!.baada kutangaza hatachapisha pesa mpya au series mpya ndio China ikatangaza kumuuzia.

Backup ya dola ni kutokana na mafuta na kibiashara ndio imeweza kufanya dunia nzima inaweza kutumika.

Ila watu wengi na wanaofahamu kuwa nchi yoyote ili kuendelea lazima kuwe na Kenki Kuu.

Ili nchi kuweza kuendesha uchumi lazima kuwa na pesa za kigeni na kwa ajili ya matumizi mengine kama ndani na nje tutakapohitaji kutoka nchi nyingine.

Sehemu kubwa anayetushikilia hiyo backup ni BoT ndio pesa zote za kigeni zipo hapo.

Jambo ambalo mpaka naeleza hili nimeona China wanachotaka kukifanya kuja na mfumo wao unaitwa Yuan wallet.

Yuan wallet ni mfumo wa kidigitali ambao utapokea pesa kwa njia yoyote ya kidigitali ambao data base ya pesa utakayolipa kama mgeni basi Benki Kuu ya kwao itachukua data pesa ya kwenu na Benki Kuu ya China itakuwa inajua data pesa za kigeni ni ngapi bila kukuathiri wewe hata kama unatoka Afghanistani utalipa pesa ya kwenu.

Tuje sasa kwenye mfumo huu kuhusu hapa kwetu Tanzania.

BoT inaweza kupata pesa za kigeni nyingi bila kupata shida na ikaweza kuzipa mabenki na hata thamani ya pesa yetu ikawa thamani.

BoT inatakiwa sasa kujiingiza kwenye mfumo unaitwa data pesa.

Data pesa ni mfumo ambao sio wa cash kwa dunia ya sasa bali ni mfumo ambao mtu anaweza kutumia benki yake alipotoka,visa,m-pesa kenya na n.k wakati hata kapo kuwa analipa basi hii data pesa itakuwa inapeleka backup kwenye BoT kuwa imepokea mfano kenya shilingi data pesa.

Hapa BoT hata kuwa anafahamu kuwa kwenye account yake ana data pesa ya pesa fulani nchini mwake.

Maana yani kila atakaye kuja hapa nchini hataruhusiwa kulipa kwa pesa yake ndani ya nchii kwa njia electronic money si cash money ya pesa yake na kama ana cash basi italazima kufika duka la data pesa kupokea.

Hizi pesa zitakazoingia kwa data pesa ndio zitalinganishwa na thamani ya pesa yetu na hata tumia hapa hapa pesa yetu.

Mfumo huu utalazimika Benki Kuu kutengeza App itakayoitwa BoT wallet

BOT wallet ni mfumo utakaounganisha watanzania na Benki Kuu ili transaction za pesa za kigeni kupokea Benki Kuu na benki kuu kukupa pesa ya ndani.

BoT itaweza kumiliki pesa nyingi za nchi za watu na itakapotaka kununua maitaji hizo nchi basi pesa tutakuwa tunayo kwa sababu itakuwa ikatazi kulipa kwa pesa yako uliyotoka nayo huko.
 
Aliyeelewa atuletee kasamari kidogo, Mkuu kamaanisha nn?

Maana kuozi dora n.k maneno ya kiuchumi haya bila kupewa somo jingine la pembeni ngumu Sana kuelewa!
 
Japo sijamuelewa sn mtoa mada, lakin sisi serikali zetu zina struggle sn na mambo ya creativity!
 
Tatizo waliopo kwenye mamlaka kukubali ushauri unaotoka nje ya mamlaka wanaona kama ni kunywa sumu. Watu wamelalamika kuhusu Paypal hadi sasa watu wameamua kunyamaza tu. Yaani BoT hawataki watu wapokee pesa kwa paypal hapa Tanzania sijui hofu yao nini. :(
 
Back
Top Bottom