BoT: Mikoa ya Kagera na Kigoma ndiyo inayoogoza kwa kuwa na noti chafu na chakavu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,249
110,829
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa imegundulika rasmi kuwa Mikoa inayoongoza kwa Kuchafua Pesa za Noti hasa zile za Tsh 10,000/= nchini Tanzania ni Mikoa ya Kigoma kwa Waha na Kagera kwa Wahaya hivyo wameombwa kuanzia sasa Kujitahidi kuwa Wastaarabu hasa katika suala zima la Usafi.

Hata hivyo kuna Uchunguzi mwingine wa Kisirisiri ( ambao siyo rasmi ) ulifanywa na Kugundua ya kwamba ni Mkoa mmoja tu nchini Tanzania ambao ndiyo unaongoza kwa Kujua Kutunza Pesa katika hali ya Usafi kama ambavyo ilitoka Benki Kuu nao ni Mkoa wa Mara ( Musoma )

Kama umeshika Pesa ya Noti hapo ulipo na ni Chafu walaumu Waha ( Kigoma ) na Wahaya ( Kagera )

Chanzo cha Taarifa hii: Gazeti na Mtandao wa MWANANCHI

Nawasilisha.
===

Habari kamili:
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeitaja mikoa ya Kigoma na Kagera kuwa ndiyo inayoongoza kwa kuwa na noti chakavu na kuwataka wenye fedha hizo au zilizoharibika kuzibadilisha kwenye matawi ya benki za biashara.

Meneja msaidizi wa uhusiano kwa umma wa BoT, Victoria Msina alisema jana mjini hapa kuwa wakazi wa mikoa hiyo wanaongoza kwa uchafuzi wa noti wakifuatiwa na wa Mkoa wa Kagera.

“Utafiti tuliofanya tumebaini mikoa ya Kigoma na Kagera inaongoza kwa kuchafua noti. Fedha zinachakaa mno ukilinganisha na mikoa mingine, ndiyo maana tumeamua kutoa elimu kuanzia na mikoa hii miwili,” alisema Msina wakati wakizungumza na wananchi mjini hapa.

BoT inatoa elimu ya umuhimu wa kutunza fedha ili kuepuka uchakavu sambamba na utambuzi wa alama ili kutofautisha noti halali na bandia kwa urahisi.

Diwani wa Kigoma Mjini, Hussein Kalyango alisema noti nyingi zinazotumika mkoani humo ni vigumu kuzitumia katika mikoa mingine.

“Kuna noti tunazitumia hapa Kigoma lakini ukifika nazo Dar es Salaam utaambiwa ni mbovu na hawazipokei. Kwa hiyo ni lazima BoT mtoe elimu kwa jamii ili wajue umuhimu wa kutunza noti zisichakae mapema,” alisema Kalyango.

Meneja msaidizi wa utunzaji fedha na alama za usalama wa BoT, Abdul Dollah aliwaambia wakazi wa mji huo kuwa benki za biashara zimepewa jukumu la kubadilisha fedha chakavu.

Alisema benki hizo zimepewa jukumu la kupokea fedha chakavu kutoka kwa wananchi, kisha kuzipeleka BoT kwa ajili ya hatua ya uteketezaji.

“Benki zote sasa zinapokea fedha mbovu na chakavu na (mwananchi) utabadilishiwa kwa kupewa fedha nzima bila kukatwa, lengo ni kupunguza usumbufu unaojitokeza,” alisema Dollah.

Aliwataka wananchi kuacha tabia ya kuuza noti mbovu au chakavu kwa watu wanaozinunua kwa gharama ndogo kwa kuwa hata wao huzipeleka kwenye benki za biashara kuzibadilisha kwa thamani halisi.

Mfanyabiashara wa Soko la Kigoma, Mathias John alisema mpango wa kubadilisha noti chakavu utasaidia kupunguza fedha mbovu zilizopo kwenye mzunguko.

Watumishi wa BoT wapo mkoani humo kwa ziara ya siku tano kuelimisha jamii juu ya utunzaji bora wa noti na wanatarajia kutembelea wilaya za Uvinza na Kasulu. Wananchi wa Kigoma Mjini wanaweza kubadilisha fedha chakavu katika benki za CRDB, NMB, NBC, TPB na Exim zilizopo mkoani humo.
 
Mkoa wa mara wabahili kutumia hela hao kigoma na kagera hela inazunguka sana haitunzwi masandukuni kama wanavyofanya Mara.Mara hela ikitua mkononi mwa mtu ndio imefika mwisho wa safari hapo hasa ikiwa noti ya elfu kumi.Mtu kuitumia anaona ubahili.Anabaki kuhifadhi vizuri badala ya kuirudisha kwenye mzunguko.Kigoma na kagera wazee wa matumizi
 
BOT wameshindwa kulinda shilingi dhidi ya Dora wanahangaika na uchakavu wa noti.

Ivi hamjui mikoa tajwa nimikoa yenye mizinguko kiduchu ya fedha?

Sababu ya noti kuchakaa ni mzunguko mdogo wa pesa unakuta noti inapita kwenye mikono ya watumiaji 50kabla ya kwenda benki lakini mikoa mingine pesa inatoka benki inapitia watumiaji wawili afu inarudi benk itachakaa saa ngapi?

Unawezaje kumwambia muuza mkaa apeleke ela Bank wakati zinarudi kununua mkaa na maporini walipo wachoma mkaa hakuna bank?

Mimi naona uwezo wa kufukiri wataalamu wetu umefika mwisho wameanza kutembelea uzoefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye siredi hii ukiingia kichwa kichwa mapovu yatakutoka, ila mimi kama mtu wa Kagera nasema hivi sisi hela tumezoea kuweka benki sio kama watu wa Musoma wanaofukia kwenye udongo/shimo

Sent using Jamii Forums mobile app

Watani zangu acheni Uchafu. Watu wa Mkoa wa Mara ni Wasafi mno na pengine ndiyo maana tuna ' Akili ' kubwa na nyingi kuliko Watu wa Mikoa ya Kigoma na Kagera. Wewe Hela imetoka Benki Kuu ikiwa safi kabisa halafu ikienda Kigoma na Kagera unakuta Muha au Mhaya anatoka Msalani / Maliwatoni hata hajanawa anashika Hela hizo kwanini zisichakae / zisifubae? Halafu angalau sasa leo nimejua ni kwanini Pesa nyingi za Noti huwa zinanukia ' Nnya Nnya ' sana kumbe ' Source ' yake ni Kigoma na Kagera.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa imegundulika rasmi kuwa Mikoa inayoongoza kwa Kuchafua Pesa za Noti hasa zile za Tsh 10,000/= nchini Tanzania ni Mikoa ya Kigoma kwa Waha na Kagera kwa Wahaya hivyo wameombwa kuanzia sasa Kujitahidi kuwa Wastaarabu hasa katika suala zima la Usafi.

Hata hivyo kuna Uchunguzi mwingine wa Kisirisiri ( ambao siyo rasmi ) ulifanywa na Kugundua ya kwamba ni Mkoa mmoja tu nchini Tanzania ambao ndiyo unaongoza kwa Kujua Kutunza Pesa katika hali ya Usafi kama ambavyo ilitoka Benki Kuu nao ni Mkoa wa Mara ( Musoma )

Kama umeshika Pesa ya Noti hapo ulipo na ni Chafu walaumu Waha ( Kigoma ) na Wahaya ( Kagera )

Chanzo cha Taarifa hii: Gazeti na Mtandao wa MWANANCHI

Nawasilisha.
Mimi ,kwa Mikoa 24 niliyotembelea ...mJI WA mUSOAM UANAONGOZA KWA KUWA NA NOTI CHAFU NA ZILIZOCHAKAA!
 
--
IMG-20190308-WA0010.jpeg

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kwenye siredi hii ukiingia kichwa kichwa mapovu yatakutoka, ila mimi kama mtu wa Kagera nasema hivi sisi hela tumezoea kuweka benki sio kama watu wa Musoma wanaofukia kwenye udongo/shimo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ha ha umesau kitu mtu wa kagera benki anazoweka hela zake ni zile international Banks ambazo wafanyakazi wake ni wasomi Wana masters degree na mabosi wao Wana PhD na wanaongea kiingereza kizuri.Hizo ndizo benki mtani wangu mhaya huweka pesa zake sio hizi local banks.Na watani zangu hao wameshatoa ushauri kuwa ili.pesa yetu iwe na thamani kubwa maneno kwenye pesa yote yaandikwe kiingereza kuandika kiswahili kunaifanya thamani yake ishuke dhidi ya dola.
 
Mimi ,kwa Mikoa 24 niliyotembelea ...mJI WA mUSOAM UANAONGOZA KWA KUWA NA NOTI CHAFU NA ZILIZOCHAKAA!

Nakupa ONYO KALI kama Wewe siyo Mhaya ( Kagera ) au Muha ( Kigoma ) au Mnyiramba na Mnyaturu ( Singida ) au Mrangi ( Kondoa Dodoma ) au Mkara ( Ukerewe Mwanza ) nakupa dakika tano ( 5 ) tu zijazo kwa niaba ya wana Mkoa wa Mara ( Musoma ) wote utengue Kauli yako hii ( namaanisha Utuombe radhi / msamaha ) vinginevyo utajuta na utajua ni kwanini Mikoa yote nchini Tanzania kuna ' Mashoga / Mapunga / Watambaliziwaji ' ila ni Mkoa mmoja tu wa Mara ( Musoma ) ndipo hakuna. Nilikupa dakika 5 sasa zimebaki 3 tu.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa imegundulika rasmi kuwa Mikoa inayoongoza kwa Kuchafua Pesa za Noti hasa zile za Tsh 10,000/= nchini Tanzania ni Mikoa ya Kigoma kwa Waha na Kagera kwa Wahaya hivyo wameombwa kuanzia sasa Kujitahidi kuwa Wastaarabu hasa katika suala zima la Usafi.

Hata hivyo kuna Uchunguzi mwingine wa Kisirisiri ( ambao siyo rasmi ) ulifanywa na Kugundua ya kwamba ni Mkoa mmoja tu nchini Tanzania ambao ndiyo unaongoza kwa Kujua Kutunza Pesa katika hali ya Usafi kama ambavyo ilitoka Benki Kuu nao ni Mkoa wa Mara ( Musoma )

Kama umeshika Pesa ya Noti hapo ulipo na ni Chafu walaumu Waha ( Kigoma ) na Wahaya ( Kagera )

Chanzo cha Taarifa hii: Gazeti na Mtandao wa MWANANCHI

Nawasilisha.
Kabla ya kulaumu nenda kaishi Kigoma kwa muda wa mwezi mmoja kisha rudi utokako. Udongo wa Kigoma ni mwekundu na vumbi lake ni jekundu hivyo kila kitu huko hushika ranging ya vumbi ambavyo ni nyekundu wakiwemo watu pia. Noti ya shilingi 2,000/= toka Kigoma inafanana rangi na ile ya 10,000/= nguo nyeupe hazifai huko, hivyo kuwalaumu Waha ni unyanyasaji wa kibaguzi kwani hata makabila mengine wakiwemo Wamakonde wapo.
 
Back
Top Bottom