BoT: Mabilioni zaidi yalichotwa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Mabilioni zaidi yalichotwa BoT

Mwandishi Wetu Machi 19, 2008

Gavana ashituka upotevu wa Sh 155bn/-

Watendaji wahaha ‘kufunika kombe'
Raia Mwema

BAADA ya kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Serikali sasa zinatishiwa na kashfa nyingine kubwa zaidi ya upotevu wa zaidi ya Sh. bilioni 155 zilizotumika katika mazingira ya kutatanisha kupitia mgodi wa dhahabu wa Buhemba mkoani Mara.

Habari zilizopatikana ndani ya Serikali zinaeleza kwamba kashfa hiyo ni zaidi ya ile ya EPA kutokana na kuwa uwezekano wa kurejesha fedha hizo ni mdogo kutokana na kuingia katika mkondo unaoihusisha zaidi Serikali yenyewe na watendaji wake wakiwahusisha wafanyabiashara wa kimataifa.

Taarifa ambazo Raia Mwema imepata zinasema kuwa kwa kushitushwa na ulaji huo mkubwa wa fedha, Kamati ya Rais inayochunguza sekta ya Madini, chini ya uongozi wa Jaji Mark Bomani, ililazimika kwenda Buhemba na kuwaita watendaji kadhaa wa Serikali akiwamo Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, ambaye ameelezwa kushitushwa na taarifa hizo.

Kamati ndogo ya Kamati hiyo ya Jaji Bomani, iliyokwenda Buhemba iliongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, ambaye hata hivyo alipoulizwa kuhusiana na sakata la Buhemba, alisema anayepaswa kuzungumzia suala hilo ni Mwenyekiti wa kamati nzima.

"Ni kweli tulikwenda Buhemba na baadaye tuliwaita watendaji kadhaa wa Serikali, lakini tumekubaliana mambo yote yanayohusu kamati yatolewe taarifa na Mwenyekiti wetu (Jaji Bomani) ambaye nina hakika atawapa taarifa mnayopaswa kupewa… Bahati mbaya siko naye karibu, mimi niko Dar es Salaam na yeye nimemwacha Bagamoyo," alisema Zitto.

Kauli kama hiyo pia ilitolewa jana na Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo inayomaliza kazi yake mwezi huu.

Kwa upande wake, Jaji Bomani aliliambia Raia Mwema katika mahojiano ya simu, jana, Jumanne, kwamba Kamati yake haitaficha kitu na kwamba baada ya kutembelea Buhemba na kuchunguza mambo yanayohusiana na mgodi huo, watatoa mapendekezo yao katika ripoti yao ya mwisho lakini alikataa kutoa ufafanuzi wowote kuhusiana na suala hilo kwa maelezo kwamba wako katika kikao.

Habari zinasema hata Gavana wa Benki Kuu, Profesa Ndulu ambaye aliitwa hivi karibuni na kamati hiyo alishitushwa na kashfa hizo na amenukuliwa akisema kwamba kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za fedha katika utaratibu mzima wa malipo ya fedha hizo ambazo ni zaidi ya zile za EPA zilizolipwa kwa utaratibu wa Dhamana za Hazina (Treasury Bonds).

Akizungumza na Raia Mwema, jana, kwa njia ya simu akiwa nchini Uingereza, Gavana Profesa Ndulu alikiri kuitwa katika kamati ya Rais inayopitia sekta ya madini, lakini hakueleza kwa kina alichojadiliana na wajumbe wa kamati kwa maelezo kwamba wao ndio wenye mamlaka ya kutoa taarifa hizo kwa kina.

"Mimi walitaka maoni yangu kuhusu mambo mengi ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu fedha za nje na mambo mengine kuhusiana na sekta ya madini, na masuala mengi tulizungumza kwa nia njema. Nadhani mungewauliza wenyewe watu wa kamati," alisema Profesa Ndulu.

Imefahamika kwamba baadhi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Meremeta ambao wanaelezwa kuwa katika nafasi hizo kutokana na nyadhifa zao bado wanaendelea kushikilia hisa hizo akiwamo Gavana wa zamani wa Benki Kuu, Dk. Daudi Ballali, ambaye ajira yake ilisitishwa na Rais Jakaya Kikwete lakini hisa zake hazijahamishwa kwa gavana wa sasa.

Tayari kuna habari kwamba kumekuwapo na juhudi za makusudi zinazofanywa na baadhi ya watendaji serikalini ambao wanajipanga kuzuia kuanikwa kwa ufisadi huo mkubwa.

Fedha hizo ambazo zilibadilishwa na kuwa Dola za Marekani 131,736,628.73 kwa maelekezo yaliyotolewa Desemba 20, 2005, siku moja kabla ya kuapishwa kwa Rais Jakaya Kikwete, zilifanyiwa uhamisho kwenda Afrika Kusini na kuingizwa Nedbank, na nyingine kuingizwa katika akaunti za kampuni ya Tangold na Meremeta.

Taarifa za wakaguzi zinaonyesha kwamba baada ya ununuzi huo wa dhamana, Benki Kuu ilizibadilisha sehemu ya dhamana hizo kuwa dola za Marekani 118,396,460.36 ambazo zilipelekwa kwenye akaunti moja isiyojulikana ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini, benki hiyo ikiwa imezipokea fedha hizo kupitia HSB Bank ya New York, Marekani zikitajwa kuwa malipo ya madeni ya kampuni mufilisi ya Meremeta Ltd.

Nyaraka ambazo Raia Mwema imeziona zinaonyesha kwamba sehemu nyingine ya fedha hizo zipatazo Dola za Marekani 13,736,628.73 zililipwa kwa kampuni ya TANGOLD kwenye akaunti ya kampuni hiyo iliyoko Benki ya NBC Corporate Branch, Dar es Salaam.

Mbali ya kamati ya madini na wakaguzi, kwa nyakati tofauti, kuhoji malipo hayo, bado usiri na juhudi kubwa za kufunika masuala hayo zimekuwa zikiendelea kufanywa.

Mwaka jana Mbunge wa Karatu Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA), aliliingiza suala hilo katika hoja yake iliyokuja kugonga mwamba.

Katika hoja yake hiyo, Dk. Slaa alibainisha kwamba Meremeta Ltd. ni kampuni binafsi ya kigeni iliyoandikishwa Agosti 19, 1997 katika kisiwa cha Isle of Man nchini Uingereza na kupewa namba ya usajili 3424504, ikimilikiwa na TRIENNEX (PTY) LTD ya Afrika Kusini yenye asilimia 50 ya hisa za kawaida na Msajili wa Hazina (Treasury Registrar) akiwa na asilimia 50.

Kwa upande wa Tanzania, Dk. Slaa alisema Meremeta ilipewa Hati ya kutimiza masharti (Certificate of Compliance) Oktoba, 1997 lakini akasema kwamba Meremeta ilifilisiwa Uingereza Januari 2006.

Hata hivyo, Dk. Slaa ameeleza kwamba pamoja na kampuni hiyo kufilisiwa nchini Uingereza, hakuna ushahidi kuwa kwa upande wa Tanzania kampuni hiyo imefilisiwa au la kutokana na kutajwa katika marejeo mbalimbali kuwa moja ya makampuni yanayozalisha dhahabu.

"Taarifa na takwimu muhimu kuhusu Sekta za Nishati na Madini', ya Julai, 2007, inaonyesha kuwa Meremeta bado inafanya kazi, na inazalisha tani 2.27 za dhahabu. Kama Serikali inasema Meremeta imefilisiwa na mali zake kuhamishiwa TANGOLD hali hii inaelezwa vipi? Taarifa hizi za utata zinaashiria nini?" alihoji Dk. Slaa.

Maelezo mengine yanayoibua utata zaidi na ambao Kamati ya Rais inayopitia mikataba ya madini itapata wakati mgumu kuitolea taarifa ni kuhusu Meremeta kudaiwa kuwa ni kampuni iliyoanzishwa kwa lengo la kusaidia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Nyumbu wakati ikiwa imeandikishwa nchi ya kigeni.

Taarifa ya awali ya wakaguzi waliokagua BoT, Juni 2006, ziliibua sakata hilo la Meremeta pamoja na kashfa nyingine lakini haikuweza kufahamika ripoti hiyo ya wakaguzi ilivyoyeyuka na kutoanikwa hadharani kabla ya wakaguzi wengine wa nje kuibua suala la EPA pekee miongoni mwa uchafu mwingi ndani ya BoT na serikalini.

Taarifa hiyo ya wakaguzi ilibainisha kwamba serikali ilitoa fedha hizo kiasi cha Sh. bilioni 155 kwa njia ya dhamana ya hazina ambayo inatakiwa kulipiwa riba ya asilimia 14.92 kila mwaka lakini hakukua na makubaliano yoyote rasmi kati ya Serikali na Meremeta hali inayoibua zaidi utata na kuonyesha hakuna njia yoyote ya kuweza kuzipata fedha hizo.

Habari zaidi zinaeleza kwamba ndani ya BoT bado kuna mianya mingi ambayo huenda ikaendelea kuibuka siku hadi siku hususan baada ya Bunge kuonyesha njia kwa kushughulikia sakata la umeme wa dharura uliokabidhiwa kwa kampuni ya Richmond Development LLC ya Marekani, sakata lililosababisha kuanguka kwa mawaziri watatu akiwamo aliyekua Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
 
Kuna haja ya Bunge kuunda kamati ya kufanya uchunguzi wa kina BoT inaonekana pale pesa haina mwenyewe kabisa.
 
Bunge letu ni Bunge uchwara wanajali zaidi maslahi yao binafsi na yale ya CCM kuliko ya nchi. Ukaguzi wa EPA uliofanywa na Ernst & Young kwa mwaka mmoja tu umegundua kwamba shilingi bilioni 133 zilikupuliwa na mafisadi, katika mwaka wa 2005 shilingi 155 bilioni nazo zilikupuliwa kupitia Meremeta na Tangold. Hii ni jumla ya shilingi bilioni 288 kwa mwaka mmoja tu! Fikiria kama ukaguzi ungekuwa toka mwaka 2000 mpaka 2006, basi si ajabu walichokupua ni mara tano au hata zaidi ya hii amount tuliyoijua hadi sasa. Bilioni 288 kwa mwaka mmoja zimekupuliwa! Duh!
 
Hili walilijua wana ccm kuwa Raia mwema inaenda kulitoa na wakaanza premptive strikes kuwachafua viongozi wa upinzani. Kama nilivyosema hapa kuwa halali mtu mpaka kieleweke!

Records zipo na magazeti yapo mengi sana na sidhani kama Lowasa na Rostam wana pesa za kutosha za kununua kila mtu, na kama wakifanikiwa, bado hawataweza kununua membaz wote wa JF! Tanzania kunahitajika kitu kifanyike haraka sana ila bado sitaki kusema ninachofikiria kwa sasas!
 
Is this not the reason of these folks to go to Butiama ? Yote haya ni kweli JK hakuyajua na huyu Gavana hakujua basi Mkapa ana kazi sana .Wacha tusikilizie maana hata comments sina .
 
Hili walilijua wana ccm kuwa Raia mwema inaenda kulitoa na wakaanza premptive strikes kuwachafua viongozi wa upinzani. Kama nilivyosema hapa kuwa halali mtu mpaka kieleweke!

Records zipo na magazeti yapo mengi sana na sidhani kama Lowasa na Rostam wana pesa za kutosha za kununua kila mtu, na kama wakifanikiwa, bado hawataweza kununua membaz wote wa JF! Tanzania kunahitajika kitu kifanyike haraka sana ila bado sitaki kusema ninachofikiria kwa sasas!

MwK, naungana na point yako katika hili kuwa ni vigumu kulificha. Hata hivyo EL na RA hawako sana katika mchezo huu na hawana sababu (at least for now) ya kulificha kwani ukubwa na uzito wake utasaidia kufunika la kwao 'dogo' la Richmond. Wao wana kila sababu ya kupenda hili suala lije mbele zaidi na zaidi, na siyo kufunika.

Watakaolia na BOT ni wengi kuliko waliolia na Richmond. Dagaa wanaweza hata kwenda jela kwa hilo la BOT.
 
pamoja na haya mapesa kuliwa kuna mtu alishawahi kusema kuwa anaenda kuhemea. Sijui kwa ajili ya tumbo lake?
 
MwK, naungana na point yako katika hili kuwa ni vigumu kulificha. Hata hivyo EL na RA hawako sana katika mchezo huu na hawana sababu (at least for now) ya kulificha kwani ukubwa na uzito wake utasaidia kufunika la kwao 'dogo' la Richmond. Wao wana kila sababu ya kupenda hili suala lije mbele zaidi na zaidi, na siyo kufunika.

Watakaolia na BOT ni wengi kuliko waliolia na Richmond. Dagaa wanaweza hata kwenda jela kwa hilo la BOT.

Asilimia kubwa ya deals za kifisadi ambazo zimefanyika tangu JK aingie madarakani mikono ya EL na RA imo ndani. Kwa hiyo kusema kwamba kwenye hili dili hawamo, hapo sikubaliani kabisa. Hakuna fisadi anaweza kufanya ufisadi mkubwa kiasi hicho bila kuwahusisha hao majamaa kutokana na ile imani kwamba walikuwa na influence kubwa serikalini na hivyo kuwashirikisha ni sawa na kujilinda ili bomu likilipuka wajue namna ya kulizima.

Kwa jinsi ninavyofahamu siasa za kupakana matope, kama hili dili wasingekuwemo basi lingeishaanikwa siku nyingi sana ili kufunika kashfa ya Richmond ambayo imewadondokea mikononi na hawakuwa na njia ya kuikwepa.
 
Kazi ipo! Hivi tunawezaje kuendelea wakati wajanja wanachota pesa hivyo bila hata aibu?

Hii ya kwetu ni sawa na baba kuiba uji wa mwanawe. Naona tumekuwa vichaa.
 
Taarifa hiyo ya wakaguzi ilibainisha kwamba serikali ilitoa fedha hizo kiasi cha Sh. bilioni 155 kwa njia ya dhamana ya hazina ambayo inatakiwa kulipiwa riba ya asilimia 14.92 kila mwaka lakini hakukua na makubaliano yoyote rasmi kati ya Serikali na Meremeta hali inayoibua zaidi utata na kuonyesha hakuna njia yoyote ya kuweza kuzipata fedha hizo.

1. Now this is very sad story, lakini ninamumainia Zitto, kuwemo kwake kwenye hii kamati ni home run, Mkulu Zitto, tunakusubiria hapa kwenye hili,

2. Rais wa zamani Mkapa, lazima kuna something anajua on this, maana kuna mahali inasema kuwa hela zilihamishwa siku rais mpya alipokuwa akiapishwa.

3. As usual Balali tena, kwa hiyo ushahidi utakosekana tutaambiwa kwa vile Balali hayupo!

4. Mama Meghji anajua nini kwenye hili? Mgonja? Mramba?

Anyways mkuu Zitto, tunakuaminia sana kwenye hili.
 
Hili walilijua wana ccm kuwa Raia mwema inaenda kulitoa na wakaanza premptive strikes kuwachafua viongozi wa upinzani. Kama nilivyosema hapa kuwa halali mtu mpaka kieleweke!

Records zipo na magazeti yapo mengi sana na sidhani kama Lowasa na Rostam wana pesa za kutosha za kununua kila mtu, na kama wakifanikiwa, bado hawataweza kununua membaz wote wa JF! Tanzania kunahitajika kitu kifanyike haraka sana ila bado sitaki kusema ninachofikiria kwa sasa!

Nimeipenda point yako kwamba" Tanzania kunahitajika kitu kifanyike haraka sana"

Mwaka 1999 Rais Mbeki wa SA aliunda kitu inayo julikna kama Scorpion.
South Africa's elite Scorpions crimefighters.

http://uk.reuters.com/article/latestCrisis/idUKL1223114320080212

Kikosi hiki kimefanya kazi yake kwa muda wa miaka 9 na kimeweza kuwabana viongozi wengi wala Rushwa ikiwa ni pamoja na mkuu wa Polisi wa SA.
Kikosi pia kimeweza kukusanya ushahidi wa Rushwa wa Mwenyekiti mpya wa ANC MH Xuma( ZUMA).

Lakini katika hali ya kusikitisha na kuzorotesha mapambano Chama cha ANC kimepitisha Azimio la kuilazimisha serikali Iue chombo hiki cha kupambana na Rushwa kubwa ili kunusuru Makalio ya Rais Mtarajiwa wa Afrika ya Kusini kubanwa Mahakamani na kupelekwa Jela kama wala Rushwa wengine.

ANC chama tunacho kizimia kwa Mapambano ya uonevu na ukandamizaji kimepitisha Azimio la kuruhusu wezi na Mharamia wa uchumi wa nchi ya SA kuendelea kutembea kifua mbele kama Mafisadi wa Bongo.

Hili ni pigo kubwa katika Mapambano ya Maendeleo na haki kwa Waafrika wote, zaidi ni aibu kubwa hasa kwetu Watanzania tulio waunga mkono SA kwa sababu Tulichopigania na kukidai kwa muda mrefu na hatimaye kukipata sasa kinapigwa vita.
Haki Inapigwa Vita

Ni lazima tuunde chombo cha kushughulikia Rushwa na Ubadhirifu wa Fedha wa Viongozi wote wakuu wa serikali ili kuinusuru Tanzania kuingia kwenye machafuko makubwa yanayoweza kuzaa Civil War

Kwetu sisi kazi hiyo asipewe Rais Kikwete.
Kazi ya kuunda kikosi cha kuwashughulikia mafisadi ibebwe na Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni lazima kiundwe chombo Kabambe kitakacho shughulikia Rushwa Kubwa za Viongozi wa juu wa serikali Ikiwezekana chombo hicho kijumuishe hata maofisa wastaafu wa Scotland Yard ya UK na wale wa Mosad ya Israel ili kuhakikisha kwamba Transaction Chafu za Vuiongozi wote wa SISIEMU na serikali yake zinapigwa Kipunga cha Katrina.

Hatuwezi kuwachunguza Viongozi wa serikali kwa kuunda Timu ya Viongozi waliomo serikalini ambao Vibarua vyao vinategemea neema ya Rais.
Viongozi wote wa kuteuliwa na rais hawatakiwi kuwemo katika chombo hiki ninacho kipendekeza.
Mkuu wa Polisi,Jeshi,Usalama wa taifa, Mwanasheria Mkuu na Mawaziri wote hawatakiwi hata kujua kinachoendelea ndani ya kikosi hicho.

Watu wanao hitajika katika kikosi cha kuchunguza Rushwa na Ubadhirifu wa fedha wa Viongozi wakuu wa Serikali ni lazima kitokane na
Majaji wastaafu wenye historia nyoofu.
Maafisa usalama wa taifa walio staafu.
Wanasheria wa kujitegemea.
Wasomi wa kitanzania wasio watumishi wa serikali walio ndani na nje ya nchi.
( Tunao Watanzania wengi wafanyao kazi katika Mashirika ya Upelelezi na Usalama hapa USA na UK)
Wastaafu kutoka kikosi cha upelelezi cha JWTZ.
Vijana wasomi wenye hamu ya kupambana na Ufisadi.
Wananchi wa kawaida wenye sifa na upeo katika Upelelzi.

Chombo hiki kinatakiwa kuwajibika moja kwa moja katika Bunge Tukufu la Jamhuri na kuripoti maendeleo ya shughuli zake za kila siku katika kamati maalumu ya Bunge ambayo ni lazima iwe na wabunge toka vyama vya upinzani pia.
Pia chombo hiki ni lazima kiwe na uwezo wa kipolisi wa kusimama Mahakamani na kutoa ushahidi wa upelelezi moja kwa moja kwa Majaji bila kuingiliwa na DPP aua mtu yeyote ndani ya serikali ya Tanzania.

Napendekeza Kikosi hiki kiitwe " NGE" as in Scorpion

Kikosi hiki kishugulikie Rushwa za Watumishi wa serikali wa vyeo vya juu kama makamishna makatibu wakuu wa wizara wakurugenzi wa wizara, mawaziri na viongozi wote wanaochaguliwa na Rais.

Nionavyo mimi kamwe hatuwezi kufanikiwa katika vita hii ya kupambana na Ufisadi kwa kuwashirikisha viongozi wanaotegemea neema ya Rais ili vibarua vyao visote nyasi.

Hawa akina Said Mwema Mwanyika Hosea na wengine wa aina yao hawawezi kamwe kuwabana watendaji wa serikali wala serikali hata ukitolewa ushahidi wa Video ukionyesha watumishi wa serikali wako chemba wakigawana maburungutu ya fedha kwenye viroba kama vile ni viazi mbambata au mihogo kutoka Lindi.

Upelelezi wa wizi wa fedha za BOT ni mchezo wa kitoto.

Ni kama Binadamu kuomba msaada wa Tumbiri kwenda wachunguza na kuwabana Kima kwa kitendo chao cha kuiba mahindi shambani kwako.
Uchunguzi utafanyika kisha uchunguzi huo utatumika kutengeneza mwafaka mpya kati ya Tumbiri na Kima na Pengine hata kutumika kuwakaribisha Sokwe kushiriki kwenye umoja huo mchafu.

Viongozi wa serikali ni lazima waundiwe mkakati mpya wa kuwabana siyo hii lelemama ya akina Mwanyika na Troop lake la Maharamia.
 
1. Now this is very sad story, lakini ninamumainia Zitto, kuwemo kwake kwenye hii kamati ni home run, Mkulu Zitto, tunakusubiria hapa kwenye hili,

2. Rais wa zamani Mkapa, lazima kuna something anajua on this, maana kuna mahali inasema kuwa hela zilihamishwa siku rais mpya alipokuwa akiapishwa.

3. As usual Balali tena, kwa hiyo ushahidi utakosekana tutaambiwa kwa vile Balali hayupo!

4. Mama Meghji anajua nini kwenye hili? Mgonja? Mramba?

Anyways mkuu Zitto, tunakuaminia sana kwenye hili.

Mkuu wote uliowataja wanahusika na kashfa moja au nyingine bado CCM imewakumbatia kama wanachama wake. Huko CCM hakuna utaratibu wa kuwafukuza wanachama waliohusika na ufisadi kwa namna moja au nyingine? Kama hakuna, basi nakuomba mkuu ulipigie debe hili CCM haiwezi kuendelea kuwakumbatia wanachama waliogubikwa na kashfa nzito nzito inabidi ianze kujisafisha haraka sana vinginevyo Watanzania hatutakose kuiita CCM Chama Cha Mafisadi. Bilioni 288 zimeyeyuka hivi hivi na wahusika wote bado wana kadi halali za CCM! Mwe! Wafanye nini mpaka CCM iwafukuze uanachama!? :confused:
 
Uchafu huo wote umeanzia Ikulu. Sasa utawezaje kuishi maisha bora kwa kusafisha sebureni unakolia halafu sehemu unayolala ukaacha hata kufua mashuka. Na wala kazi haiko kwao kujisafisha, kazi iko kwetu kuwasafisha. Watanzania inatakiwa kusimame imara, tuwaamshe waliolala ili kwamba uchaguzi unafuata ni kuwapiga chini tu. Wananchi wakisema NO ni NO.
Nafikiri kwa uchaguzi ujao tunatakiwa kuweka historia ya upigaji kura kwa wingi huki tukikikataa cha FISADI. Maelezo lazima yatolewe kuhusu hizo pesa zilizo kuwa transfered siku 1 kabla rais hajaapishwa. Zakia Meghji, Mramba, Mgonja, Balali, Chenge na hata Mkapa mnatakiwa mueleze wananchi hizi transaction. Na hata kama hamuhusiki moja kwa moja lakini mtakuwa na taarifa kuhusu hiyo mali ya WADANGANYIKA.
Nafikiri kama walivyosema wengine hapa, kuna pesa nyingi tu itakuwa imeliwa na ingekuwa jambo la maana kama wengeirudisha ile kampuni Ernst & Young kufanya uchunguzi mwingine. Jamani hizi ni pesa nyingi sana, watu wanajichotea tu huku watanzania wengine wanateseka huko vijijini. Mlishindwa kusaidia wanafunzi kule Ukraine, oh serikali haina pesa kumbe........mmmmhhh!!

Watanzania tuwabane hawa watu mpaka hizi hela zimerudi. Tukiwakomalia wabunge nao wataikomalia serikali na chama chao. Mkapa anatakiwa ajibu hizi tuhuma na si kukubali usemi wa JK eti tumwache Mzee wa watu apumzike. Apumzike na huku uhujuma uchumi umetokea, jamani jamani how can you back up ur 2015 Dira ya Uondoaji Umaskini kama mtaachiana fedha za wananchi??????????????? Yaani inanitia hasira
 
Back
Top Bottom