BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Mabilioni zaidi yalichotwa BoT
Mwandishi Wetu Machi 19, 2008
Gavana ashituka upotevu wa Sh 155bn/-
Watendaji wahaha ‘kufunika kombe'
Raia Mwema
BAADA ya kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Serikali sasa zinatishiwa na kashfa nyingine kubwa zaidi ya upotevu wa zaidi ya Sh. bilioni 155 zilizotumika katika mazingira ya kutatanisha kupitia mgodi wa dhahabu wa Buhemba mkoani Mara.
Habari zilizopatikana ndani ya Serikali zinaeleza kwamba kashfa hiyo ni zaidi ya ile ya EPA kutokana na kuwa uwezekano wa kurejesha fedha hizo ni mdogo kutokana na kuingia katika mkondo unaoihusisha zaidi Serikali yenyewe na watendaji wake wakiwahusisha wafanyabiashara wa kimataifa.
Taarifa ambazo Raia Mwema imepata zinasema kuwa kwa kushitushwa na ulaji huo mkubwa wa fedha, Kamati ya Rais inayochunguza sekta ya Madini, chini ya uongozi wa Jaji Mark Bomani, ililazimika kwenda Buhemba na kuwaita watendaji kadhaa wa Serikali akiwamo Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, ambaye ameelezwa kushitushwa na taarifa hizo.
Kamati ndogo ya Kamati hiyo ya Jaji Bomani, iliyokwenda Buhemba iliongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, ambaye hata hivyo alipoulizwa kuhusiana na sakata la Buhemba, alisema anayepaswa kuzungumzia suala hilo ni Mwenyekiti wa kamati nzima.
"Ni kweli tulikwenda Buhemba na baadaye tuliwaita watendaji kadhaa wa Serikali, lakini tumekubaliana mambo yote yanayohusu kamati yatolewe taarifa na Mwenyekiti wetu (Jaji Bomani) ambaye nina hakika atawapa taarifa mnayopaswa kupewa… Bahati mbaya siko naye karibu, mimi niko Dar es Salaam na yeye nimemwacha Bagamoyo," alisema Zitto.
Kauli kama hiyo pia ilitolewa jana na Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo inayomaliza kazi yake mwezi huu.
Kwa upande wake, Jaji Bomani aliliambia Raia Mwema katika mahojiano ya simu, jana, Jumanne, kwamba Kamati yake haitaficha kitu na kwamba baada ya kutembelea Buhemba na kuchunguza mambo yanayohusiana na mgodi huo, watatoa mapendekezo yao katika ripoti yao ya mwisho lakini alikataa kutoa ufafanuzi wowote kuhusiana na suala hilo kwa maelezo kwamba wako katika kikao.
Habari zinasema hata Gavana wa Benki Kuu, Profesa Ndulu ambaye aliitwa hivi karibuni na kamati hiyo alishitushwa na kashfa hizo na amenukuliwa akisema kwamba kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za fedha katika utaratibu mzima wa malipo ya fedha hizo ambazo ni zaidi ya zile za EPA zilizolipwa kwa utaratibu wa Dhamana za Hazina (Treasury Bonds).
Akizungumza na Raia Mwema, jana, kwa njia ya simu akiwa nchini Uingereza, Gavana Profesa Ndulu alikiri kuitwa katika kamati ya Rais inayopitia sekta ya madini, lakini hakueleza kwa kina alichojadiliana na wajumbe wa kamati kwa maelezo kwamba wao ndio wenye mamlaka ya kutoa taarifa hizo kwa kina.
"Mimi walitaka maoni yangu kuhusu mambo mengi ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu fedha za nje na mambo mengine kuhusiana na sekta ya madini, na masuala mengi tulizungumza kwa nia njema. Nadhani mungewauliza wenyewe watu wa kamati," alisema Profesa Ndulu.
Imefahamika kwamba baadhi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Meremeta ambao wanaelezwa kuwa katika nafasi hizo kutokana na nyadhifa zao bado wanaendelea kushikilia hisa hizo akiwamo Gavana wa zamani wa Benki Kuu, Dk. Daudi Ballali, ambaye ajira yake ilisitishwa na Rais Jakaya Kikwete lakini hisa zake hazijahamishwa kwa gavana wa sasa.
Tayari kuna habari kwamba kumekuwapo na juhudi za makusudi zinazofanywa na baadhi ya watendaji serikalini ambao wanajipanga kuzuia kuanikwa kwa ufisadi huo mkubwa.
Fedha hizo ambazo zilibadilishwa na kuwa Dola za Marekani 131,736,628.73 kwa maelekezo yaliyotolewa Desemba 20, 2005, siku moja kabla ya kuapishwa kwa Rais Jakaya Kikwete, zilifanyiwa uhamisho kwenda Afrika Kusini na kuingizwa Nedbank, na nyingine kuingizwa katika akaunti za kampuni ya Tangold na Meremeta.
Taarifa za wakaguzi zinaonyesha kwamba baada ya ununuzi huo wa dhamana, Benki Kuu ilizibadilisha sehemu ya dhamana hizo kuwa dola za Marekani 118,396,460.36 ambazo zilipelekwa kwenye akaunti moja isiyojulikana ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini, benki hiyo ikiwa imezipokea fedha hizo kupitia HSB Bank ya New York, Marekani zikitajwa kuwa malipo ya madeni ya kampuni mufilisi ya Meremeta Ltd.
Nyaraka ambazo Raia Mwema imeziona zinaonyesha kwamba sehemu nyingine ya fedha hizo zipatazo Dola za Marekani 13,736,628.73 zililipwa kwa kampuni ya TANGOLD kwenye akaunti ya kampuni hiyo iliyoko Benki ya NBC Corporate Branch, Dar es Salaam.
Mbali ya kamati ya madini na wakaguzi, kwa nyakati tofauti, kuhoji malipo hayo, bado usiri na juhudi kubwa za kufunika masuala hayo zimekuwa zikiendelea kufanywa.
Mwaka jana Mbunge wa Karatu Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA), aliliingiza suala hilo katika hoja yake iliyokuja kugonga mwamba.
Katika hoja yake hiyo, Dk. Slaa alibainisha kwamba Meremeta Ltd. ni kampuni binafsi ya kigeni iliyoandikishwa Agosti 19, 1997 katika kisiwa cha Isle of Man nchini Uingereza na kupewa namba ya usajili 3424504, ikimilikiwa na TRIENNEX (PTY) LTD ya Afrika Kusini yenye asilimia 50 ya hisa za kawaida na Msajili wa Hazina (Treasury Registrar) akiwa na asilimia 50.
Kwa upande wa Tanzania, Dk. Slaa alisema Meremeta ilipewa Hati ya kutimiza masharti (Certificate of Compliance) Oktoba, 1997 lakini akasema kwamba Meremeta ilifilisiwa Uingereza Januari 2006.
Hata hivyo, Dk. Slaa ameeleza kwamba pamoja na kampuni hiyo kufilisiwa nchini Uingereza, hakuna ushahidi kuwa kwa upande wa Tanzania kampuni hiyo imefilisiwa au la kutokana na kutajwa katika marejeo mbalimbali kuwa moja ya makampuni yanayozalisha dhahabu.
"Taarifa na takwimu muhimu kuhusu Sekta za Nishati na Madini', ya Julai, 2007, inaonyesha kuwa Meremeta bado inafanya kazi, na inazalisha tani 2.27 za dhahabu. Kama Serikali inasema Meremeta imefilisiwa na mali zake kuhamishiwa TANGOLD hali hii inaelezwa vipi? Taarifa hizi za utata zinaashiria nini?" alihoji Dk. Slaa.
Maelezo mengine yanayoibua utata zaidi na ambao Kamati ya Rais inayopitia mikataba ya madini itapata wakati mgumu kuitolea taarifa ni kuhusu Meremeta kudaiwa kuwa ni kampuni iliyoanzishwa kwa lengo la kusaidia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Nyumbu wakati ikiwa imeandikishwa nchi ya kigeni.
Taarifa ya awali ya wakaguzi waliokagua BoT, Juni 2006, ziliibua sakata hilo la Meremeta pamoja na kashfa nyingine lakini haikuweza kufahamika ripoti hiyo ya wakaguzi ilivyoyeyuka na kutoanikwa hadharani kabla ya wakaguzi wengine wa nje kuibua suala la EPA pekee miongoni mwa uchafu mwingi ndani ya BoT na serikalini.
Taarifa hiyo ya wakaguzi ilibainisha kwamba serikali ilitoa fedha hizo kiasi cha Sh. bilioni 155 kwa njia ya dhamana ya hazina ambayo inatakiwa kulipiwa riba ya asilimia 14.92 kila mwaka lakini hakukua na makubaliano yoyote rasmi kati ya Serikali na Meremeta hali inayoibua zaidi utata na kuonyesha hakuna njia yoyote ya kuweza kuzipata fedha hizo.
Habari zaidi zinaeleza kwamba ndani ya BoT bado kuna mianya mingi ambayo huenda ikaendelea kuibuka siku hadi siku hususan baada ya Bunge kuonyesha njia kwa kushughulikia sakata la umeme wa dharura uliokabidhiwa kwa kampuni ya Richmond Development LLC ya Marekani, sakata lililosababisha kuanguka kwa mawaziri watatu akiwamo aliyekua Waziri Mkuu, Edward Lowassa.