BOT lazima kieleweke - Asema Seif Sharif Hamad / Awaited Zanzibar President | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BOT lazima kieleweke - Asema Seif Sharif Hamad / Awaited Zanzibar President

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwiba, Sep 21, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  MGOMBEA urais wa Chama cha Wananchi (CUF) visiwani hapa, Maalim Seif Sharif Hamad amesema akichaguliwa kuingia Ikulu, atahakikisha Zanzibar inapewa mgawo wa asilimia 11.02 badala ya 4.5 inayopewa na Benki Kuu ya Tanzania(BoT).
  Pia, amesema atafuatilia matatizo na malalamiko mengine ili kupata haki zote ambazo Zanzibar inastahili kuzipata kutoka BoT na kuhakikisha uadilifu wa utendaji wa benki kuu unatendeka.
  Aliyasema hayo jana visiwani hapa katika mkutano wake na waandishi wa habari, ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kukutana nao kila wiki kufafanua kipengele kimoja cha ilani ya CUF, ambapo alikutana nao kujadili masuala uchumi.
  “Nitafanya mazungumzo na serikali ya muungano wa Tanzania kwa lengo la kuitangaza Zanzibar kama ni ‘off-shore banking and off-shore companies centre’ kwa lengo la kuifanya kuwa kama kituo cha huduma katika eneo la Afrika Mashariki.
  “Nitahakikisha inapewa mgawo wa asilimia 11.04 badala ya asilimia 4.5 inayopata hivi sasa kutoka BoT,” alisema Maalim Seif.
  Alifafanua kwamba Zanzibar inastahili kupata asilimia 11.04 kutokana na kwamba ilitoa hisa ya asilimia hizo katika uanzishwaji wa benki kuu.
  Kuhusu ajira Maalim Seif alisema atahakikisha anaweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika viwanda, kukuza utajiri wenye tija ili kuchangia ukuaji wa pato.
  “Tutaanzisha vyuo maalumu vya kutoa elimu ya amali ili kuwawezesha vijana wanaomaliza shule na wasiokuwa na kazi kuingia katika soko la ajira lenye tija na mustakabali mzuri,” alisema
  Kuhusu kukuza uwekezaji, maalim Seif alisema atarekebisha sheria ya uwekezaji iwe bora na kuimarisha utekelezaji wa kweli uwavutie wawekezaji.
  Alisema kuwa ataunda mamlaka moja ya uwekezaji itakayokuwa na dhamana ya kukuza na kusimamia uwekezaji.
  “Tutaanzisha benki ya biashara Zanzibar ambayo itakuwa ikitoa mikopo kwa lengo la kuwainua wawekezaji wa ndani ili waweze kuwekeza na kutoa mchango katika pato la taifa sambamba na kutoa ajira kupitia miradi itakayoanzishwa na benki hii,” alisema
  kuhusu uondoshaji wa umaskini, Maalim Seif alisema ataanzisha miradi mipya yenye kujielekeza kuanzisha ajira kwa vijana.
  Aliahidi kusambaza huduma zote muhimu za kiuchumi hasa maji na umeme sambamba na vitega uchumi katika visiwa vyote vya ndani katika kipindi cha miaka mitano lengo likiwa ni kuwabakisha wananchi katika maeneo yao.
  “Serikali ya CUF itawapa kila motisha unahohitajia Wazanzibar waliopo nje ili walete nyumbani akiba zao na kuwahakikishia usalama wa mali zao,” alisema Maalim seif na kuongeza; “kitengo kitakachosimamia hayo kitakuwa chini ya rais.”
  Kuhusu mfumo wa mapato yatokanayo na kodi, alisema serikali yake itafanya mazungumzo ya haraka na serikali ya muungano kwa lengo la kusawazisha kasoro na kuweka mfumo wa kodi unaonufaisha zanzibar na watu wake.
  “Tutafanya mazungumzo ya kuangalia uwezekano wa TRA kuiachia bodi ya mapato ya Zanzibar(ZRB) ambayo imeonyesha ufanisi mkubwa katika utendaji wake wa kazi, dhamana ya kukusanya mapato na kodi zote za ndani,” alisema
  Akiongelea usimamizi wa mapato ya umma na utumishi serikalini, alisema jambo la kwanza atahakikisha wafanyakazi wastaafu hewa wote wanaondoshwa katika orodha ya malipo na mafao.
  Alisema kuwa atawastaafisha wafanyakazi waliopitiliza muda wao wa kustaafu pamoja na kuwalipa mafao yao kwa kiwango kipya cha juu zaidi muda mfupi baada ya kustaafu.
  “Serikali itatoa mishahara maalumu ya kuvutia wataalamu ili waweze kuja na kubakia kufanya kazi Zanzibar,” alisema
  Akizungumzia suala la nguvu kazi, alisema atarekekibisha na kutekeleza sheria na taratibu zitazopelekea utumiaji mzuri wa nguvu kazi ikiwa ni pamoja kuweka mfumo mzuri wa maslahi kwa wafanyakazi.
  “Tutaunda na kutekeleza mpango unaofaa kwa mafunzo ya kazini na katika taasisi za elimu. Tutasimamia sekta binafsi kulinda maslahi ya wafanyakazi na kuhakikisha sheria zilizowekwa zinafuatwa,” alisema
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Maalim Seif aahidi kujenga vyuo vya michezo Z'bar


  [​IMG]MGOMBEA urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad amesema akiingia Ikulu atahakikisha anaendeleza sekta ya michezo kwa kujenga vyuo mahsusi kwa ajili hiyo.
  Akizungumza jana visiwani hapa katika mkutano wake na waandishi wa habari, ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kila wiki, alisema hatua yake hiyo ni sehemu yake ya mkakati wa kuendeleza vijana kiuchumi.
  "Michezo ni ajira, ukiwaendeleza vijana wenye vipaji kwa kupata mafunzo maalumu katika michezo mbalimbali, utakuwa umewainua kiuchumi wao binafsi pamoja na wa Zanzibar," alisema.
  Aliongeza; "Katika hili nitahakikisha vinaanzishwa vyuo mbalimbali maalum kwa ajili ya michezo ikiwa ni pamoja na kuleta wataalam katika fani hiyo."
  Katika mkutano huo ambao Maalim Seif alikuwa akizungumzia mkakati wake wa kuinua uchumi, alisema pamoja na mambo mengine, atahakikisha visiwa hivyo vinakuwa kinara duniani katika michezo hasa mpira wa miguu.
  Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CUF, Septemba 16 mwaka huu, katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja, Maalim Seif aliahidi kuiingiza Zanzibar katika Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa.
  Pia, aliahidi kujenga viwanja vipya vya kisasa vya michezo katika kila mkoa ikiwamo viwanja vya ndani.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nilifikiri atavunja Muungano kumbe ataenda BOT kudai vijisenti?
   
 4. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  KWELI...! VUNJA MUUNGANO....YAKHEEEEEE...! naipenda cuf kwa hilo tu.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Sep 21, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Anatafuta sababu za kudai eti Muungano hauna faida! Hiyo 11.04% ameipataje?
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  Mwiba,

  ..Maalim Seif kama yuko serious angedai Zenj iwe na Central Bank na sarafu yao wenyewe.

  ..Zenj inapaswa kuwa na mamlaka yake ya kodi tofauti kabisa na TRA. ila baada ya hapo bidhaa zinazoingia Tanganyika kutoka Zenj zilipiwe kodi kama bidhaa zinazotokea sehemu yoyote ile.
   
Loading...