BoT: Hatua za kisera kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa Sekta Binafsi na kupunguza viwango vya riba

Ukiusoma huo mwongozo vizuri,unawapa mabenki uhuru wa kuamua kufuata hayo masharti au lah-we have a very long way to go.Njia thabiti ni mabenki yenyewe kulazimishwa na hali ya soko kushusha riba.Kiuhalisia riba za Tanzania ni kubwa mno mno.

Mkuu hali ya soko itasukuma mabenki kushusha riba. Watu siku hizi hawaangalii jina la benki unakoweka pesa zako, wanachofuata ni huduma wanayotaka kama inapatikana.

Leo hii benki yeyote ikishusha riba, watu wataambizana tu kwamba kuna benki wana riba ndogo za mikopo, watu watakimbilia huko, hiyo italazimisha benki zingine zishushe kunusuru kukimbiwa na wateja.

Ikiwa mtu hana ulazima wa kukopa sasa hivi bora akasubiria kidogo hadi mwakani hizi sheria na taratibu zikianza kutumika, unaweza kukopa sasa hivi ukapigwa riba ya sasa baadae wakija kubadili unaendelea kulipa mkopo kwa ile ile riba ya zamani.

Ilinikuta hii nilikua nalipa 22.5% wakati benki walishusha hadi 16%. Na walikua wananibembeleza nichukue tena nikawaambia nikitaka ntaenda tena. Kwa hii habari, tutaonana mwakani tena ikishakua 10%.
 
Kwa hatua hii, hapa Serikali imeonesha nia kweli ya kuongeza pesa mtaani.

Kama riba ya Benki Kuu imeshushwa hadi 3% kwa ajili ya ku support Taasisi za Kifedha ikiwemo Mabenki ya kibiashara, kwanini Benki hizi hazishushi hizo Riba kwa Wateja wao??

Unakuta Mabenki bado wana ng'a ng'ana na riba ya 17 hadi 16%, Naomba Serikali itoe maagizo haya Mabenki yashushe Riba kufikia 8% angalau.

Kama wao wanapewa Riba 3% kwanini washindwe kutoa hizo 8%. Faida ya 5% hiyo mbona inatosha.

Niipongeze serikali kwa kuchukua hatua madhubuti ili kuziongezea Bank uwezo wa kukopesha wananchi

Nionavyo mimi

1. Kwanini Bank zisishushe riba - nakubaliana na wewe kwamba inabidi riba zishuke ila kwa jinsi Benki zinavyo operate sidhani kama zinaweza kushusha riba overnight ukumbuke Banks pia inalipia baadhi ya deposits kupitia fixed deposits, call deposits and other arrangements kwa hiyo hizi meausures zitasaidia benki ku adjust over time

2. Benki zikiwa na pesa ya kukopesha innabidi pia zipate wanachi wanao kopesheka na kimsingi wanao hitaji mikopo ni wengi lakini walipaji ni wachache , serikali ingeenda mbali zaidi kurahisisha pia utaratibu wa kufanya biashara ikiwemo kupunguza mlolongo wa vibali na leseni , misamaha ya kodi kwa biashara changa zenye chini ya mwaka mmoja,

3.Kuongeza kasi ya urasimishaji wa biashara ..kuunganisha vitambulisho vya Hayati Magufuli na vitambulisho vya NIDA ili kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi na kufikia walipaji kodi wengi zaidi maana tatizo lingine kubwa walipaji kodi ni wachache sana

4.Kuweka viwango vya kodi rafiki - mtu atakopa nna kufanya biashara na akipata faida na viwango vya kodi vikawa rafiki watu wengi zaidi watalipa kodi na serikali kupata stahiki zake lakini pia wakopaji kupata uwezo wa kurejesha mikopo
 
Ahsante sana Prof Luwoga na timu yako kwa kuliona hilo, sasa mnapaswa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa maelekezo hayo.

tusitoe maelekezo halafu tukajigungia maofisini, tunapaswa kufuatilia.

Riba pia Zishuke ili watu waweze kujikwamua.
 
Benki kuu ni regulator na ndiye anayeset riba ya base point. Nadhani enki zinacharge kufuatana na riba inayotolewa na benki kuu. Kama riba inayowakopesha ni ndogo lazima benki zitashusha riba. Ila benki nyingi hawana mitaji ya kutosha wakati demand ya mikopo ni kubwa sana, ndiyo maana riba ni kubwa. Pia riba inayotozwa kwenye amana ni kubwa hivyo benki nyingi hazikopeshi bali hununua amana za serikali na hii inazidi kupunza fedha ambazo zingetolewa kama mikopo kwa watu binafsi. hence riba kuwa kubwa kwa mikopo. Solution ni riba za bonds ba treasury bills zishushwe ili mabenki yapendelee kukopesha kwa watu binafsi badala ya kufanya biashara na serikali. Hii ni ngumu kutekelezeka maana serikali ina uhitaji mkubwa wa fedha hivyo lazima itakopa tu, so sijui itakuwaje. Tusubiri tuone.
BoT wanasema watazikopesha hizi benki 1Trillion kwa riba ya 3% ili zitekeleza mpango huu wa kushusha riba.

Kama maelezo yako ni sahihi,je kauli yao hii ni changa la macho?
 
Nadhani sheria ya Tanzania haijaipa mamlaka benki kuu kuzilazimisha benki za biashara kushusha riba mpaka % flani,but ina power kubwa ya ku-influence riba kupitia policy zake kwenye soko Example.Let's say NMB,TPB, & TIB zikakubaliana na hzo policy za Benki kuu kwa kukubali kukopa kwenye huo mfuko wake kwa 3% ili ziweze kukopesha kwa 10% or less-automatically zitavutia wateja wengi kutoka mabenki mengine na hivyo ili mabenki mengine yaweze kushindana yatalazimika kushusha riba ili kukabiliana na hali ya soko.
Naunga mkono.

Tatizo sio BOT kutoa WARAKA ila shida ipo kwenye utekelezaji na kusimamia walichoandika kwenye huo WARAKA.

Je hizi 1 trillion ni tofauti na alizosema waziri wa fedha ili kuongeza mzunguko wa pesa mtaani?
 
BENKI KUU YA TANZANIA

Barabara ya Jakaya Kikwete​

S. L. P. 2303 40184 DODOMA​

TANZANIA
Simu: +255 26 2962586
Barua Pepe: botcommunications@bot.go.tz BANK OF TANZANIA
16 Jakaya Kikwete Road P.O. Box 2303
40184 DODOMA TANZANIA
Phone: +255 26 2962586
Email: botcommunications@bot.go.tz

TAARIFA KWA UMMA​

Hatua za kisera kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza viwango vya riba

Kwa muda mrefu, hali ya uchumi wa Tanzania ilikuwa imara na thabiti, kabla ya kuathiriwa na janga la UVIKO-19 kuanzia mwaka 2020. Uchumi ulikua kwa wastani wa asilimia 6.7 katika kipindi cha 2010-2019, na mfumuko wa bei ulikuwa ukipungua hadi kufikia wastani wa asilimia 3.8 mwaka 2019. Mikopo inayotolewa na benki za biashara kwa sekta binafsi ilikua kwa asilimia 15, wakati riba za mikopo zilikuwa zikishuka hadi asilimia 17 kutoka zaidi ya asilimia 20.

Janga la UVIKO-19 limeathiri shughuli za kiuchumi, kutokana na nchi zinazofanya biashara na Tanzania kuchukua hatua kudhibiti kuenea kwa UVIKO19, ikiwemo vizuizi vya kusafiri. Kwa sababu hiyo, Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kupunguza athari za janga hilo katika shughuli za kiuchumi na kuchochea ukuaji wa uchumi. Pamoja na hatua hizo, kasi ya ukuaji ilipungua hadi kufikia asilimia 4.8 mwaka 2020 kutoka asilimia 7 kwa mwaka uliotangulia. Ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi pia ulipungua, kufikia ukuaji wa kati ya asilimia 2.3 hadi asilimia 9.1. Viwango vya riba kwa mikopo inayotozwa na benki za biashara vimeendelea kuwa juu, kwa wastani wa asilimia 17, licha ya ongezeko la ukwasi na hatua zingine zilizochukuliwa.

Ili kutoa msukumo mkubwa wa kuongeza kasi ya mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza riba, na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kutekeleza hatua za kisera zifuatazo, kuanzia tarehe 27 Julai 2021:

Kupunguza kiwango cha sehemu ya amana za mabenki kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu (Reduction of statutory minimum reserve requirement-SMR). Benki Kuu imetoa unafuu kwa benki za biashara kwa kupunguza kiwango cha kisheria cha amana ambacho benki na taasisi za fedha zinatakiwa kuweka Benki Kuu, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza sera ya fedha. Nafuu hii itatolewa kwa benki itakayotoa mikopo kwa sekta ya kilimo kulingana na kiasi cha mkopo kitakachotolewa. Aidha, benki itakayonufaika itatakiwa kutoa mikopo kwa sekta ya kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka. Hatua hii inalenga kuongeza mikopo katika sekta ya kilimo,na kupunguza riba katika mikopo itakayotolewa.

Kulegeza masharti ya usajili wa mawakala wa benki (relaxation of agent banking eligibility criteria). Benki Kuu ya Tanzania imeondoa sharti la uzoefu wa kufanya biashara kwa angalau miezi 18 kwa waombaji wa biashara ya wakala wa benki. Badala yake, waombaji wa biashara ya wakala wa benki watatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Kitambulisho cha Taifa. Hatua hii itachangia kuongeza fedha katika mabenki kutokana na ongezeko la amana na kupunguza riba za mikopo.

Ukomo wa riba kwenye akaunti za makampuni ya watoa huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi (Limitation of interest rate paid on mobile money trust accounts). Benki Kuu imeweka ukomo wa kiwango cha riba kinachotolewa na benki za biashara kwenye akaunti za makampuni yanayotoa huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi. Riba itakayotolewa kwenye akaunti hizi haitazidi riba itolewayo na benki husika katika amana za akiba (savings deposit rate). Hatua hii inalenga kupunguza gharama za upatikanaji wa fedha kwa benki zinazotumika kukopesha, hivyo kuchangia kupunguza riba za mikopo.

Kuanzishwa kwa mfuko maalum wa kukopesha mabenki na taasisi za fedha ili ziweze kukopesha sekta binafsi. Benki Kuu imeanzisha mfuko maalum wenye thamani ya shilingi trilioni moja ambao utatumika kukopesha mabenki na taasisi za fedha kwa riba ya asilimia 3, ili taasisi hizo ziweze kukopesha sekta binafsi. Benki au taasisi ya fedha itakayofaidika na mfuko huu itatakiwa kukopesha sekta binafsi kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka. Hatua hii itaongeza ukwasi na kupunguza riba za mikopo kwa sekta binafsi.

Kupunguza kiwango cha mtaji kinachotakiwa kuwekwa na benki za biashara kwa ajili ya kuweza kutoa mikopo (Reduction of risk weight on loans). Benki Kuu imepunguza kiwango cha mtaji kinachotakiwa kuwekwa na benki za biashara kwa ajili ya kuweza kutoa mikopo. Hatua hii itasaidia kutoa fursa kwa benki za biashara kutoa mikopo zaidi kwa sekta binafsi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Hatua hizi za kisera zimechukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, Sura. 197 na Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Sura ya 437. Benki Kuu itatoa mwongozo wa namna ya utekelezaji wa hatua hizi kwa benki, taasisi za fedha na makampuni yanayotoa huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi. Pamoja na hatua hizi, Benki Kuu inaziagiza benki za biashara na taasisi za fedha kuweka na kutekeleza mikakati ya kupunguza riba za mikopo na kuhamasisha upatikanaji wa amana.

Prof. Florens D.A.M Luoga
Gavana
BENKI KUU YA TANZANIA

27 Julai 2021​
 
Mh. Rais na Serikali kupitia BOT kweli mmeonyesha nia kubwa sana kwa vitendo ya kushusha riba ya mikopo hadi 10% au chini. Ikiwa BOT itatoa mikopo kwa mabenki ya biashara kwa 3% na mabenki ya biashara yakakopesha kwa 9% mfano, hii itainua watu wengi sana sanaa kiuchumi, ndani ya miaka 2 au 3 tangu mabenki yakianza kutekeleza maamuzi haya ya BOT basi maisha ya watanzania mamilioni yanaenda kubadilika. Na pia BOT wangesema marejesho ingechukua maximum hata 10 yrs kwa mkopaji mwenye sifa na miaka kama inaruhusu.

Yaani 9% riba, maximum time for loan repayment iwe 10 yrs, hapa serikali ya Mama Samia itabadili maisha ya mamilioni kwa muda mfupi sana.

Hongera Mh. Rais wetu Mama Samia.
 
Niipongeze serikali kwa kuchukua hatua madhubuti ili kuziongezea Bank uwezo wa kukopesha wananchi

Nionavyo mimi

1. Kwanini Bank zisishushe riba - nakubaliana na wewe kwamba inabidi riba zishuke ila kwa jinsi Benki zinavyo operate sidhani kama zinaweza kushusha riba overnight ukumbuke Banks pia inalipia baadhi ya deposits kupitia fixed deposits, call deposits and other arrangements kwa hiyo hizi meausures zitasaidia benki ku adjust over time

2. Benki zikiwa na pesa ya kukopesha innabidi pia zipate wanachi wanao kopesheka na kimsingi wanao hitaji mikopo ni wengi lakini walipaji ni wachache , serikali ingeenda mbali zaidi kurahisisha pia utaratibu wa kufanya biashara ikiwemo kupunguza mlolongo wa vibali na leseni , misamaha ya kodi kwa biashara changa zenye chini ya mwaka mmoja,

3.Kuongeza kasi ya urasimishaji wa biashara ..kuunganisha vitambulisho vya Hayati Magufuli na vitambulisho vya NIDA ili kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi na kufikia walipaji kodi wengi zaidi maana tatizo lingine kubwa walipaji kodi ni wachache sana

4.Kuweka viwango vya kodi rafiki - mtu atakopa nna kufanya biashara na akipata faida na viwango vya kodi vikawa rafiki watu wengi zaidi watalipa kodi na serikali kupata stahiki zake lakini pia wakopaji kupata uwezo wa kurejesha mikopo
Analysis makini sana.
 
Naunga mkono.

Tatizo sio BOT kutoa WARAKA ila shida ipo kwenye utekelezaji na kusimamia walichoandika kwenye huo WARAKA.

Je hizi 1 trillion ni tofauti na alizosema waziri wa fedha ili kuongeza mzunguko wa pesa mtaani?
Itakuwa ni katika mpango huo huo uliozungumziwa na Madilu.
 
Mh. Rais na Serikali kupitia BOT kweli mmeonyesha nia kubwa sana kwa vitendo ya kushusha riba ya mikopo hadi 10% au chini. Ikiwa BOT itatoa mikopo kwa mabenki ya biashara kwa 3% na mabenki ya biashara yakakopesha kwa 9% mfano, hii itainua watu wengi sana sanaa kiuchumi, ndani ya miaka 2 au 3 tangu mabenki yakianza kutekeleza maamuzi haya ya BOT basi maisha ya watanzania mamilioni yanaenda kubadilika. Na pia BOT wangesema marejesho ingechukua maximum hata 10 yrs kwa mkopaji mwenye sifa na miaka kama inaruhusu.

Yaani 9% riba, maximum time for loan repayment iwe 10 yrs, hapa serikali ya Mama Samia itabadili maisha ya mamilioni kwa muda mfupi sana.

Hongera Mh. Rais wetu Mama Samia.
Mkuu mbona unachekesha.

Unatoa pongezi kwa jambo ambalo bado halijafafanuliwa vizuri utekelezaji wake?

Unapongeza hali hiyo nzuri uliyoibeba akilini mwako na kuielezea hapa, ambayo wewe mwenyewe umeieleza kama ni ya kufikirika tu?

Imenibidi nicheke wakati nikikusoma.

Ikitokea iwe kama ulivyoielezea hapo, nami nitaungana nawe kutoa pongezi za dhati. Wakati huo bado sana.
 
Kuhusu hili la deni la mikopo ya elimu ya juu, je walifuta malimbikizo ya retention fee yote ya nyuma? Ama walishimamisha kuongezeka kwa retention fee lakini wakakutaka kulipa ile ya miezi/miaka ya nyuma iliyolibikizwa kabla ya maagizo ya Rais?
Mama anazidi kuupiga.

Alianza mikopo ya bodi ghafla nikajikuta milioni 7.8 za dhulma zimefutwa. Nilishakata tamaa deni kuisha.

Sasa benki riba zinaanzwa kupunguza kwa agizo lake. Kwa taarifa hii nmeshamuarifu fundi wa kupaua ajiandae. Rangi.

Mungu akubariki Madame President.
 
Kuna kitu hakiko sahihi katika maelezo ya Benki Kuu.

Katika aya ya pili inayoanza na maneno haya: "Janga la UVIKO-19 limeathiri bshughuli...", na kuendelea hadi kwenye maelezo ya ukuaji wa mikopo inayoeleza ifuatavyo: " Ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi pia ulipungua kufikia ukuaji wa kati ya asili mia 2.3 hadi asili mia 9.1"

Hii ina maana mikopo iliongezeka wakati wa UVIKO-19? Au ulipungua toka asilimia kubwa zaidi hadi kufikia asili mia 9.1?
Au, kabla ya UVIKO mikopo ilikuwa inaongezeka kwa asili mia 9.1, na ikashuka hadi asili mia 2.3 kutokana na kuathiriwa na janga la UVIKO-19?
 
Mkuu hali ya soko itasukuma mabenki kushusha riba. Watu siku hizi hawaangalii jina la benki unakoweka pesa zako, wanachofuata ni huduma wanayotaka kama inapatikana.

Leo hii benki yeyote ikishusha riba, watu wataambizana tu kwamba kuna benki wana riba ndogo za mikopo, watu watakimbilia huko, hiyo italazimisha benki zingine zishushe kunusuru kukimbiwa na wateja.

Ikiwa mtu hana ulazima wa kukopa sasa hivi bora akasubiria kidogo hadi mwakani hizi sheria na taratibu zikianza kutumika, unaweza kukopa sasa hivi ukapigwa riba ya sasa baadae wakija kubadili unaendelea kulipa mkopo kwa ile ile riba ya zamani.

Ilinikuta hii nilikua nalipa 22.5% wakati benki walishusha hadi 16%. Na walikua wananibembeleza nichukue tena nikawaambia nikitaka ntaenda tena. Kwa hii habari, tutaonana mwakani tena ikishakua 10%.
Nami ilinikuta.Fafizo kwenye kilimo Mazal ya Muda mrefu kama mayawa, ko ososho, vanilla mkopo haupati
 
Back
Top Bottom