BoT: Hatua za kisera kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa Sekta Binafsi na kupunguza viwango vya riba

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
2,933
2,000
Benki kuu ya Tanzania imetoa muongozo wa benki za biashara kupunguza riba kwa sekta binafsi.

Benki kuu imetenga fungu la Trilioni moja ambayo itatumika kuzikopesha benki na taasisi za fedha kwa riba ya 3% na kutaka benki zitoe mikopo kwa riba isiyozidi 10%.

Binafsi napongeza hizi hatua za serikali katika kuongeza ukwasi na mzunguko wa pesa mitaani. Riba kwenye mabenki ya biashara iko juu sana.

20210727_121117.jpg
20210727_121120.jpg
20210727_121134.jpg
20210727_121137.jpg
 
Attachments

 • File size
  150.6 KB
  Views
  9
 • File size
  157 KB
  Views
  7

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
6,124
2,000
Mama anazidi kuupiga.

Alianza mikopo ya bodi ghafla nikajikuta milioni 7.8 za dhulma zimefutwa. Nilishakata tamaa deni kuisha.

Sasa benki riba zinaanzwa kupunguza kwa agizo lake. Kwa taarifa hii nmeshamuarifu fundi wa kupaua ajiandae. Rangi.

Mungu akubariki Madame President.
 
John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
1,677
2,000
Sector iliyopunguziwa kuwa chini ya asilimia kumi ni kilimo
kwa nini wao bot wasikopeshe
Sasa benki kuu ikikopesha sekta binafsi,taasisi za kibiashara zitafanya kazi gani? Naona hapa riba ya 10% inagusa pia na mikopo mingine kiujumla-Anyway,bado naona utekelezaji huu utachukua muda maana mapendekezo haya ya kisera juu ya hizi taasisi kupunguza riba yamekaa ki hiyari zaid (Optional)
 
Renegade

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
6,174

Asilimia 7% Inatosha kufanya biashara, kwa maana nyingine hili ni lazimisha la kushusha riba kuwa 10% kwa benki zote.
 
John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
1,677
2,000
Asilimia 7% Inatosha kufanya biashara, kwa maana nyingine hili ni lazimisha la kushusha riba kuwa 10% kwa benki zote.
Ukiusoma huo mwongozo vizuri,unawapa mabenki uhuru wa kuamua kufuata hayo masharti au lah-we have a very long way to go.Njia thabiti ni mabenki yenyewe kulazimishwa na hali ya soko kushusha riba.Kiuhalisia riba za Tanzania ni kubwa mno mno.
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,936
2,000
Hii ni jambo zuri sana na litasaidia kukuza uchumi.

Madhara ya benki kutoza riba kubwa kwenye mikopo. Inashawishi wafanya biashara ku cut corners na kutoa rushwa.
Lazima ukwepe kodi au uchimbe shimo la choo cha serikali kwa milioni 100 ndio uweze kurudisha mkopo na upate faida!!
 
gwankaja

JF-Expert Member
May 16, 2011
7,781
2,000
Ukiusoma huo mwongozo vizuri,unawapa mabenki uhuru wa kuamua kufuata hayo masharti au lah-we have a very long way to go.Njia thabiti ni mabenki yenyewe kulazimishwa na hali ya soko kushusha riba.Kiuhalisia riba za Tanzania ni kubwa mno mno.
Ni kubwa na hazilipiki.. ndo maana watu wengi wanashindwa kulipa na biashara zinakufa!
 
Katwangilo

JF-Expert Member
Jun 10, 2021
446
500
Mama anazidi kuupiga.

Alianza mikopo ya bodi ghafla nikajikuta milioni 7.8 za dhulma zimefutwa. Nilishakata tamaa deni kuisha.

Sasa benki riba zinaanzwa kupunguza kwa agizo lake. Kwa taarifa hii nmeshamuarifu fundi wa kupaua ajiandae. Rangi.

Mungu akubariki Madame President.
Mzee salary za mwezi huu zimetoka? Na je kama zimetoka mfumo umekaaje braza
 
Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
2,299
2,000
Kwa hatua hii, hapa Serikali imeonesha nia kweli ya kuongeza pesa mtaani.

Kama riba ya Benki Kuu imeshushwa hadi 3% kwa ajili ya ku support Taasisi za Kifedha ikiwemo Mabenki ya kibiashara, kwanini Benki hizi hazishushi hizo Riba kwa Wateja wao??

Unakuta Mabenki bado wana ng'a ng'ana na riba ya 17 hadi 16%, Naomba Serikali itoe maagizo haya Mabenki yashushe Riba kufikia 8% angalau.

Kama wao wanapewa Riba 3% kwanini washindwe kutoa hizo 8%. Faida ya 5% hiyo mbona inatosha.
 
samakinchanga

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
1,717
2,000
watu wa mabenki mje hapa mtujibu kwanini nyie mmepunguziwa asilimia lakini wateja binafsi bado mmekomaa asilimia kubwa yaani 17,16 why
 
John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
1,677
2,000
Kwa hatua hii, hapa Serikali imeonesha nia kweli ya kuongeza pesa mtaani.

Kama riba ya Benki Kuu imeshushwa hadi 3% kwa ajili ya ku support Taasisi za Kifedha ikiwemo Mabenki ya kibiashara, kwanini Benki hizi hazishushi hizo Riba kwa Wateja wao??

Unakuta Mabenki bado wana ng'a ng'ana na riba ya 17 hadi 16%, Naomba Serikali itoe maagizo haya Mabenki yashushe Riba kufikia 8% angalau.

Kama wao wanapewa Riba 3% kwanini washindwe kutoa hizo 8%. Faida ya 5% hiyo mbona inatosha.
Nadhani sheria ya Tanzania haijaipa mamlaka benki kuu kuzilazimisha benki za biashara kushusha riba mpaka % flani,but ina power kubwa ya ku-influence riba kupitia policy zake kwenye soko Example.Let's say NMB,TPB, & TIB zikakubaliana na hzo policy za Benki kuu kwa kukubali kukopa kwenye huo mfuko wake kwa 3% ili ziweze kukopesha kwa 10% or less-automatically zitavutia wateja wengi kutoka mabenki mengine na hivyo ili mabenki mengine yaweze kushindana yatalazimika kushusha riba ili kukabiliana na hali ya soko.
 
chase amante

JF-Expert Member
Feb 24, 2018
5,005
2,000
Aharakishe utoaji wa namna ya kutekeleza hizo sera kwa benki na kampuni zinazotoa Huduma ya kifedha kwa mitandao ya simu.

Huenda, tukapunguziwa makato ya miamala.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom