BOT boresheni mwonekano wa fedha za Tanzania kuhamasisha watafutaji

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Ukichunguza mwonekano wa pesa zetu kuanzia coin mpk noti, kweli hazivutii kwa mtafutaji kuzitafuta kisawasawa.

Tanzania ina vitu vingi sana (current) kama rasilimali nzuri sana zinazoitambulisha nchi yetu. Tuna gase, tuna water falls, national parks, madini, watu nk ambao tunaweza kudesign tukapachika kwenye hela zetu,siyo kila kitu Mlima Kilimanjaro, twiga na simba.

Ukitaka kumvutia mteja au mtafutaji, weka bland nzuri yenye mvuto na inayoeleweka kirahisi, na mara zote imguse huyo mtu mpk awe inspired.

BoT tunaomba muangalie namna bora zaidi ya kubadili bland ya fedha za tanzania ili muonekano wake uwavutie watafutaji, hakika tutauaga umaskini kwa speed hii tunayokwenda nayo ya hapa kazi tu.
 
Back
Top Bottom