Boss wa KQ ashauri Serikali ya Tanzania iiache ATCL - changa la macho? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Boss wa KQ ashauri Serikali ya Tanzania iiache ATCL - changa la macho?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Jun 6, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  WAKATI Tanzania inajipanga upya kufufua Shirika lake la Ndege (ATCL), Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Kenya (KQ), Titus Naikuni, amesema kama Tanzania inataka shirika hilo liendelee, Serikali yake inapaswa kujitoa katika uendeshaji.

  Akijibu jana maswali ya wandishi wa habari kutoka nchi nne wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, baada ya kuwasilisha ripoti ya utendaji wa KQ inayoishia Machi 2010, Naikuni alisema utafiti umeonesha kila mahali barani Afrika serikali ilipoingilia uendeshaji wa shirika la ndege, lilipata matatizo.

  Alifafanua kwamba, serikali inaweza kuwekeza mtaji, lakini akasisitiza kuwa hata kama ikiwekeza mtaji, lazima iache wataalamu waendeshe bila kuingiliwa na sekta binafsi itakuja yenyewe.

  Serikali ya Kenya inamiliki asilimia 23 tu ya hisa katika KQ ambayo inajipanga kuongeza safari zake katika miji zaidi ya Afrika, huku shirika la ndege la kimataifa la KLM likimiliki asilimia 26 na sehemu iliyobakia ya hisa ikimilikiwa na kampuni na watu mbalimbali duniani.

  Wiki mbili zilizopita, serikali ilishauriwa kuivunja ATCL na kuanza upya kama ilivyofanyika katika Shirika la Bima la Taifa (NIC), kwa madai kuwa shirika hilo limekuwa likichukua fedha za Serikali kuliko kutoa matumaini ya kukua.

  Wakati KQ inayomiliki ndege 28 kwa sasa, ikijipanga kuagiza ndege nyingine tisa ambazo ni kubwa aina ya Boing 787 na isipozipata, imeshaanza kutafuta mbadala wa kufikia lengo hilo kwa kupata ndege aina ya Airbus 330 ifikapo mwaka 2013, ili pamoja na mambo mengine, liwe shirika kubwa la ndege barani Afrika. ATCL ina ndege moja ambayo inasuasua.

  Naikuni alipoulizwa iwapo KQ, ambayo imepata faida baada ya kodi licha ya soko la huduma za ndege kuathiriwa na mtikisiko wa uchumi duniani, itakuwa tayari kushirikiana na Tanzania kuifufua ATCL, alishauri ushirikiano huo uanze kwanza kati ya kampuni ya Precision kabla ya KQ.

  "Sisi tuko tayari kwa ushirikiano na shirika lolote, lakini kwa nini mnawaza kushirikiana na KQ badala ya kushirikiana na Precision ambayo iko nyumbani?," alihoji.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Precision, Alfonse Kioko ambayo asilimia 49 ya hisa za shirika analoliongoza zinamilikiwa na KQ, alisema wako tayari kwa mazungumzo ya kuifufua ATCL.

  Hata hivyo, alitaka Watanzania waione Precision kama shirika la pili la kitaifa baada ya ATCL, kwa kuwa linamilikiwa kwa sehemu kubwa na Watanzania na limeajiri Watanzania wengi zaidi ya wageni.

  Chanzo: Gazeti Habari Leo.

  My take:

  Katika sakata hili hapa naona wale wenye nia yao ya kuua kabisa ATCL ndo naona wanajipanga taratibu. Binafsi sikubaliani na ushauri wa huyo boss wa KQ kwamba ATCL ishirikiane na Precision air kwani hawa hawa KQ wanamiliki 49% ya precision air na kama wajinga wetu wa CCM wakiingia mkenge huu basi bora tusiwe na shirika la ndege kabisa.

  Mbona kabla ya Mkapa na basil mramba shirika lilikuwa tishio ktk ukanda huu? ATC ya wakati ule ilikuwa mpaka inaruka kwenda New Delhi, SA n.k. kwa nini leo iwe hivyo? Tunajua Basil mramba na wenzake wana hisa precision air. Mimi nashauri kama ni kuvunja wavunje lakini lianzishwe shirika jipya na wafanyakazi wapya na wabia wapya na siyo kuungana na watu walioshiriki kuua ATCL.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Biashara ya ndege inahitaji watu dedicated, wenye malengo na wenye maamuzi. Kwa dunia ya sasa inayokwenda haraka, serikali yetu mfu ambayo haiwezi kusimamia lolote kuendelea kujiingiza huku ni kuunguza fedha za wavuja jasho. Iachie watu binafsi au itafute mtaji na kuuza hisa baadae.
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  MKuu Lakini unaonaje ushauri wa huyo boss wa Kenya airways
   
 4. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ama kweli umaskini tabia na wakenya will never change ina maana kumbe huyo tapeli mwingine nae anajifanya sitaki kumbe nataka akijua wana hisa yao tayari huko kwenye 'Precision air' anasubiri serikali ichukue 'ATCL' iungane na upande wa biashara yao nyingine. Halafu tax payers money zitupwe huko wao waendelee kuifanya Tz shamba la bibi, si ajabu biashara yenyewe ifeli vile vile i doubt kama watabadilisha namna ya uendeshaji wake uliowafikisha hapo in the first place.

  Tuna kazi kubwa na inavyooneka serikali yetu au washauri wake yote ni mijitu mijizi si ajabu haya mashirika mengi yanayo wekeza Tz somehow kuna vigogo wenye hisa. Kwa wao mradi serikali itupe hela wajichotee kama walivyoua mashirika ya ndani yaliyokuwako tangia zama hizo, serikali yetu inachojua ni kutupa hela tu bila ya kujali kama itarudi au la; duuh.

  This idiocy needs to stop kwa kweli serikali inabidi iache huu upuuzi ingawa mimi ni mshabiki wa capitalism lakini hii si sawa. Amna wawekezaji wenye good intention so far kwetu inavyoonekana everywhere i read the government throws money hila atusikii wakipata faida kwani mashirika yote uhishia kuboronga tu.

  Hatua za kuchukua in my opinion kwanza serikali aina budi zaidi ya kuendeleza biashara zake na kufufua viwanda vyote au makampuni yote yanayo sua sua na kuongeza ajira nchini. Yaani kusiwe na share holder hata mmoja in the beggining, kote kwenye migodi, viwandani na mashirika mengine yote na tuache hizi tabia za kusema wahindi ndio wanaweza tuletea ufundi au namna ya kuendeleza hizi biashara tena wahindi njaa kama 'wabangladeshi' au hata hao bombay.

  Pili serikali inapoona inahitajika expertice fulani ambayo kwetu kuna uhaba ianze kutoa full scholarship na iombe nchi zilizoendelea kupata patnership flani hivi kwenye trainings. Si lazima europe hata south africa au china watu waende pewa 'work experience' huko hili haya makampuni yawe yanaongozwa na watu wanaojua wanachokifanya (sio longolongo kama za gavana wetu na waziri wetu wa fedha).

  Tatu serikali iakikishe haya mashirika yanatoa faida kabla ya kufikiria kuyaweka kwenye mikono ya wawekezaji. Na si kwa namna ya sasa inabidi serikali ianze na kuuza hisa za hizi kampuni kupitia 'Dar Stock Exchange' hili kuwe na wahusika wengi na kutoa tabia ya vigogo kujifanya wao ndio wanao stahili hizi hisa. Watu wengi wataangalia mwelekeo na maslahi yao.

  Kupitia ununuaji wa hisa mpaka wawekezaji wakweli watokee na kuanza kununua hizi hisa kwa ukubwa mwisho tutampata mwekezaji wakweli atakae kua analinda maslahi na biashara ifanye kazi kama biashara zingine zozote bila ya serikali kuwa mzamini. Kwani amna mwandawazimu atakaewekeza kwenye risk business.

  lakini zote hizo zitakuwa ni kazi bure bila ya kuuwa rushwa, rushwa ni adui waki na rushwa ni adui wa maendeleo mpaka tutapojifunza hilo.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha sana mkuu kuona kama hatuna wasomi au labda ni wizi tu?
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ushauri nikizingatia hali ya sasa ambapo kila kitu kipo shaghalabaghala ni vema pesa ya wavuja jasho isipelekwe huko. Nukta.
   
 7. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu,
  Sisi watanzania tuna matatizo na tukiambiwa udhaifu wetu tunakuwa wakali sana. Kama hatuwezi kuyatambua mapungufu yetu na kuchukua hatua za dhati kujirekebisha tutaendelea kuwa na matatizo wakati wenzetu wanaendelea.
  Kwa wale ambao hawafahamu ni kuwa 1977 baada ya kuvunjika kwa EAC, [wakati ule tulikuwa na uhusiano mzuri sana na serikali ya udachi]
  Shirika la KLM lilitoa pendekezo serikalini la kujenga mahusiano ya karibu na ATC katika uongozi, mafunzo nk. Tatizo likaja wataalam wetu hasa walio toka EAA walishauri serikali isikubali ushirika huo kwani ATC ilikuwa na wataalam wa kutosha kuliendesha. Matokeo yake KLM walikwenda Kenya na hivi leo ndiyo mnaona shirika la KQ [ambalo liliundwa katika kipindi kimoja na ATC]ni moja kati ya mashirika bora afrika. Na vilevile kwa wanaokumbuka wakati precision inaanza lilikuwa shirika dogo tu na halikuwa tishio kabisa kwa ATC lakini leo kutokana na ubia na KQ na kupitia shirika hilo ubia na KL limekuwa shirika kubwa na lakuaminika na ninaamini litaendelea kuwa tishio kwa ATC kama mambo tutayaangalia kisiasa na/au faida za muda mfupi.
  Kwa kusema hivyo siyo kama ninapendekeza ubia na KQ la hasa lakini ili shirika letu liende mbele vizuri, ni budi kama alivyopendekeza CEO wa KQ kuwa baada ya kuwekeza, serikali isijiingize kwenye utendaji na litakapo anza kusimama shirika liwekwe kwenye DSE kwa serikali kupunguza hisa zake na kuruhusu wawekezaji wandani na nje wawekeze kuongeza mtaji na baada ya hapo shirika hilo liwajibike kwa wanahisa. Ajira kwenye shirika hili kwa kuanzia ziwe wazi kwa wataalamu wa ndani na nje ninaamini ikifanyika hivi shirika hili litapaa lakini vinginevyo litaendelea kula pesa za walipa kodi na viongozi kula hizo pesa kwa safari na vikao visivyokuwa na tija.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hoja yako nimeelewa kiasi.

  Tatizo nilionalo ni kwamba kama shirika eventually litakuja kuhodhiwa na watu binafsi, say WAGENI na waTz, kuna haja gani ya serikali kuhangaika kupata huo mtaji? (Nadhani ndio hoja ya Br. Juma hapo juu). Niko very skeptical na hii dhana ya uwekezaji, kwamba tunadhani uchumi utakuwa kwa kukaribisha kila kitu kishikwe na mgeni. Hii dhana ni mfu, kama mweleko wenyewe ndio hio basi hatufiki popote.
   
Loading...