Boss Mchina anavyotuhangaisha sababu ya Corona na kuonesha ubaguzi kipindi hiki kigumu

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,353
11,492
Anaandika Sodonkwi Chande

"Mimi ni mfanyakazi kampuni mmoja ya wakandarasi ya Kichina shughuli zangu mara nyingie hutuweka ofisini na pia kwenda site na viongozi wetu ambao asilimia 75 ni Wachina, then ndio tunakuja sisi mainjinia Waswahili.

Toka last week jamaa alianzisha utaratibu wa kuwa dereva awe anatuchukua sisi tunaoshinda wote na Wachina kutupeleka makwetu na kuturudisha.

Nliuliza why hilo, hii care imeanza lini, ndio kuja kugundua kuwa anasema "Nyie Waafrika corona haiwaui msije mkapata huko mkaja kutuambukiza sisi" kumbe suala lilikuwa ni kujiepusha wao na si kutuepusha sisi kwa corona.

Tukagoma wote kwa kuwa ni mwaka wa tatu huu jamaa hawajatuongeza salary kabisa na watu wakidai mmoja mmoja anafukuzwa, tukashauriana kuwa tupo mainjinia 7 wa Kibongo tunataka katika salary aongeze Tsh 200,000. Suala la usafiri liwe juu yetu ili kila mtu aje na gari lake na si daladala au lift ya ofisi.

Tulikubaliana na kumwambia mwajiri hatutaki panda hiyo gari ya ofisi tubanane kama ndizi ituzungushe sehemu mbalimbali kurudi majumbani atuongeze kimkataba salary ya Tsh 200,000 au atupe likizo but hatutapanda gari la ofisi kwa kipindi hiki tu then corona ikiisha watu waanze tena panda daladala.

Mgomo ulianza Jumatatu dereva akitaka kuondoka nasi tunamgomea aende mwenyewe, leo HR katuita katupa mikataba imeongezwa 200,000 kwa kila mtu na sasa kila mtu aje na usafiri binafsi; asiye nao, aidha atumie bodaboda au aiche pesa awe anachukuliwa na gari ya ofisi.

Mchina kaogopa kuondoka kwa corona na kaogopa kutufukuza kazi wote kwa pamoja. Imekuwa win-win situation. Alitaka kutubagua nasi tukaamua sasa tubaguane tu.
 
Back
Top Bottom