Boss anataka kufungua biashara kupitia kitambulisho changu. Je, kuna madhara?

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
1,230
2,000
Greetings Great Thinkers!

Nilianzisha huu uzi,

Naondoka nyumbani kwenda kutafuta maisha, naenda Iringa kwanza. Mwenye kazi au connection tafadhali na hatimaye nilifika salama.

Baada ya kukaa kwa siku kadhaa, nimekuja kupata kazi kwenye LODGE fulani hapa Iringa mjini na nina wiki kama 2 hivi tangu nianze kazi.

Kazi yangu huwa napiga usiku halafu mchana napiga vibarua vya hapa na pale.

Katika siku chache hizi, boss wangu ametokea kuniamini kwa kiasi fulani ambapo amesema kuna biashara yake anataka kuifungua ila ameniomba kitumike kitambulisho changu.

Je, hii ipoje wakuu? Ni sahihi? Nini madhara yatakayoweza kutokea labda huko mbeleni lets say nikiamua baadae kuondoka au kuacha kazi?

Naombeni ushauri & nawatangulizia shukurani!
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,877
2,000
Haya mambo bana ni magumu. Huwezi kujua anafanya mambo yepi katiba biashara yake ambayo yanakiuka taratibu za nchi za kuendesha biashara, Kwa mfano anakwepa kulipa kodi au analipa kidogo sana, Sasa siku wakimstukia unadhani ni nani atatiwa hatiani na kuwekwa lupango? Akili mkichwa.

Na mimi kuna ndugu yangu anatumia line yangu nimuachie au msala?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
1,230
2,000
Kitambulisho kipi.anataka kutumia.?

Je yeye Hana kitambulisho hicho?

Biashara yake hyo ya lodge alifungulia kitambulisho cha Nani?

Ukipata majibu ya hapo juu ndio utajua Kama n sahihi au sio sahihi kutumia kitambulisho chako

Siku njema

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Alitaka kitambulisho cha mpiga kura.

tukiachana na maswala ya kuwa anacho au hana kitambulisho.

Je, ni madhara gani yanaweza kujitokeza endapo kitatumika cha kwangu?

Je, namna nzuri ya kuukwepa huu mtego ni ipi? Maana alikwishampigia mkewe ila nikamwambia asubiri kesho tuzungumze vizuri.
 
witnessj

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
24,517
2,000
Haya mambo bana ni magumu. Huwezi kujua anafanya mambo yepi katiba biashara yake ambayo yanakiuka taratibu za nchi za kuendesha biashara, Kwa mfano anakwepa kulipa kodi au analipa kidogo sana, Sasa siku wakimstukia unadhani ni nani atatiwa hatiani na kuwekwa lupango? Akili mkichwa.
Hujanijibu swali langu mkuu

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
BOFREE

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
523
1,000
Greetings Great Thinkers!

Nilianzisha huu uzi,

Naondoka nyumbani kwenda kutafuta maisha, naenda Iringa kwanza. Mwenye kazi au connection tafadhali na hatimaye nilifika salama.

Baada ya kukaa kwa siku kadhaa, nimekuja kupata kazi kwenye LODGE fulani hapa Iringa mjini na nina wiki kama 2 hivi tangu nianze kazi.

Kazi yangu huwa napiga usiku halafu mchana napiga vibarua vya hapa na pale.

Katika siku chache hizi, boss wangu ametokea kuniamini kwa kiasi fulani ambapo amesema kuna biashara yake anataka kuifungua ila ameniomba kitumike kitambulisho changu.

Je, hii ipoje wakuu? Ni sahihi? Nini madhara yatakayoweza kutokea labda huko mbeleni lets say nikiamua baadae kuondoka au kuacha kazi?

Naombeni ushauri & nawatangulizia shukurani!

Kwanza kabisa kama kitambulisho chako kikitumika kutengeneza namba ya mlipa kodi( TIN) mazara yake ni kwamba akilimbikiza kodi unaonekana wewe ndio unadaiwa na hautakuja kufanya biashara ya kulipa kodi mpaka ulipe deni la TRA sababu mtu mmoja hawezi kuwa na TIN zaidi ya moja labda iwe kampuni

Madhara naona ni hayo tu mengne sio shida sana

Ila faida utakayookua nayo unaweza kudhulumu biashara sababu document ni zako
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,112
2,000
Na mimi kuna ndugu yangu anatumia line yangu nimuachie au msala?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Huu msala, kuna jamaa tumekutana naye mahabusu yeye kakaa siku zaidi ya 20 ndani bila dhamana alisajilia mtu laini na mhusika akawa anatapeli watu mtandaoni kupitia hiyo line na taarifa ni za mwana. Jamaa katapeli zaidi ya 60M ndipo walipofuatilia taarifa za line wakakuta ni za huyu mchizi wakajua ni yeye alienda bebwa na maafisa. Jamaa hajui lolote.

So mtu kutumia taarifa zako ni very risk.

Kuwa naye makini kama ni ndugu na kama humuamini kwa mwenendo wake fanya maamuzi chukua line yako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom