Bosi wangu kanipa mkataba wa kazi ambao ni kinyume na makubaliano halisi ya kazi

maishakujipanga

Senior Member
Feb 13, 2017
115
116
Naombeni msaada wa kisheria.

Nimeajiriwa kampuni moja private. Baada ya kufanya kazi muda mrefu bila kupewa mkataba, sasa juzi nikaletewa mkataba lakini sikuuelewa kwa sababu upo tofauti na uhalisia.

Mfano: Kabla ya mkataba nilikuwa nalipwa laki nne cash yote bila makato yoyote. Ila baada ya mkataba unaonesha nalipwa laki 2 na nusu basic salary. Na hiyo 2.5 ndo makato yote ya serikarl yanakatwa hapo.

Nilipoongea na bosi akasema nisign hiyo ya kwenye mkataba then pesa nyingine laki 1.5 nitakuwa napewa pembeni.

Je, hii ni sahii au sio sahihi?
Bado nipo njiapanda nikubali kusign au nikatae kusign.
 
Sign HARAKA USIMTIE MASHAKA la sivyo muda sio mrefu utaambulia mkataba mzuri sana unaoutaka na ulio halali kabisa LAKINA KIBARUA HAKUNA, hii ni kwa uzoefu wangu,

Ajira na mshahara source yake ni Production/Uzalishaji na SIO kwamwe Sheria na haki yako.
 
Kama ni kweli, maana yake wanakwepa kodi ya serikali. Na wewe ukikubaliana na huo mkakati, maana yake unashirikiana nao kwenye kukwepa kodi, siku likija kubumbuluka, kuna uwezekano mkubwa pia ikajulikana kuwa kuna pesa ulikua unalipwa pembeni, ambayo itakufanya na wewe mshiriki mwenza kwenye kosa la kukwepa kodi (uhujumu uchumi).

Kama ni uongo, maana yake watakua wanakudhulumu haki yako ya msingi.
Either way, sioni kama ni safe kwako, iwe kweli au iwe uongo.
 
Naona kama kuna marekebisho ya kufanya kidogo.

Kabla ya mkataba ulikuwa nalipwa laki nne cash yote bila makato yoyote.

Ila baada ya mkataba unaonesha unalipwa laki 2 na nusu basic salary. Na hiyo 2.5 ndo makato yote ya serikari yanakatwa hapo.

ulipoongea na bosi akasema usign hiyo ya kwenye mkataba then pesa nyingine laki 1.5 utakuwa napewa pembeni.

NB:
1: Hapa anakwepa kukulipia katika Mifuko ya hifadhi ya jamii maana anapaswa achangie 10% ya mshahara ambayo ni sawa na 40,000/=, na wewe uchangie kiasi hicho hicho. kwa hiyo mchango wako unapaswa uwe 80,000/= kila mwezi, sasa kama itakuwa laki mbili, basi mchango wako utakuwa 40,000/= kwa mwezi, na utakuwa unapoteza 40,000/= kila mwezi.

2: Likitibuka, utalipwa stahiki zako kulingana na kiwengo kinachoonekana kweny mtataba, 200,000/= na siyo 400,000/=
 
Naombeni msaada wa kisheria.
Nimeajiliwa kampuni moja private.

Baada ya kufanya kazi muda mrefu bila kupewa mkataba, sasa juzi nikaletewa makataba lakini sikuuelewa kwa sababu upo tofauti na uhalisia.

Mfano.
Kabla ya mkataba nilikuwa nalipwa laki nne cash yote bila makato yoyote.

Ila baada ya mkataba unaonesha nalipwa laki 2 na nusu basic salary. Na hiyo 2.5 ndo makato yote ya serikari yanakatwa hapo.

Nilipoongea na bosi akasema nisign hiyo ya kwenye mkataba then pesa nyingine laki 1.5 nitakuwa napewa pembeni.

Je, hii ni sahii au sio sahii?
Bado nipo njiapanda nikubali kusign au nikatae kusign.

Sasa hapo hujaelewa ninj?

Majitu masnitch sana

Hiyo kazi wakutimue tu usije waharibia kikampuni chao
 
Back
Top Bottom